Seminari na Vyuo
Mapendekezo kwa Ajili ya Mazingira Mbalimbali ya Ufundishaji na Wanafunzi


“Mapendekezo kwa Ajili ya Mazingira Mbalimbali ya Ufundishaji na Wanafunzi,” Kufundisha katika Njia ya Mwokozi: Kwa Ajili ya Wote Wanaofundisha Nyumbani na Kanisani (2022)

“Mapendekezo kwa Ajili ya Mazingira Mbalimbali ya Uufundishaji na Wanafunzi,” Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Picha
wanaume wakifundisha familia

Mapendekezo kwa Ajili ya Mazingira Mbalimbali ya Ufundishaji na Wanafunzi

Kanuni za kufundisha katika njia ya Mwokozi zinaweza kutumika kwenye fursa yo yote ya kufundisha—nyumbani, kanisani, na mahali pengine po pote. Hata hivyo, kila fursa inakuja na hali zake yenyewe ya kipekee. Sehemu hii inatoa mapendekezo ya ziada ambayo ni mahususi kwa aina tofauti za wanafunzi na mazingira mbalimbali ya ufundishaji.

Nyumbani na Familia

Nyumbani Ndipo Mahali Bora zaidi pa Kufundisha na Kujifunza Injili

Rais Russell M. Nelson amefundisha kwamba nyumbani panapaswa kuwa “kitovu cha kujifunza injili” (“Kuwa Mtakatifu wa Siku za Mwisho wa Mfano,” Liahona, Nov. 2018, 113). Ufundishaji ambao unafanyika kanisani au seminari ni wa thamani na unahitajika, lakini unakusudiwa kusaidia ufundishaji ambao hufanyika nyumbani. Sehemu kubwa—na sehemu iliyo bora zaidi—kwa ajili ya kujifunza injili, kwa wote, sisi wenyewe na kwa familia zetu, ni nyumbani.

Lakini hiyo haimaanishi kwamba usomaji mzuri unatokea tu wenyewe nyumbani; unahitaji jitihada ya makusudi. Rais Nelson amependekeza kwamba inawezekana ukahitaji “mabadiliko” au “kufanyia marekebisho nyumba yako”—siyo lazima kuporomosha kuta au kuongeza sakafu mpya lakini pengine kwa kujitathmini kwa ujumla hali ya kiroho katika nyumba yako, ikijumuisha mchango wako katika roho hiyo (“Kuwa Mtakatifu wa Siku za Mwisho wa Mfano,” 113). Kwa mfano, fikiria juu ya muziki, video, na vyombo vingine vya habari nyumbani mwako; picha juu ya kuta; na njia ambayo washiriki wa familia yako wanavyoongea na kutendeana. Je, vitu hivi vinaalika ushawishi wa Roho Mtakatifu? Je, unatenga muda kwa ajili ya kujifunza injili, kama mtu binafsi na kama familia? Je, wana familia wanahisi kupendwa, salama na karibu na Mungu wanapokuwa nyumbani mwako?

Yawezekana usijisikie kwamba wewe unao udhibiti juu ya hali ya kiroho nyumbani mwako. Kama hiyo ndiyo hali halisi, uwe mshawishi bora unayeweza kumwomba Bwana msaada. Yeye ataheshimu jitihada zako za haki. Unapojaribu kufundisha na kujifunza injili, hata kama huoni matokeo unayotamani mara moja, wewe unafanikiwa.

Kujifunza Nyumbani Kunajengwa juu ya Msingi wa Uhusiano

“Wapende wale unaowafundisha” inatumika katika aina zote za kufundisha injili, lakini nyumbani, upendo unapaswa kuja kiurahisi zaidi na utasikika kwa kina zaidi. Hata kama nyumba yako ina upungufu kidogo wa ubora, inakusudiwa kuwa kitovu cha kufundisha injili kwa sababu hapo ndipo mahali ambapo uhusiano wa kudumu zaidi unapojengwa. Walimu nje ya nyumbani wanaweza kuwa na uzoefu zaidi au wamepata mafunzo kama walimu, lakini kamwe hawawezi kunakili uwezekano wa kupenda, uhusiano ambao uko nyumbani Kwa hiyo lea uhusiano huo. Tumia muda na juhudi muhimu kuwasikiliza wanafamilia wako na jenga kuaminiana na kuelewana. Hii itasaidia kutengeneza msingi imara kwa ajili ya jitihada zako za kufundisha na kujifunza injili hapo nyumbani.

Kujifunza Nyumbani Kunaweza Kupangwa lakini Pia Hujitokeza Pasipo Kutarajia

Madarasa mengi ya kanisani hutokea mara moja kwa wiki, yenye ratiba ya kuanza na kumalizika, lakini hii siyo daima katika suala la nyumbani. Unaweza kuwa na ratiba ya somo la jioni ya nyumbani au kujifunza maandiko kama familia, lakini fursa za kufundisha katika familia mara kwa mara hujitokeza pasipo kutarajia, katika nyakati za kila siku—wakati wa kula, kazi za nyumbani, kucheza mchezo, kusafiri kwenda kazini au shule, kusoma kitabu, au kuangalia sinema pamoja. Mvua kubwa yaweza kuwa nafasi ya kuzungumza kuhusu jinsi ambavyo Mwokozi anavyotukinga kutokana na dhoruba za kiroho. Kijana anayekabiliwa na uamuzi mgumu wa kufanya anaweza kuwa tayari kujifunza kuhusu kupokea ufunuo binafsi. Mtoto anayeogopa anaweza kufaidika kutokana na ushuhuda kuhusu Mfariji. Watoto ambao wanakosa adabu au wanaotendeana vibaya wanaweza kufundishwa kuhusu toba na msamaha.

Kwa vile nyakati kama hizi sio za kutarajiwa, hauwezi kujitayarisha kwa ajili yazo kama vile unavyoweza kujitayarisha kwa ajili ya somo. Hata hivyo, wewe unaweza kujiandaa mwenyewe kwa kuwa msikivu kwa Roho na kujitahidi “kuwa tayari daima” (1 Petro 3:15). Wakati wo wote unaweza kuja kuwa wakati wa kufundisha.

Kujifunza Nyumbani Kuna Kuwa na Jitihada Ndogo Ndogo, Rahisi na Endelevu

Wazazi wakati mwingine wanakufa moyo majaribio yao ya kufundisha injili nyumbani yanapoonekana kutofanikiwa. Ikihukuliwa moja moja, jioni ya nyumbani moja, kikao cha kujifunza maandiko, au mazungumzo ya injili yawezekana isionekane kukamilisha kitu. Lakini mkusanyiko wa jitihada ndogo ndogo, na rahisi, zenye kujirudia kwa mwendelezo wa muda, zinaweza kuwa na nguvu zaidi na zenye kuimarisha kuliko nyakati chache za kukumbukwa au somo kubwa moja. “Mambo yote lazima yatakuja kutimia katika wakati wake,” Bwana alisema. “Kwa hiyo, msichoke kutenda mema, kwa kuwa mnaijenga misingi ya kazi kubwa. Na kutokana na mambo madogo huja yale yaliyo makuu” (Mafundisho na Maagano 64:32–33; ona pia Alma 37:6–7). Kwa hivyo usikate tamaa, na usiogope kuhusu kukamilisha kitu kikubwa kila wakati. Uwe na mwendelezo tu katika jitihada zako.

Nyumbani, Kujifunza na Kuishi Injili Havitenganishwi

Injili inachukua uhusiano mara moja nyumbani. Humo watu ambao unajifunza injili pamoja nao ni watu utakaoishi nao injili hiyo—kila siku. Ukweli, muda mwingi, kuishi injili ni jinsi gani sisi tunajifunza injili. Kwa hivyo unapojifunza na kufundisha injili nyumbani, angalia njia unazoweza kuunganisha kile unachojifunza na kile unachofanya. Nyumbani mwako, acha injili iwe kitu unachojitahidi kukiishi, siyo tu kitu unachokizungumzia.

Picha
mwanamke akiwafundisha watoto

Fursa za kufundisha injili katika familia mara kwa mara hutokea katika hali isiyopangwa, nyakati za kila siku.

Kufundisha Watoto

Watoto Wanahitaji Mabadiliko

Watoto wote ni tofauti, na wanapokua, mahitaji yao yatabadiklika. Kubadilisha mbinu zako za ufundishaji kutakusaidia wewe kukidhi mahitaji yao tofauti tofauti. Kwa mfano, zingatia kutumia yafuatayo:

  • Hadithi. Hadithi huwasaidia watoto kuona jinsi ambavyo injili inatumika katika maisha ya kila siku. Tumia hadithi kutoka katika maandiko, kutoka katika maisha yako mwenyewe, kutoka katika historia ya familia yako, au kutoka kwenye magazeti ya Kanisa hususani kuhusu Mwokozi. Panga njia za kuwahusisha watoto katika hadithi—kwa kushikilia picha, kurudia kirai, au kuigiza sehemu.

  • Vielelezo vya Kufundishia. Picha, video, na vitu vinaweza kusaidia watoto kuelewa na kukumbuka kanuni za injili. Picha nyingi na video zinaweza kupatikana katika Media Library kwenye ChurchofJesusChrist.org.

  • Muziki. Nyimbo za dini na nyimbo takatifu nyinginezo zinaweza kuwasaidia watoto kuhisi upendo wa Mungu, kumhisi Roho, na kujifunza ukweli wa injili. Melodi, uzani, na mashairi rahisi vinaweza kuwasaidia watoto kukumbuka kweli za injili kwa miaka mingi ijayo. Unapoimba na watoto, wasaidie kugundua na kuelewa kanuni zinazofundishwa katika nyimbo hizo.

Watoto wengi wanajifunza vyema zaidi wakati milango mingi ya fahamu inapohusishwa. Tafuta mbinu za kuwasaidia watoto watumie milango yao ya fahamu ya kuona, kusikia, na kugusa wanapojifunza. Katika hali zingine, unaweza hata kupata njia za kujumuisha hisia zao za kunusa na kuonja!

Watoto Ni Wabunifu

Wakati unapowaalika watoto kuchora, kujenga, kupaka rangi, au kuandika kitu kinachohusika na kanuni ya injili, unawasaidia kuelewa vyema kanuni hiyo, na unawapa kitu halisi cha kukumbuka juu ya kile walichojifunza. Wanaweza pia kutumia kile walichobuni kushiriki kile walichojifunza na wengine. Kila toleo la gazeti la Rafiki linajumuisha shughuli za ubunifu kwa ajili ya watoto.

Watoto ni Wadadisi

Watoto wanapouliza maswali, ona hizo kuwa ni fursa, na sio vurugu. Maswali ya watoto ni kiashirio kwamba wako tayari kujifunza na maswali yao yanakupa wewe utambuzi wa thamani katika kujua kile wao wanachofikiri na kuhisi. Wasaidie kuona kwamba majibu ya maswali yao kiroho yanaweza kupatikana katika maandiko na maneno ya manabii walio hai.

Watoto Wanahitaji Upendo Hata Wanapokuwa Wana vurugu

Mara nyingine mtoto hutenda katika njia ambazo huvuruga kujifunza kwa wengine. Mara nyingi tabia za vurugu zinatokana na hitaji lisilotimizwa. Wakati haya yanapotokea, kuwa mvumilivu, mwenye upendo, na mwenye kuelewa kuhusu changamoto ambazo mtoto anaweza kuwa akikabiliana nazo. Anaweza kuwa anahitaji tu nafasi nyingi za kushiriki katika somo kwa njia chanya—kwa mfano, kushikilia picha, kuchora kitu ubaoni, au kusoma maandiko.

Ikiwa mtoto anaendelea kuwa msumbufu, inaweza kuwa bora kuzungumza naye binafsi. Katika roho wa upendo na uvumilivu, eleza matarajio yako na imani yako kwamba anaweza kufanya hivyo. Msifie mtoto anapokuwa amefanya chaguzi bora.

Watoto Wana Mengi ya Kushiriki

Wakati ambapo watoto wanajifunza jambo geni, kawaida wanapenda kushiriki na wengine. Himiza hamu hii kwa kuwapatia watoto nafasi za kufundishana kanuni za injili, mmoja na mwingine, kwa washiriki wa familia zao, na marafiki zao. Pia waombe washiriki nawe fikira zao, hisia, na uzoefu unaohusiana na kanuni unazofundisha. Utakuta kwamba wana utambuzi ulio rahisi, safi, na wenye nguvu.

Watoto Wanaweza Kumhisi Roho lakini Yawezekana Wakahitaji Msaada wa Kutambua Ushawishi Wake

Hata watoto ambao bado hawajapokea kipawa cha Roho Mtakatifu wanaweza kuhisi ushawishi Wake wanapojifunza kuhusu Yesu Kristo na injili Yake. Wanapofanya chaguzi sahihi wanaweza kuhisi idhinisho la Mwokozi kupitia Roho. Wafundishe watoto kuhusu njia tofauti Roho anazowasiliana nasi. Wasaidie kutambua sauti Yake Yeye anaposema nao. Hii itawaandaa wao kukuza tabia ya kutafuta na kutendea kazi ufunuo binafsi katika maisha yao yote.

Kufundisha Vijana

Vijana Wanao Uwezekano Mkubwa wa Kuwa

Vijana wana uwezekano wa kuwa wenye kufanya mambo ya ajabu katika huduma ya Bwana. Matukio mengi ambayo yamerekodiwa katika maandiko yanaonyesha wazi kwamba Mungu anayo imani katika uwezo wa kiroho wa vijana. Ikiwa vijana watahisi unawaamini, imani yao katika uwezo wao mtakatifu itakua, na watakushangaza na yale wanaweza kutimiza. Kwa upendo wasaidie kuona ono la kile ambacho Baba wa Mbinguni anajua wanaweza kuwa. Fuata mfano wa Mwokozi kwa kuendelea kuwapenda na kuwahimiza, kwa uvumilivu ukifanya kazi pamoja nao, na kamwe usikate tamaa juu yao.

Vijana Wanajifunza kuhusu Wao Wenyewe

Vijana unaowafundisha wanajenga misingi ya shuhuda zao. Wapo kwenye mchakato wa kugundua imani na misimamo yao. Wanafanya maamuzi ambayo yataathiri mwelekeo wa maisha yao. Kusalimika kiroho katika nyakati hizi za hatari na kutimiza misheni ya Bwana kawa ajili yao, vijana unaowafundisha watahitaji kujua jinsi ya kupata nguvu wakati wa majaribu yao, majibu kwa maswali yao na ujasiri wa “kusimama kama mashahidi wa Mungu” (Mosia 18:9).

Vijana wanayo hamu inayokua ya kujifunza kwa hoja na matukio kuliko kwa kuambiwa tu. Hii inamaanisha kwamba kufundisha kijana kunahitaji ujuzi mzuri wa kusikiliza. Vijana wanapohisi kuelewa, watajisikia huru zaidi kupata ushauri na mwongozo. Wahakikishie kwamba Bwana anawajua na atawasaidia wakati wanapopigana mieleka na maswali na majaribu. Wanaweza kufanya imani yao katika Yeye kwa kukuza tabia za kila siku za kusali na kujifunza maandiko na kwa kuwahudumia wengine. Kuwahimiza vijana kushiriki katika madarasa ya Kanisa na kujifunza wao wenyewe inaweza kuwasaidia kuwa na uzoefu wao binafsi ambao utajenga ushuhuda wao wa urithi wa kiungu.

Vijana Wengi Wanajisikia Vizuri Kutumia Teknolojia

Ikiwa vijana unaowafundisha wana vifaa vyao vya kielektroniki, kumbuka kwamba vifaa hivi ni vifaa vya kuboresha kujifunza. Wafundishe jinsi ya kutumia maandiko ya kielekroniki na nyenzo nyinginezo zinazopatikana katika Maktaba ya Injili. Unaweza pia kutuma ujumbe na tovuti kwa vijana katikati ya wiki ili kuwasaidia kujiandaa kwa masomo yajayo.

Picha
Darasa la Shule ya Jumapili

Vijana wanahitaji kuelewa kile ambacho Baba wa Mbinguni anajua wanaweza kuwa.

Kufundisha Watu Wazima

Watu Wazima Wanaweza Kuwajibikaji kwa ajili ya Kujifunza Kwao

Wanafunzi watu wazima wanao uwezo wa kujiongoza wenyewe katika aina za kujifunza injili (ona 2 Nefi 2:26). Waalike kujiandaa kwa ajili ya majadiliano ya injili kwa kujifunza kitu kabla ya muda, na wahimize kushiriki kile wanachojifunza kwa njia ya Roho. Unaweza pia kuwauliza ni kanuni gani ya injili ambayo wangependa kutumia muda ili kujifunza pamoja.

Watu Wazima Huchota Kutoka kwenye Uzoefu Wao Wanapojifunza

Ayubu alieleza, “Wazee ndio walio na hekima; na katika kuishi siku nyingi iko fahamu” (Ayubu 12:12). Kwa ujumla, hekima na uelewa wa kiroho huja baada ya matukio ya miaka mingi. Unapowafundisha watu wazima, waalike kushiriki matukio ambayo yamejenga imani yao kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Hii itawapa wao fursa ya kushuhudia kuhusu jinsi wao walivyokuja kujua kwamba kanuni za injili wanazojifunza ni za kweli. Kuelezeana uzoefu pia kunajenga uhusiano kati ya wale unaowafundisha, kusaidia “wote … wapate kujengana” (Mafundisho na Maagano 88:122).

Watu Wazima Wanatafuta Matumizi Utendaji

Watu wazima unaowafundisha yawezekana wakawa na kazi na majukumu mengi katika taaluma, jamii, miito ya Kanisa, na familia zao. Wanapojifunza injili, mara nyingi wanafikiria kuhusu jinsi kile wanachojifunza kinavyoweza kuwasaidia wao katika kazi zao. Waalike kuona jinsi neno la Mungu linavyohusika na hali zao za kipekee. Unaweza kufanya hivyo kwa kuwauliza jinsi kanuni za injili zilivyo na maana na kutumika katika maisha yao.

Watu Wazima Wanaweza Kufikiri katika Njia Changamani

Kwa sababu ya uzoefu wao na maarifa, watu wazima wanajua kwamba hapatakuwa daima na majibu rahisi kwa naswali ya injili. Wanaweza wakashukuru kwamba kifungu cha maandiko kinaweza kikawa na maana nyingi, na wanaweza wakatumia kanuni moja ya injili kwenye hali tofauti za maisha. Waalike kutafakari jinsi kanuni za injili zinavyohusika kwa kila mmoja na kile kinachofanyika katika maisha yao. Himiza ushiriki na majadiliano ili waweze kujifunza kutokana na mitazamo ya kipekee ya kila mmoja.

Picha
mwanamke akifundisha darasa

Watu wazima wanaweza kushiriki uzoefu mwingi ambao umejenga imani yao kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Kuwafundisha Watu wenye Ulemavu

Msaidie Kila Mtu Akue na Aendelee

Joseph Smith alifundisha, “Akili zote na roho zote ambazo Mungu ametuma ulimwenguni zina uwezo wa kupanuka” (Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith [2007], 210). Chukulia kwamba watoto wote wa Mungu wanao uwezo wa kuongezeka katika maarifa na kukua. Mwombe Bwana akusaidie kujua jinsi ya kumsaidia watoto kila mtu.

Jifunze kuhusu Mahitaji Maalumu

Zungumza na wanafunzi au wazazi wao au walezi. Tafuta ni kwa jinsi gani kila mmoja anajifunza vizuri zaidi na mbinu zipi zina msaada zaidi. Ungeweza pia kushauriana na viongozi wengine na walimu ambao wana uzoefu na utambuzi wa kushiriki. Kwa ajili ya msaada wa mbinu za kufundishia, ona disabilities.ChurchofJesusChrist.org.

Tengeneza Mazingira Chanya

Tengeneza mazingira chanya ambapo kila mtu anahisi yuko salama na anapendwa. Usidhanie tu kuwa wanafunzi wote wenye ulemavu wako sawa, na mtendee kila mtu kwa upendo na heshima. Watie moyo wengine kuwa wakarimu na wenye kujali.

Hakikisha Kwamba Wote Wanaweza Kushiriki

Mabadiliko madogo madogo yanaweza kufanywa kwenye shughuli ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wote wanaweza kujifunza, ikijumuisha wale wenye mapungufu ya kimaumbile au wenye shida ya kujifunza. Kwa mfano, kama shughuli inapendekeza kuonesha picha, mnaweza kuimba wimbo unaohusiana kama mbadala ili kujumuisha wanafunzi wenye mapungufu ya kuona.

Imarisha Utaratibu na Muundo Endelevu wa Darasa

Njia moja ya kuweka utaratibu ni kutengeneza bango lenye ratiba. Ratiba yako inaweza kujumuisha sala, muda wa kufundisha, na muda wa shughuli. Kufuata ratiba kunaweza kusaidia kupunguza hisia za kutokuwa na uhakika na wasi wasi kwa baadhi ya wanafunzi

Elewa Kwa Nini Tabia zenye Kuleta Changamoto Hutokea.

Jifunze kuhusu ulemavu au hali ambazo zinaweza kushawishi mtu kutenda isivyofaa. Kuwa makini sana kwenye kile kinachofanyika wakati tabia zenye kuleta changamoto zinapojitokeza. Kwa sala fikiria jinsi ya kurekebisha hali ili kuwasaidia vizuri zaidi wanafunzi.

Kwa taarifa zaidi kuhusu kufundisha watu wenye ulemavu, ona disabilities.ChurchofJesusChrist.org.

Picha
Darasa la Wasichana

Walimu wanaweza kutengeneza mazingira chanya ya kujifunzia mahali ambapo kila mmoja atahisi kukubalika na kupendwa.

Kufundisha kwa Njia ya Mitandao

Jizoeze Kutumia Teknolojia

Kabla ya darasa au mkutano wako, tumia muda kiasi kupata ufahamu wa teknolojia ambayo utakuwa ukiitumia. Chunguza baadhi ya sehemu zake, kama vile jinsi ya kushiriki video au picha. Fikiria kufanya mkutano wa “jaribio” na wanafamilia au marafiki.

Kata nyingi na vigingi vina wataalamu wa teknolojia. Yawezekana pia ukawajua wengine wenye uzoefu na mikutano ya kimtandao. Omba ushauri wao au mwongozo.

Ondosha Uwezekano wa Vivurugaji

Ikiwezekana, tafuta sehemu tulivu ya kufanyia mkutano wako. Mwingiliano wa kelele unaweza kuwa wenye kuvuruga. Wahimize wanafunzi wafanye vivyo hivyo au kuzima vipaza sauti vyao ikiwa hawazungumzi.

Tumia Kamera

Ikiwezekana, iweke kamera yako ikiwa imewaka ili wanafunzi waweze kuona uso wako. Waalike (lakini usiwalazimishe) wanafunzi kuwasha kamera zao pia. Hii inaweza kusaidia kujenga roho ya umoja na kusaidiana.

Tumia Kipengele cha Virtual Chat

Mikutano mingi kwa njia ya mitandao huwaruhusu washiriki kuandika maswali au maoni kwenye dirisha la mazungumzo. Baadhi pia huwaruhusu washiriki kuinua mikono yao kwa njia ya mitandao. Waruhusu wanafunzi wajue kuhusu vipengele hivi. Unaweza kutaka kumpatia mtu mwingine kazi ya kuangalia mikono iliyoinuliwa au maoni katika chati ili uweze kufokasi usikivu wako kwenye kuongoza mjadala.

Tafuta Njia za Kuwashirikisha Wanafunzi

Kujifunza kwa njia ya mtandao wakati mwingine hufanya vigumu kwa watu kuonekana na kuwasikiliza. Fanya juhudi za makusudi za kuwashirikisha wale wanaotaka kushirikishwa. Wakati mwingine hii inamaanisha kutengeneza vikundi vidogo vidogo (kwa mfano, kwa kuvunja darasa kubwa la Shule ya Jumapili). Wakati mwingine inamaanisha kuwaomba wanafunzi kabla ya wakati kushiriki katika njia mahususi. Usiache ukomo wa teknolojia usababishe wewe kusahau kuhusu au kuwasahau watu ambao wanashauku na wako tayari kujifunza.

Chapisha