2022
Nguvu ya Ukuhani katika Janga
Machi 2022


“Nguvu ya Ukuhani katika Janga,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mar. 2022.

Dhima na Mimi

Vijana wakielezea jinsi wanavyoishi maneno ya Dhima ya Wasichana na ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni

Nguvu ya Ukuhani katika Janga

“Nitampenda Mungu … na kutumia ukuhani Wake ili kuwatumikia wengine, nikianzia nyumbani mwangu mwenyewe.”

mkate na maji

Picha kutoka Getty Images

Tulipoanza kuhudhuria Kanisa nyumbani kwa sababu ya janga la UVIKO-19, nilisaidia kutoa sakramenti kwa familia yangu. Ilipendeza kuweza kufanya hivi nyumbani kwangu, na ilinifanya nitambue jinsi ninavyoshukuru kwa sakramenti. Ninashukuru kwamba niliweza kuishi wakati huu wa kuwa na kanisa nyumbani.

Mmoja wa majirani zetu alihitaji mtu wa kumletea sakramenti. Hakukuwa na mtu yeyote nyumbani kwake ambaye angeweza kuandaa au kubariki sakramenti kwa sababu mumewe alikuwa amefariki miaka michache iliyopita. Alikuwa pia akiwa mwangalifu kwa wageni kwa sababu ya janga hilo. Baba yangu na mimi ni kaka zake wanaomtumikia, kwa hivyo tulitaka kumpa sakramenti wakati amevaa barakoa na kuchukua tahadhari nyingine kwa usalama wake.

Alishukuru sana kwamba tungeweza kuja. Ilinifanya nihisi huzuni kidogo kwamba alikuwa mpweke, kwani alikuwa peke yake nyumbani kwake wakati wa janga hilo. Lakini pia nilishukuru kwamba ningeweza kumpa kitu muhimu sana kumfanya afurahi. Ilikuwa vizuri kuweza kumtumikia. Ilinifurahisha kuwa baba yangu na mimi tuliweza kwenda kumtumikia jirani yetu.

Ninashukuru kuwa na ukuhani kwa sababu hauninufaishi mimi tu bali pia watu wengine. Unanisaidia kuwa mtu bora na unanisaidia kuona jinsi ninavyoweza kuhudumia wengine. Kupitisha sakramenti nyumbani kwangu na kwa jirani yangu kulifungua macho yangu. Ninahitaji kutumia fursa hiyo kupitisha sakramenti na kuwahudumia watu ambao hawawezi kujifanyia wenyewe. Ninashukuru ningeweza kutumia ukuhani kubariki watu wengine na familia yangu.

Mwandishi anaishi Utah, Marekani.