Seminari na Vyuo
Dhumuni la Kufundisha katika Njia ya Mwokozi


“Dhumuni la Kufundisha katika Njia ya Mwokozi,” Kufundisha katika Njia ya Mwokozi: Kwa Ajili ya Wote Wanaofundisha Nyumbani na Kanisani (2022)

“Dhumuni la Kufundisha katika Njia ya Mwokozi,” Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Dhumuni la Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Kanuni ambazo zimeelezwa katika nyenzo hii zinaweza kumsaidia kila mwalimu wa injili afundishe katika njia ya Mwokozi. Hiyo inajumuisha wazazi, akina kaka na akina dada wahudumiaji, walimu wa seminari na chuo, na mtu yeyote ambaye wito wake wa Kanisa unampa fursa ya kufundisha.

Unaweza kujifunza nyenzo hii wewe mwenyewe au kuitumia ili kuongoza majadiliano na wengine kuhusu jinsi ya kuwa mwalimu bora. Kwa mfano, nyenzo hii ingeweza kutumika katika jioni za nyumbani, mikutano ya urais, mikutano ya baraza la kata au kigingi, mikutano ya mafunzo kwa ajili ya walimu wa seminari na chuo, na mikutano ya baraza la walimu (ona “Kwa Ajili ya Viongozi—Kuwasaidia Walimu Wafanikiwe”).

Jinsi Nyenzo Hii Ilivyoundwa

Sehemu ya 1 inasisitiza umuhimu wa kufokasi juu ya Yesu Kristo wakati wowote tunapofundisha kanuni za injili Yake. Sehemu hii inaelezea kile tunachokifundisha.

Sehemu ya 2 inasisitiza Kanuni za Kufundisha Kama Kristo. Sehemu hii inaeleza jinsi tunavyofundisha.

Sehemu ya 3 inatoa mapendekezo yanayofaa ili kuwasaidia walimu watumie kanuni hizo za kufundisha kama Kristo.