2022
Roho Anaweza Kunisaidia Kujua Jinsi ya kuhudumu
Machi 2022


“Roho Anaweza Kunisaidia Kujua Jinsi ya Kuhudumu,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Machi 2022.

Dhima na Mimi

Vijana wakielezea jinsi wanavyoishi maneno ya Dhima ya Wasichana na ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni

Roho Anaweza Kunisaidia Kujua Jinsi ya Kuhudumu

“Kama mfuasi wa Yesu Kristo, ninajitahidi kuwa kama Yeye. Ninatafuta na kufanyia kazi ufunuo binafsi na kuwatumikia wengine katika jina Lake takatifu.”

Picha
msichana

Wakati wa janga la UVIKO-19, watu wengi walipata kipato cha chini au hata walipoteza kazi zao. Nilitaka kupunguza mzigo wao kidogo. Kwa msaada kutoka kwa mama na baba yangu, na kutumia pesa yangu binafsi, nilianza kuwapa chakula wale wanaohitaji. Kwa kawaida nilifanya hivi kwa kuagiza chakula kwa wengine kupitia programu ya teksi ya baiskeli. Wakati mwingine niliacha chakula kwenye maeneo yaliyotengwa kwa wale ambao wana uhitaji.

Nchini Indonesia kuna madereva wengi wa teksi za pikipiki. Tunatumia programu kwenye simu zetu ili kuweka nafasi kwa ajili ya huduma zao. Wakati wa janga hilo, madereva walikuwa na wakati mgumu kupata wateja.

Siku moja, nilifuata msukumo kutoka kwa Roho kumsaidia dereva fulani. Niliagiza chakula kwa kutumia programu ya teksi ya baiskeli. Lakini alipofika kwenye mgahawa kuchukua chakula, nilimtumia mazungumzo, nikimwambia kwamba chakula hicho kilikuwa hasa ni kwa ajili yake. Alishangaa na hakuamini kwamba kilikuwa kwa ajili yake. Niliposema ni kwa ajili yake, alinishukuru mara moja na kuniombea. Alisema angechukua chakula na kupeleka nyumbani kumpa mtoto wake. Alionekana kuwa mwenye furaha sana. Hii ilinifanya nifurahi sana pia!

Ingawa mimi na familia yangu pia tulikuwa tunakabiliwa na changamoto, nilisikiliza Roho na nikachagua kuhudumu. Tuliweza kupata shangwe na furaha, ambayo ilitusaidia kushinda changamoto zetu.

Ninashukuru sana kwa Roho Mtakatifu. Uzoefu huu unanikumbusha andiko kutoka Agano Jipya, Yohana 13:34: “Amri mpya nawapa, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi. nanyi mpendane vivyo hivyo.” Ninajua tunapomfuata Roho, tutapokea baraka za ajabu kutoka kwa Baba wa Mbinguni.

Mwandishi anaishi West Java, Indonesia.

Chapisha