2022
Fanya Kilicho Muhimu Zaidi
Mei 2021


“Fanya Kilicho Muhimu Zaidi,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2022.

Kikao cha Wanawake

Fanya Kilicho Muhimu Zaidi

Dondoo

Picha
bango la ubao wa mishale

Pakua PDF

Kuwa mfuasi wa Yesu Kristo kunahusisha zaidi ya kutumaini au kuamini tu. Kunahitaji juhudi, kusonga, na kuweka msimamo. Kunahitaji kwamba tufanye kitu …

Katika juhudi zetu za kufanya kitu au kufanya chochote, tungeweza kujiuliza wenyewe, “Ni nini kilicho muhimu zaidi?” …

  • Kuna “likes” ngapi tunapata katika posti zetu za mitandao ya kijamii? Au tunapendwa na kuthaminiwa kiasi gani na Baba yetu wa Mbinguni?

  • Kuvaa mtindo mpya kabisa wa nguo? Au kuonyesha heshima kwa miili yetu kwa kuvaa kwa staha?

  • Kutafuta majibu kupitia utafutaji wa intaneti? Au kupokea majibu kutoka kwa Mungu kupitia Roho Mtakatifu?

  • Kutaka vingi zaidi? Au kuridhika na kile ambacho tayari tumepewa? …

… Injili ya Yesu Kristo ni injili ya matendo na injili ya furaha! Hebu tusipuuzie uwezo wetu wa kufanya mambo yale yaliyo muhimu zaidi. Urithi wetu wa kiungu hutupatia ujasiri na kujiamini kufanya na kuwa vyote ambavyo Baba yetu wa Mbinguni anajua tunaweza kuwa. …

… Siyo tu kuhusu kufanya zaidi. Ni kuhusu kufanya kilicho muhimu. Ni kutumia mafundisho ya Kristo katika maisha yetu kadiri tunavyojitahidi kuwa zaidi kama Yeye. …

Tunapoyakita maisha yetu kwa Yesu Kristo, tutaongozwa kufanya kile kilicho muhimu zaidi. Na tutabarikiwa kwa nguvu ya kiroho, kuridhika na shangwe!

Chapisha