2022
Upendo Mtakatifu katika Mpango wa Baba
Mei 2021


“Upendo Mtakatifu katika Mpango wa Baba,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2022.

Kikao cha Jumapili Alasiri

Upendo Mtakatifu katika Mpango wa Baba

Dondoo

Picha
bango la mlima ukichomoza kupita mawingu

Pakua PDF

Katika Kanisa la urejesho la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za mwisho, tuna uelewa wa kipekee wa mpango wa Baba yetu wa Mbinguni. Hii inatupatia njia tofauti ya kuangalia azma ya maisha haya ya duniani, hukumu takatifu ambayo inafuata na hatma ya kudura yenye utukufu ya watoto wote wa Mungu. …

… Mafundisho yaliyofunuliwa ya Kanisa la Urejesho la Yesu Kristo yanafundisha kwamba watoto wote wa Mungu—isipokuwa wachache sana kuwafikiria hapa—hatimaye wataishia katika ufalme wa utukufu. …

… Iliyo juu zaidi ya hizi ni kuinuliwa kwenye ufalme wa selestia, ambapo tunaweza kuwa kama Baba yetu na Mwanaye, Yesu Kristo. …

… Kazi ya Kanisa la urejesho ni kuwasaidia watoto wote wa Mungu kustahili kwa kile Mungu anachotamani kama hatma yao ya mwisho. …

Muhimu kwetu sisi ni ufunuo wa Mungu kwamba kuinuliwa kunaweza kufikiwa kupitia tu uaminifu kwenye maagano ya ndoa ya milele kati ya mwanamume na mwanamke. Mafundisho hayo matakatifu ndiyo sababu ya sisi kufundisha kwamba “jinsia ni hulka muhimu ya utambuzi wa milele wa maisha kabla ya maisha ya duniani, maisha ya duniani na utambulisho na lengo la milele” [“Familia: Tangazo kwa ulimwengu,” ChurchofJesusChrist.org]. …

… Tunathibitisha kwamba tangazo kwa familia, lililopatikana kutokana na mafundisho yasiyobadilika, linafafanua aina ya mahusiano ya familia ambapo sehemu muhimu sana ya maendeleo yetu ya milele inaweza kutokea. …

… Ni lazima tutafute kushiriki kweli hizi za milele pamoja na wengine. Lakini pamoja na upendo tunaodaiwa kwa majirani zetu wote, siku zote tunakubali maamuzi yao. Kama nabii wa Kitabu cha Mormoni alivyofundisha, lazima tusonge mbele tukiwa na upendo kwa Mungu na wanadamu wote” [2 Nefi 31:20].

Chapisha