2022
Kuuponya Ulimwengu
Mei 2021


“Kuuponya Ulimwengu,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2022.

Kikao cha Jumapili Asubuhi

Kuuponya Ulimwengu

Dondoo

Picha
bango la Kapteni Moroni na bendera ya uhuru

Pakua PDF

Uhuru wa dini ni nini?

Ni uhuru wa kuabudu katika mifumo yake yote: uhuru wa kukusanyika, uhuru wa kuzungumza, uhuru wa kutenda kwenye imani binafsi na uhuru kwa ajili ya wengine kufanya vivyo hivyo. Uhuru wa dini unamruhusu kila mmoja wetu kujiamulia wenyewe kile tunachoamini, jinsi tunavyoishi na kutenda kulingana na imani yetu na nini Mungu hutarajia juu yetu. …

Katikati ya machafuko mnamo 1842, Joseph [Smith] alichapisha kanuni za msingi 13 za Kanisa linalokua, ikiwa ni pamoja na hii: “Tunadai haki ya kumwabudu Mungu Mwenyezi kulingana na mwongozo wa dhamiri yetu sisi wenyewe, na tunawaruhusu watu wote haki hiyo, na waabudu namna, mahali, au chochote watakacho” [Makala ya Imani 1:11].

Kauli yake ni jumuishi, yenye kuweka huru na yenye heshima. Hicho ndicho kiini cha uhuru wa dini. …

Fikiria pamoja nami njia nne ambazo jamii na watu binafsi wananufaika kutokana na uhuru wa dini.

Kwanza. Uhuru wa dini unaheshimu amri kuu ya kwanza na ya pili, ukimuweka Mungu kama kiini cha maisha yetu. …

Pili. Uhuru wa dini unachochea madhihirisho ya imani, tumaini na amani. …

Tatu. Dini inawasukuma watu kuwasaidia wengine. …

Na nne. Uhuru wa dini unafanya kazi kama nguvu ya kuunganisha na kuleta pamoja kwa ajili ya kuchagiza desturi na maadili. …

Ninawaalika muunge mkono kusudi la uhuru wa dini. Ni kielelezo cha kanuni iliyotolewa na Mungu ya haki ya kujiamulia.

Chapisha