Seminari na Vyuo
Wapende Wale Unaowafundisha


“Wapende Wale Unaowafundisha,” Kufundisha katika Njia ya Mwokozi: Kwa Ajili ya Wale Wanaofundisha Nyumbani na Kanisani (2022)

“Wapende Wale Unaowafundisha,” Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Picha
Yesu Kristo akiongea na mwanamke kisimani

Mwokozi akiwa kama mfano wetu, upendo unakuwa kichocheo cha ufundishaji wetu.

Wapende Wale Unaowafundisha

Kila kitu ambacho Mwokozi alifanya wakati wote wa huduma Yake duniani kilichochewa na upendo. Tunapojitahidi kuwa wafuasi wa kweli wa Kristo, tunaweza kujazwa na upendo huo huo (ona Yohana 13:34–35; Moroni 7:47–48; 8:26). Upendo wa Kristo unapokuwa mioyoni mwetu, tunatafuta kila njia inayowezekana ili kuwasaidia wengine kujifunza kuhusu Kristo na kuja Kwake. Upendo unakuwa kichocheo cha ufundishaji wetu.

Wapende Wale Unaowafundisha

  • Waone wanafunzi katika njia ambayo Mungu anawaona.

  • Tafuta kuwajua—kuelewa hali zao, mahitaji yao na nguvu zao.

  • Waombee kwa majina.

  • Tengeneza mazingira salama ambapo wote wanaheshimiwa na kujua michango yao inathaminiwa.

  • Tafuta njia sahihi za kuelezea upendo wako

Mwokozi Aliona Uwezekano wa Kiungu wa Kuwa katika Kila Mmoja Aliyemfundisha

Karibia watu wengi katika Yeriko walifikiri wanajua yote waliyohitaji kujua kuhusu Zakayo. Yeye alikuwa mwenye baa na mtoza ushuru—kiongozi mkubwa, kwa kweli— alikuwa tajiri. Kwa uwazi, walifikiri, hakuwa mwaminifu na mlarushwa. Lakini Yesu alitazama moyo wa Zakayo akaona mtu mwenye kuheshimika “mwana wa Ibrahimu” (ona Luka 19:1–10). Mwokozi aliona watu siyo tu kama walivyoonekana lakini kama walivyokuwa—na kama wanavyoweza kuwa. Katika wavumi wasiostahiwa kama Simoni, Andrea, Yakobo, na Yohana, Yeye aliwaona viongozi wa baadae wa Kanisa Lake. Katika mtesaji wa kuogopwa Sauli, Yeye aliona “chombo kiteule,” ambaye angeweza kuhubiri injili Yake mbele za wafalme na mataifa (ona Matendo ya Mitume 9:10–15). Na ndani yako wewe na kila mtu unayemfundisha, Mwokozi anamwona mwana au binti wa Mungu mwenye uwezekano usio na kikomo.

Miongoni mwa watu unaowafundisha, yawezekana kabisa ukawa na wengine ambao wanaonekana waaminifu na waongofu na wengine wanaoonekana kutovutiwa au hata waasi. Kuwa mwangalifu usifanye neno lisilohakikishwa kutokana tu kile unachokiona. Roho Mtakatifu anaweza kukusaidia wewe kuona ndani ya kila mtu baadhi ya vitu Mwokozi anavyoona—na kukusaidia kuanza kuwapenda katika njia anayofanya Yeye.

Maswali ya Kutafakari: Mfikirie kila mtu unayemfundisha, na tafakari jinsi Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanavyohisi kuhusu kila mmoja. Je, yawezekana Wao wanaona nini ndani yake? Ni kwa jinsi gani mawazo haya yanaathiri jinsi unavyofikiria?

Kutoka katika Maandiko: 1 Samweli 16:7; Zaburi 8:4–5; Warumi 8:16–17; Mafundisho na Maagano 18:10–14

Mwokozi Anatujua Sisi na Anaelewa Hali Zetu, Shida Zetu na Nguvu Yetu

Mwanamke Msamaria hakuja kisimani kusikia ujumbe wa injili. Yeye alikuja kuchota maji. Lakini Mwokozi aliweza kutambua kwamba kiu yake ilikuwa zaidi ya kiu ya kimwili. Yeye alijua kuwa alikuwa na zamani yenye matatizo ya uhusiano usioimara. Hivyo Yesu akachukua mahitaji ya kimwili ambayo alivutiwa nayo haraka—maji yaletayo uzima—na akayaunganisha na mahitaji ya kina ya kiroho “maji ya uzima” na “maisha yasiyo na mwisho.” Mwishoni mwa maongezi yao, mwanamke akapata ushahidi binafsi kwamba Yesu alikuwa Kristo, akivutiwa kwa sehemu na jinsi Yeye alivyomjua vyema. “[Yeye] ameniambia mambo yote ambayo nimefanya,” alisema. “Je, huyu siye Kristo?” (ona Yohana 4:6–29).

Kuwa mwalimu kama Kristo kunajumuisha kuwajua watu unaowafundisha na kujitahidi kuelewa kile kilichoko mioyoni mwao. Unaweza kupendelea kujua maisha yao na kuonyesha huruma. Unaweza kutafuta njia za kuelewa historia zao, vipaji, mapendeleo na mahitaji yao. Unaweza kuona jinsi wanavyojifunza vizuri zaidi. Unaweza kuuliza maswali, kusikiliza kwa makini, na kutazama. Zaidi ya yote, unaweza kusali ili upate uelewa ambao Roho pekee ndiye anayeweza kutoa. Kadiri unavyomwelewa vyema mtu, ndivyo unavyoweza vyema kumsaidia kupata maana binafsi na nguvu katika injili ya Yesu Kristo. Mara unapokuwa umeelewa kiu ya mtu, Roho anaweza kukufundisha jinsi ya kusaidia kuzima kiu hiyo kwa maji ya uzima ya Mwokozi.

Maswali ya Kutafakari: Je, ni kipi unachokijua tayari kuhusu watu unaowafundisha? Je, ni kipi kilicho muhimu kwao? Je! ni uwezo wao gani? Je, wanasumbuka na nini? Je, unaweza kufanya nini ili kuwaelewa vyema zaidi?

Kutoka kwenye Maandiko: Zaburi 139:1–5; Mathayo 6:25–32; Marko 10:17–21; Yohana 10:14; 3 Nefi 17:1–9

Mwokozi aliwaombea Wale Aliowafundisha.

Fikiria jinsi Simoni Petro alivyojisikia aliposikia Mwokozi akimwambia, “Simoni, Simoni, tazama, Shetani anakutamani, … lakini nimekuombea, kwamba imani yako isikutindike” (Luka 22:31–32). Ni kwa jinsi gani angekugusa wewe kujua kwamba Yesu alikuwa amesali kwa Baba kwa ajili yako? Watu wa kale wa Amerika walipata tukio kama hili, nao walilielezea kwa njia hii: “Hakuna ye yote anayeweza kuona shangwe iliyojaza nafsi zetu wakati tulipomsikia [Yesu] akituombea kwa Baba” (3 Nefi 17:17).

Unaweza pia kufikiri kuhusu kile kinachotokea ndani yako wakati wewe unaposali kwa ajili ya mtu—mara kwa mara, kwa jina. Je, ni kwa jinsi gani sala zako zinaathiri jinsi unavyohisi kuhusu mtu huyo? Ni kwa jinsi gani zinaathiri matendo yako? Ni wazi Baba wa Mbinguni anasikia na anajibu sala za dhati za mwalimu ambaye ana hamu ya kumsaidia mwanafunzi. Na katika hali nyingi, njia moja anayojibu sala hizo ni kwa kugusa moyo wa mwalimu na kumshawishi kufanya au kusema kitu ambacho kitamsaidia mwanafunzi kuuhisi upendo Wake.

Maswali ya Kutafakari: Unapofikiria kuhusu watu unaowafundisha, je, kuna mtu ye yote ambaye unahisi ana hitaji maalumu la sala zako? Je, unahisi kushawishika kuombea nini kwa niaba yake? Je, ni baraka zipi zinaweza kuja unapowaalika wanafunzi kuombeana?

Kutoka kwenye Maandiko: Yohana 17; Alma 31:24–36; 3 Nefi 18:15–24; 19:19–23, 27–34

Mwokozi Alihakikisha Kwamba Wote Walijisikia Kuheshimika na Kuthaminiwa

Mtazamo wa jumla miongoni mwa viongozi wa dini katika siku za Yesu ulikuwa kwamba watenda dhambi wanapaswa kutengwa. Kwa sababu ya hili, wakati viongozi hawa walipomwona Yesu akiingiliana na wenye dhambi, walikasirika. Inawezekanaje mtu anayeshirikiana na watu wa aina hii anaweza kuwa mwalimu wa kiroho.

Yesu, hata hivyo, alikuwa na njia tofauti. Yeye alitafuta kuwaponya wale waliokuwa wagonjwa kiroho (ona Marko 2:15–17; Luka 4:17–18). Yeye kwa mwendelezo aliwafikia wale waliokuwa tofauti na wale waliokuwa wamewazunguka wao au waliosumbuka zamani, na aliingiliana na wale waliotenda dhambi. Yeye alisifia imani ya askari wa Kirumi (ona Mathayo 8:5–13). Alimwita mtoza ushuru aliyedhaniwa vibaya kuwa mmoja wa wanafunzi Wake wa kuaminika (ona Marko 2:14). Mwanamke alipotuhumiwa kwa uzinzi, Yeye alimfanya ajisikie yuko salama na akamshawishi kutubu na kuishi maisha bora zaidi (ona Yohana 8:1–11).

Lakini Yesu alifanya zaidi ya hilo. Alilea mtazamo wa aina hiyo hiyo wa kukubalika na upendo miongoni mwa wanafunzi Wake Mfano Wake hakika ulikuwa katika mioyo ya Mitume Wake wakati muda ulipofika kwa wao kuipeleka injili kwa watu wote. Inaakisiwa katika maneno ya Petro: “Hakika natambua kwamba Mungu hana upendeleo” (Matendo 10:34).

Kuna uwezekano mkubwa sana kwamba karibia kila mtu uliyeitwa umfundishe anataabika katika njia fulani kuhisi kuwa anaheshimiwa na kuthaminiwa. Kwa njia ambayo wewe unawapenda na kuwaheshimu, unaweza kuonyesha kwamba siyo tu wanakaribishwa bali wanahitajika. Unaweza kuwatembelea hata wale wasiohudhuria, wanaohangaika, au wale wanaoonekana kutopendezwa, kuwa mvumilivu kama maendeleo yanaonekana kuja pole pole. Unaweza kumsaidia kila mmoja kuhisi yuko salama na mwenye amani kushiriki mawazo yake na waaminio wenzake. Na unaweza kufanya mengi zaidi juu ya hilo. Unaweza kuwashawishi wanafunzi wote kukusaidia kutengeneza mazingira ambapo mafundisho yanafundishwa katika roho ya heshima, ya kuwa wa hapa, na ya upendo.

Maswali ya Kutafakari: Je, ni kitu gani kinamsaidia mtu kuhisi kuheshimika na kuthaminiwa? Ni nini kinamshawishi mtu kuheshimu na kuthamini wengine? Kwa sala unapofikiria kuhusu watu unaowafundisha, unasukumwa kufanya nini ili kwamba wote waweze kuhisi kukaribishwa na kuhitajika?.

Kutoka kwenye Maandiko: Yohana 4; 2 Nefi 26:27–28, 33; Alma 1:26; 3 Nefi 18:22–25

Picha
baba akiwafundisha watoto

Walimu wanaweza kuwasaidia wale wanaowafundisha kuhisi kupendwa.

Mwokozi Alielezea Upendo Wake kwa Wale Aliowafundisha

Mwisho wa siku ya ajabu, yenye kuinua ya kufundisha na kutumikia miongoni mwa Wanefi Yesu aliona kwamba ulikuwa wakati wa Yeye kuondoka. Alikuwa na watu wengine wa kuwatembelea. “Nendeni nyumbani kwenu,” Alisema, “na kutayarisha akili zenu kwa kesho.” Lakini watu walikaa pale tu “wakilia,” wakimwangalia “kwa uthabiti kama wanaotaka kumwambia akae nao kwa muda mrefu zaidi.” Akitambua hitaji lao wasilolisema na “kujawa na huruma,” Yesu alikaa nao kwa muda mfupi (3 Nefi 17:3, 5–6). Aliwabariki wagonjwa wao na wanaoteseka. Alipiga magoti na kuomba pamoja nao. Alilia pamoja nao, na Yeye alilifurahi pamoja nao.

Kwa sala zingatia kujifunza maneno na matendo ya Mwokozi katika 3 Nefi 17. Tafakari upendo aliouonyesha kwa wale Aliowafundisha. Tafuta maelezo ya upendo Wake katika maeneo mengine katika maandiko. Kisha fikiria kuhusu watu unaowafundisha. Je, mnaonyeshaje kwa usahihi upendo kwa ajili yao? Mruhusu Roho akuongoze. Kama unapata ugumu kuhisi au kuelezea upendo kwa wale unaowafundisha, anza kwa kushuhudia juu ya upendo wa Mungu. Kisha “uombe kwa Baba kwa nguvu zote za moyo, kwamba tujazwe na [upendo msafi wa Kristo], ambao ametoa kwa wote ambao ni wafuasi wa kweli wa Mwanawe, Yesu Kristo” (Moroni 7:48). Na ukumbuke kwamba mashaka yako kwa ajili ya kufundisha somo hayapaswi kukuvuruga kutoka katika kuelezea upendo kwa njia ya maneno na matendo yako. Mara nyingi njia unazowatendea watu ni muhimu kama vile yale unayowafundisha.

Maswali ya Kutafakari: Jinsi gani Mwokozi amekusaidia wewe kujua upendo Wake kwako wewe? Jinsi gani mzazi au mwalimu mwingine alikusaidia wewe kuhisi upendo Wake? Je, watu unaowafundisha wanafahamu kwamba wewe unawapenda? Je, wanajua kwamba Mwokozi anawapenda?

Kutoka kwenye Maandiko: Marko 6:31–42; Yohana 13:3–16, 34–35; 15:12–13; 1 Wakorintho 13:1–7; 1 Yohana 4:7–11

Baadhi ya Njia ya Kutumia Kile Unachojifunza

  • Kama unafundisha darasa, jifunze majina ya wanafunzi na uyatumie unapofundisha.

  • Eleza shukrani yako wanafunzi wanapochangia.

  • Ingiliana na wanafunzi kabla na baada ya kufundisha.

  • Wasaidie wanafunzi kukuza hali ya upendo na heshima kwa kila mmoja.

  • Sikiliza kwa makini—unapokuwa unafundisha na nyakati nyinginezo.

  • Fanya vitendo vya huduma kwa wale unaowafundisha.

  • Uwe tayari kubadilisha mipango yako ya ufundishaji ili utumie muda zaidi kwenye kanuni ambazo ni muhimu kwa wale unaowafundisha.

Chapisha