Miito ya Misheni
Sura ya 3: Mwaliko wa Kubatizwa na Kuthibitishwa


“Sura ya 3: Mwaliko wa Kubatizwa na Kuthibitishwa,” Hubiri Injili Yangu: Mwongozo wa Kushiriki Injili ya Yesu Kristo (2023)

“Mwaliko wa Kubatizwa na Kuthibitishwa,” Hubiri Injili Yangu

Sura ya 3

Mwaliko wa Kubatizwa na Kuthibitishwa

Picha
Njoo kwenye Zizi la Mungu, na Walter Rane

Mafundisho ya Msingi

Sisi sote tu watoto wa Baba wa Mbinguni. Tumekuja ulimwenguni ili kupata fursa ya kujifunza, kukua, na kuwa zaidi kama Yeye ili tuweze kurudi kwenye uwepo Wake (ona Musa 1:39. Hatungeweza kuwa kama Yeye au kurudi Kwake bila msaada wa kiungu. Baba yetu wa Mbinguni alimtuma Mwanawe, Yesu Kristo, ili kulipia makosa yetu na kuvunja kamba za kifo (ona 3 Nefi 27:13–22).

Tunapata nguvu za Kristo za ukombozi kwa kutumia imani katika Yeye iongozayo kwenye toba, kubatizwa, kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu kupitia uthibitisho, na kuvumilia hadi mwisho. Kuweka agano la ubatizo ni hatua ya kwanza katika kujiunganisha sisi wenyewe kwa Mungu ili Roho Mtakatifu aweze kututakasa, kutuimarisha, na kubadilisha asili yetu kwa wema. Kupata uzoefu huu wa nguvu ya utakaso kunaitwa kuzaliwa upya kiroho. (Ona 2 Nefi 31:7, 13–14, 20–21; Mosia 5:1–7; 18; 27:24; 3 Nefi 27:20; Yohana 3:5.)

Kuzaliwa upya kiroho kunaanza wakati tunapobatizwa kwa maji na kwa Roho. Ubatizo ni ibada yenye shangwe na tumaini. Tunapobatizwa tukiwa na moyo uliovunjika na roho iliyopondeka, tunaanza maisha mapya kwa nguvu endelevu za Mungu. Baada ya sisi kubatizwa na kuthibitishwa, tunaweza kuendelea kuimarishwa kwa kushiriki sakramenti kwa kustahili. (Ona 2 Nefi 31:13; Mosia 18:7–16; Moroni 6:2; Mafundisho na Maagano 20:37.)

Kutoa Mwaliko

Unapohisi kuongozwa na Roho, waalike watu kubatizwa na kuthibitishwa. Hii inaweza kutokea wakati wa somo lolote.

Fundisha mafundisho juu ya ubatizo na uwasaidie watu waelewe mafundisho ya Kristo (ona somo la 3). Fundisha kuhusu umuhimu na shangwe ya agano la ubatizo, kupokea ondoleo la dhambi, na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu kupitia uthibitisho.

Waandae watu kwa ajili ya mwaliko wa ubatizo kwa kuhakikisha wao wanaelewa kile wewe unachowafundisha na agano watakalofanya. Agano la ubatizo ni kama ifuatavyo:

  • Kuwa radhi kujichukulia juu yetu jina la Yesu Kristo.

  • Kushika amri za Mungu.

  • Kumtumikia Mungu na watu wengine.

  • Kuvumilia hadi mwisho. (Ona somo la 4.)

Unaweza kushiriki yafuatayo:

“Tunapobatizwa, tunashuhudia mbele za [Mungu] kwamba [sisi] tunaingia katika agano na Yeye, kwamba [sisi] tutamtumikia yeye na kushika amri Zake.’ Tunapofanya agano hili, Yeye anaahidi kwamba ‘atatuteremshia Roho wake kwa wingi zaidi juu [yetu]’ (Mosia 18:10).”

Mwaliko wako juu ya kubatizwa unapaswa kuwa mahususi na wa moja kwa moja. Ungeweza kusema:

“Je, utafuata mfano wa Yesu Kristo kwa kubatizwa na mtu ambaye ametawazwa kufanya ibada hili? Tutakusaidia ujiandae kwa ajili ya ubatizo. Tunaamini unaweza kuwa tayari siku ya [tarehe]. Je, utajiandaa kubatizwa tarehe hiyo?”

Kama ilivyo kwa mwaliko wowote unaoutoa, ahidi baraka kubwa ambazo watu watapokea pale wanapokubali mwaliko wa kubatizwa na kushika maagano yanayohusika. Shiriki ushuhuda wako juu ya baraka hizi.

Fundisha kwamba ubatizo na uthibitisho siyo mwisho wa safari. Bali, ni sehemu katika njia ya uongofu ambao huleta tumaini, shangwe, na nguvu ya Mungu kwa utimilifu zaidi katika maisha ya mtu (ona Mosia 27:25–26). Baada ya watu kubatizwa na kuthibitishwa, wanategemea kutakaswa na Roho pale wanapoendelea katika njia ya agano.

Kama inawezekana, waalike wale unaowafundisha wahudhurie kwenye huduma ya ubatizo na mkutano wa sakramenti ambapo mtu atakuwa akithibitishwa.

Mawazo kwa ajili ya Mwaliko wa Kubatizwa

Fikiria kurejelea hadithi za kimaandiko juu ya Yesu akibatizwa (ona Mathayo 3:13–17). Ungeweza pia kuonesha video ya Biblia ikionesha ubatizo wa Mwokozi au video ya Kitabu cha Mormoni ya wafuasi wa Mwokozi wakibatiza.

Ungeweza pia kusoma hadithi ya Nefi kuhusu ubatizo wa Yesu 2 Nefi 31:4–12). Kusoma hadithi za ubatizo wa Yesu Kristo kunaweza kuwaimarisha wale wanaofundishwa.

Kujifunza Maandiko

Jifunze maandiko yafuatayo:

Andika muhtasari wa kile ulichojifunza.

Chapisha