Seminari na Vyuo
Ujumbe kutoka kwa Urais wa Kwanza


“Ujumbe kutoka kwa Urais wa Kwanza,” Kufundisha katika Njia ya Mwokozi: Kwa Ajili ya Wote Wanaofundisha Nyumbani na Kanisani (2022)

“Ujumbe kutoka Urais wa Kwanza,” Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Ujumbe kutoka kwa Urais wa Kwanza

Wapendwa akina kaka na akina dada

Ni fursa tukufu iliyoje uliyonayo kufundisha injili ya Yesu Kristo! Iwe wewe una wito au hauna wito mahususi wa kufundisha, wewe ni mwalimu. Kama mfuasi wa Bwana Mwalimu, Yesu Kristo, unazo fursa za kushiriki nuru Yake popote uendapo—nyumbani, kanisani, unapowahudumia wengine, na miongoni mwa marafiki zako. Kufundisha injili ni wajibu mtakatifu. Ni sehemu muhimu ya kazi ya Bwana, na inafanya kazi vyema zaidi tunapoifanya katika njia Yake.

Tunakualika wewe kujifunza zaidi kuhusu Yesu Kristo na jinsi Yeye alivyofundisha injili. Kwa sala jifunze maneno Yake, matendo Yake, na sifa Zake, na jitahidi kumfuata Yeye kwa karibu zaidi. Kufundisha katika Njia ya Mwokozi kunaweza kuwa mwongozo wako.

Urais wa Kwanza

Chapisha