2022
Unganika
Machi 2022


“Unganika,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Machi 2022

Unganika

Adam L.

15, Jamaica

Picha
mvulana

Picha na Christina Smith

Wazazi wangu wananionyesha jinsi ya kuwa kama Kristo. Wakati wote wanasaidia watu!! Na wanapowahudumia wengine, hawalalamiki. Wanaitakasa siku ya Sabato. Pia wanasali kila asubuhi na usiku.

Ninajifunza vitu vingine kutoka kwa wazazi wangu. Baba yangu ni mwana sanaa mahiri. Yeye ni mzuri sana hasa katika kuchora kwa penseli. Ninaweka lengo ili kuboresha sanaa yangu, hivyo namtazama kwa karibu.

Lengo lingine nililonalo ni kupata alama nzuri shuleni. Wakati mwingine huwa na wasiwasi wakati wa mitihani. Wakati mmoja ulizidi sana, kwa hivyo nilisali. Baadaye, nilijisikia mwepesi na mwenye furaha ndani. Niliweza kufanya mtihani bila matatizo. Ninajua Roho Mtakatifu alinisaidia kuacha kuwa na woga.

Wakati mmoja nilikuwa katika mradi wa huduma kusaidia kuchora kuta za shule iliyo karibu. Mwanzoni sikutaka kuwapo, lakini hatimaye nilianza kujisikia vizuri kuhusu hilo. Sasa, kila ninapopita kwenye shule hiyo, inanifanya nijisikie wa kipekee. Ninajua niliwasaidia watoto pale.

Chapisha