Seminari na Vyuo
Fundisha Mafundisho


“Fundisha Mafundisho,” Kufundisha katika Njia ya Mwokozi: Kwa Ajili ya Wote Wanaofundisha Nyumbani na Kanisani (2022)

“Fundisha Mafundisho,” Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Picha
Yesu Kristo akifundisha hekaluni alipokuwa na umri wa miaka 12

Kristo akiwa Hekaluni, na Heinrich Hofmann

Fundisha Mafundisho

Ingawa Yesu alikua katika hekima na maarifa katika maisha Yake yote, Yeye hakuwa msomi kama viongozi wengine wa dini wa siku Zake. Lakini bado Yeye alipofundisha, watu walistaajabia, wakisema, “Amepataje huyu kujua elimu, ambaye hakusoma?” Je, kwa nini mafundisho Yake yalikuwa yenye nguvu kubwa? “Mafunzo yangu si yangu,” Mwokozi alieleza, “ila ni yake yeye aliyenipeleka” (Yohana 7:15–16). Mafundisho ni ukweli wa milele—unaopatikana katika maandiko na maneno ya manabii wa siku za mwisho—ambayo hutuonyesha njia ya kuwa kama Baba yetu wa Mbinguni na kurudi Kwake. Bila ya kujali jinsi ulivyomzoefu kama mwalimu, unaweza kufundisha kwa uwezo, kama vile Mwokozi alivyofundisha mafundisho ya Baba. Wewe pamoja na wale unaowafundisha mtastaajabia baraka Mungu anazotuma wakati kufundisha kwako na kujifunza vimewekwa katika msingi wa neno Lake.

Kufundisha Mafundisho

  • Jifunze mafundisho ya Yesu Kristo kwa ajili yako mwenyewe.

  • Fundisha kutoka katika maandiko na maneno ya manabii wa siku za mwisho.

  • Wasaidie wanafunzi kutafuta, kutambua na kuelewa kweli katika maandiko.

  • Fokasi kwenye kweli ambazo zinaongoza kwenye uongofu na kujenga imani katika Yesu Kristo.

  • Wasaidie wanafunzi kupata uhusiano binafsi katika mafundisho ya Yesu Kristo.

Mwokozi Alijifunza Mafundisho

Inaonekana wazi kwamba Mwokozi alijifunza kutoka kwenye maandiko katika ujana Wake akizidi kuendelea “katika hekima … na akimpendeza Mungu” (Luka 2:52). Uelewa wake wa kina juu ya mafundisho ya Baba yalikuwa dhahiri wazazi Wake walipomkuta hekaluni katika umri mdogo akiwafundisha walimu wa Kiyahudi na kujibu maswali yao (ona Tafsiri ya Joseph Smith, Luka 2:46 [katika Luka 2:46, tanbihi c]). Baadae Shetani alipojitokeza mwenyewe akiwa na majaribu makali nyikani, elimu ya Yesu juu ya mafundisho katika maandiko ilimsaidia kupinga majaribu hayo (ona Luka 4:3–12).

Wewe pia unaweza kutafuta kujifunza mafundisho ya kweli kwa kina zaidi kabla ya kuyafundisha. Unapojiandaa kufundisha na kujifunza na wengine, angalia kwa makini kwa kile Bwana alichosema kuhusu ukweli unaofundisha. Pekua maandiko na maneno ya manabii walio hai kwa ajili ya ufafanuzi na ushauri. Kuishi na kutumia kweli unazojifunza kutamwalika Roho ili akufundishe mafundisho haya kwa njia za kina zaidi na kuthibitisha ukweli wa mafundisho katika mioyo ya wale unaowafundisha.

Maswali ya Kutafakari: Kwa nini ni muhimu kuzielewa kweli za injili wewe mwenyewe? Ni kwa jinsi gani umepata uelewa wa kina zaidi wa kweli za injili? Unahisi ushawishi wa kufanya nini ili kuboresha kujifunza kwako maandiko na maneno ya manabii walio hai?

Kutoka kwenye Mandiko: Mithali 7:1–3; 2 Nefi 4:15–16; Mafundisho na Maagano 11:21; 88:118

Mwokozi Alitufundisha kutoka kwenye Maandiko

Baada ya kifo cha Mwokozi, wawili kati ya wanafunzi Wake walikuwa wakitembea na kuongea wakiwa wamechanganyika na huzuni na mshangao mioyoni mwao. Ingewezaje kuleta maana ya kile kilichotokea hivi punde? Yesu wa Nazareti, mtu waliyemtumaini kuwa Mkombozi wao, alikuwa amekufa kwa siku tu sasa. Na kisha kukawa na taarifa kwamba kaburi lake lilikuwa tupu, na malaika wakitangaza kwamba Yeye yuko hai! Katika wkati huu muhimu sana katika imani ya wanafunzi hawa, mgeni alijiunga katika safari yao. Aliwafariji kwa “kuwaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu [Mwokozi].” Hatimaye, wasafiri wale wakatambua kwamba mwalimu wao alikuwa Yesu Kristo Mwenyewe na kwamba hakika alikuwa amefufuka. Ni kwa jinsi gani walimtambua Yeye? “Je, mioyo yetu haikuwa inawaka ndani yetu,” baada waliwaza, “wakati alipokuwa anaongea na sisi njiani, na kutufunulia aandiko?” (Luka 24:27, 32).

Mzee D. Todd Christofferson alifundisha, “Dhumuni kuu la maandiko yote ni kujaza nafsi zetu kwa imani katika Mungu na Mwanawe Yesu Kristo” (“Baraka ya Maandiko,” Liahona, Mei 2010, 34). Wakati wote wa huduma Yake, Yesu alitumia maandiko kufundisha, kusahihisha, na kuwashawishi wengine. Hakikisha kwamba mafundisho yako hayaendi nje ya maandiko na maneno ya manabii. Kwa uaminifu kabisa unapotegemea maneno ya Mungu katika kufundisha kwako, unaweza kuwatendea wengine kile Mwokozi alitenda. Unaweza kuwasaidia wao kumjua Yeye, kwani sisi sote tunahitaji imani yetu kwa Mwokozi iimarishwe mara kwa mara. Mapenzi yako juu ya maandiko yatathibitika kwa wale unaowafundisha, na ufundishaji wako utamwalika Roho ili kusababisha mioyo yao kuwaka kwa ushuhuda juu ya Baba na Mwana.

Maswali ya Kutafakari: Je, ni kwa jinsi gani wewe umeshawishika na mwalimu aliyekuwa akitumia maandiko kukusaidia wewe kuja kumjua vyema Mwokozi? Ni nini unapaswa kufanya ili kutegemea zaidi maandiko na maneno ya manabii unapofundisha. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kuelewa na kupenda neno la Mungu?

Kutoka kwenye Maandiko: Luka 4:14–21; Alma 31:5; Helamani 3:29–30;3 Nefi 23

Mwokozi Aliwasaidia Watu Kutafuta, Kutambua, na Kuelewa Ukweli

Mwanasheria mmoja aliwahi kumuuliza Yesu, “Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?’” Katika jibu, Mwokozi alimwongoza muulizaji kwenye maandiko: “Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje?” Hili lilimpeleka mtu yule siyo tu kwenye jibu lake—“Mpende Bwana Mungu wako … Na jirani yako”—lakini pia kwenye swali la ufuatiliaji: “Na jirani yangu ni nani?” Mwokozi alijibu swali hili kwa mfano kuhusu wanaume watatu ambao walimwona msafiri mwenzao katika uhitaji. Ni mmoja tu katika wale watatu, Msamaria, aliyekuwa akichukiwa na Wayahudi kwa sababu tu ya mahali anakotoka, alisimama akamsaidia. Yesu kisha akamwalika mwanasheria yule kujibu swali lake yeye mwenyewe: “Waonaje wewe, katika hao watatu, ni yupi aliyekuwa jirani yake yule aliyeangukia kati ya wanyang’anyi?” (ona Luka 10:25–37).

Kwa nini unafikiria Mwokozi alifundisha katika njia hii—alijibu maswali kwa mialiko ya pekua, tafakari, na gundua? Sehemu ya jibu ni kwamba Bwana anathamini jitihada za kutafuta ukweli. “Tafuteni, nanyi mtapata,” Amealika tena na tena na tena (ona, kwa mfano, Mathayo 7:7; Luka 11:9; Mafundisho na Maagano 4:7). Yeye anazawadia matendo ya imani na subiri kwa watafutaji.

Kama Mwokozi, unaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kutambua na kuelewa ukweli. Maandiko, kwa mfano, yamejaa kweli za injili, lakini wakati mwingine, inahitaji jitihada ya dhati kuzipata. Mnapojifunza pamoja kutoka kwenye maandiko, simama na waulize wale unaowafundisha ni ukweli gani wa injili wameuona. Wasaidie kuona jinsi kweli hizi zinavyohusika kwenye mpango wa wokovu wa Baba wa Mbinguni. Wakati mwingine kweli za milele zimeelezwa katika maandiko, na wakati mwingine zimefafanuliwa katika hadithi na maisha ya watu tunaosoma habari zao. Inaweza pia kuwa ya msaada kuchunguza pamoja usuli wa historia ya mistari unayosoma, vile vile maana ya mistari hiyo na jinsi inavyotumika kwetu sisi leo.

Maswali ya Kutafakari: Je, unatambuaje kweli za milele katika maandiko au maneno ya manabii? Ni kwa jinsi gani kweli hizo zinabariki maisha yako? Je, ni zipi baadhi ya njia unazoweza kuwasaidia wanafunzi kutambua na kuelewa kweli ambazo zitakuwa na maana kwao na kuwaleta karibu zaidi na Mungu?

Kutoka kwenye: Yohana 5:39; 1 Nefi 15:14; Mafundisho na Maagano 42:12

Picha
wanafunzi wakijisomea

Tunaweza kuwasaidia wale tunaowafundisha kutafuta na kutambua ukweli wao wenyewe

Mwokozi Alifundisha Ukweli Ambao Uliongoza kwenye Uongofu na Kujenga Imani

Siku moja ya Sabato, Mwokozi na wanafunzi Wake, wakiwa wanaona njaa, walipita kwenye shamba na kuanza kula nafaka. Mafarisayo, daima walikuwa na hamu ya kusisitiza pointi muhimu kwenye sheria ya Musa, ilionyesha kwamba kukusanya nafaka ilikuwa ni aina ya kazi, ambayo ilikatazwa siku ya Sabato (ona Marko 2:23–24). Kwa kutumia kirai kutoka kwa nabii Yakobo katika Kitabu cha Mormoni, Mafarisayo “waliangalia zaidi ya lengo” (Yakobo 4:14). Kwa maneno mengine, walikuwa wamefokasi zaidi juu ya tafsiri ya mazoea ya amri ambapo walikosa madhumuni ya kiungu ya amri hizo—kutusogeza karibu zaidi na Mungu. Ukweli, Mafarisayo hata hawakutambua kwamba Mtu aliyetoa amri hiyo ya kuheshimu hiyo Sabato alikuwa amesimama mbele yao.

Mwokozi alichukua fursa hiyo kushuhudia juu ya utambulisho Wake wa kiungu na kufundisha kwa nini Sabato ni muhimu. Iliumbwa kwa ajili yetu sisi kama siku ya kumwabudu Bwana wa Sabato, Yesu Kristo Mwenyewe (ona Marko 2:27–28). Ukweli wa jinsi hiyo unatusaidia kuelewa kwamba amri za Mungu ni zaidi ya tabia ya nje tu. Zimekusudiwa zitusaidie kubadili mioyo yetu na kuwa waongofu kamili.

Kwa uangalifu fikiria mafundisho na kanuni unazoamua kufokasi juu yake. Wakati ziko kweli nyingi katika maandiko ambazo zinaweza kujadiliwa, ni vyema kufokasi juu ya kweli za injili ambazo zinatuongoza kwenye uongofu na kujenga imani katika Yesu Krsito. Ukweli rahisi, na wa msingi Mwokozi aliofundisha na kuonyesha mfano wake una nguvu kubwa ya kubadilisha maisha yetu—kweli kuhusu Upatanisho Wake, mpango wa wokovu, amri za upendo kwa Mungu na upendo kwa jirani yetu, na kadhalika. Mwalike Roho atatoe ushuhuda juu ya kweli hizi, akiwasaidia kuzama chini kabisa ya mioyo ya wale unaowafundisha.

Maswali ya Kutafakari: Ni zipi baadhi ya kweli za injili ambazo zimekusaidia wewe kuja kuwa mwongofu zaidi kwa Yesu Kristo na kuwa na imani kubwa zaidi Kwake? Je, mwalimu alikusaidiaje wewe kufokasi juu ya kweli muhimu zaidi za injili? Je! Unaweza kufundisha nini ambacho kitawasaidia wengine kuongoka zaidi kwa Yesu Kristo?

Kutoka kwenye Maandiko: 2 Nefi 25:26; 3 Nefi 11:34–41; Mafundisho na Maagano 19:31–32; 68:25–28; 133:57; Musa 6:57–62

Mwokozi Aliwasaidia Watu Kutafuta Uhusiano Binafsi katika Mafundisho Yake

“Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi, tena hula nao,”Mafarisayo walinung’unika kuhusu Yesu—wakimaanisha kwamba hiyo haikuwa tabia sahihi kwa mwalimu wa kiroho (Luka 15:2). Yesu aliona kwamba hii ilikuwa fursa ya kufundisha kweli muhimu. Ni kwa jinsi gani Yeye angefanya hivyo? Ni kwa jinsi gani Yeye angewasaidia Mafarisayo kuona kwamba ilikuwa ni mioyo yao—na sio Wake—ambao haikuwa safi na ilihitaji uponyaji? Ni kwa jinsi gani Yeye angetumia mafundisho Yake kuonyesha kwamba mawazo yao na tabia zao zilihitaji mabadiliko?

Yeye alilifanya hili kwa kuzungumza nao juu ya kondoo ambaye alipotea kutoka kundini na juu ya sarafu iliyopotea. Yeye alizungumza juu ya mwana muasi aliyetafuta msamaha na juu ya kaka mkubwa ambayo alikataa kumpokea au kula naye. Kila moja ya mifano hii ilikuwa na kweli ambazo zilihusika na jinsi Mafarisayo walivyokuwa wakiwaangalia watu wengine, akiwafundisha kwamba kila nafsi ina thamani kubwa (ona Luka 15). Mwokozi hakuwaambia Mafarisayo—au ye yote kati yetu—ajitambulishe naye katika mifano Yake. Wakati mwingine tunakuwa yule baba mwenye shauku. Wakati mwingine sisi ni yule kaka mwenye wivu. Mara nyingi sisi ni yule kondoo aliyepotea au mwana mpumbavu. Lakini hali yetu iwayo yo yote ile, kupitia mifano Yake, Mwokozi anatualika kutafuta uhusiano katika mafundisho Yake—ili kugundua kila Yeye anachotaka sisi kujifunza na kile tunachohitaji kubadilisha katika mawazo yetu sisi wenyewe na tabia zetu.

Unaweza kutambua kwamba baadhi ya wanafunzi hawaoni kwa nini baadhi ya kweli zina maana kwao. Unapozingatia mahitaji ya wale unaowafundisha, fikiria kuhusu jinsi kweli katika maandiko zinavyoweza kuwa za maana na zenye kutumika katika hali zao. Njia mojawapo unayoweza kuwasaidia wanafunzi kuona uhusiano wa kweli wanazogundua ni kwa kuwauliza maswali kama “Hili linawezaje kukusaidia wewe na hilo unalopitia sasa? Kwa nini ni muhimu kwako kujua hili? “Je! Ni tofauti gani hili linaweza kufanya katika maisha yako? Wasikilize wale unaowafundisha. Waruhusu kuuliza maswali Watie moyo kufanya muunganiko kati ya mafundisho ya Mwokozi na maisha yao wenyewe. Ungeweza pia kushiriki jinsi wewe ulivyopata uhusiano wa maisha yako mwenyewe katika yale unayofundisha. Kufanya hili kunaweza kumwalika Roho ili awafundishe wanafunzi mmoja mmoja jinsi mafundisho yanavyoweza kuleta tofauti katika maisha yao.

Maswali ya Kutafakari: Ni kitu gani hicho ambacho hufanya kweli za injili kuwa zenye maana na muhimu kwetu? Je, ni nini kinakusaidia wewe kupata uhusiano binafsi unaposoma injili? Je, unafanya nini ili kufokasi kwenye kweli ambazo zinahusika na wale unaowafundisha?

Kutoka kwenye Maandiko: 1 Nefi 19:23; 2 Nefi 32:3; Mafundisho na Maagano 43:7–9

Baadhi ya Njia za Kutumia Kile Unachojifunza

  • Tathmini kile unachofundisha ili kuhakikisha kwamba unafundisha mafundisho ya kweli? Maswali yafuatayo yanaweza kusaidia:

    • Je, ninachopanga kufundisha kinatokana na maandiko na maneno ya manabii wa siku za mwisho?

    • Je, ni manabii wengi wamefundisha hili? Je, viongozi wa sasa wa Kanisa wanafundisha kuhusu nini?

    • Je, hili litawasaidiaje wengine kujenga imani katika Yesu Kristo, kutubu, na kuendelea kwenye njia ya agano?

    • Je, hili linaoana na misukumo ya Roho Mtakatifu, au ninahisi kutotulia kiroho kuhusu hili?

  • Kila siku jifunze neno la Mungu ili kujifunza mafundisho ya kweli wewe mwenyewe.

  • Waombe wanafunzi kusoma maandiko na maneno ya manabii wa sasa unapofundisha.

  • Wafundishe jinsi ya kutumia tanbihi, Mwongozo wa Maandiko, na nyenzo nyinginezo wanapojifunza maandiko.

  • Waalike wanafunzi kutafuta kweli katika vifungu vya maandiko au hadithi.

  • Toa ushuhuda juu ya jinsi wewe ulivyokuja kujua mafundisho kuwa ni ya kweli.

  • Tumia hadithi au sitiari ili kuwasaidia wanafunzi kupata uelewa wa kina wa kweli za injili?

Chapisha