2022
Vidokezo Vitatu vya Kupunguza Ubishi katika Familia Yako
Machi 2022


“Vidokezo vitatu vya Kupunguza Ubishi katika Familia Yako,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Machi 2022

Msaada wa Kimaisha

Vidokezo Vitatu vya Kupunguza Ubishi katika Familia Yako

Je, familia yako wakati mwingine hubishana? Hauko peke yako.

Picha
msichana
Picha
mvulana

Vielelezo na Alyssa M. Gonzalez

  • “Hivyo si haki! Sasa ni zamu yangu!”

  • “Hee, hukuomba kuazima hicho!”

  • “Baba! Anita alimetolea ulimi nje!”

Kama maneno kama hayo si mapya kwako, wewe unaweza kuwa sehemu ya familia. Na hakuna familia yenye kinga dhidi ya sehemu ya migogoro. Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili aliwahi kushiriki kwamba watoto wake waliwahi kulalamika, “Mama, huyu anapumua hewa yangu!”1

Ni kawaida kwa mabishano kuingia kwenye familia. Na kwa kweli, mtu hufanya kazi ya ziada ili kufanikisha hilo. Mwokozi alifundisha wazi, “Yule ambaye ana roho ya ubishi siye wangu, lakini ni wa ibilisi, ambaye ni baba wa ubishi, na huchochea mioyo ya watu kubishana na hasira mmoja kwa mwingine” (3 Nefi 11:29).

Lakini usiogope! Injili inatufundisha kwamba kuna mengi tunaweza kufanya ili kupunguza ubishi katika familia zetu—na kupata furaha nyingi!

Kidokezo cha 1: Ondoa Mafuta

Picha
msichana na kopo la mafuta

Moto unahitaji mafuta ili kuwaka. Ubishi ni ule ule. Na hakuna kitu kinachochochea ubishi kama kubishana zaidi. Kwa hivyo, unaweza kufanya nini ikiwa mtu anaanza kubishana nawe?

Naam, kiurahisi unaweza kukataa tu kubishana. Mwokozi ndiye mfano wetu kamili katika hili. Katika huduma Yake yote alichukiwa, kutendewa vibaya, alisalitiwa, na mwishowe alisulubiwa. Hata hivyo, hata wakati majibu yake yalikuwa ya nguvu na ya moja kwa moja, Yeye hakuwahi kuwa na roho ya ubishi. Na mwishowe Yeye hakupigana, hata wakati angeweza kuita “zaidi ya vikosi kumi na viwili vya malaika” kumsaidia Yeye (Mathayo 26:53). Badala yake, aliwaombea maadui zake, hata wakati akiwa msalabani (ona Luka 23:34).

Kukataa kubishana hukuruhusu wewe kuwa msikilizaji bora. Na wakati tunasikiliza vizuri, tunaweza kuwasiliana vizuri na kuwa wapatanishi. Kukataa kubishana pia ni pamoja na kujibu kwa sauti tulivu na kufanya kila tuwezalo kudhibiti hisia zetu.

Bila mafuta yaliyoongezwa, hoja nyingi na mabishano hupungua. Kama maandiko yanavyofundisha, “Jibu laini huondoa ghadhabu” (Mithali 15:1).

Kidokezo cha 2: Onyesha Upendo

Picha
familia

Kuonyesha upendo kwa wanafamilia wako ni mojawapo ya njia bora za kuzuia migogoro nyumbani. Kufanya hivyo kunaweza hata kuzuia ubishi usionekane mwanzoni!

Walakini hata wakati ubishi unaweza fanikiwa kwa kujihami kwetu, upendo na fadhili bado zinaweza kubadilisha mambo.

Fikiria hadithi ya mwanamke aliyepatikana katika uzinzi. Kulingana na sheria ya Musa, alipaswa apigwe mawe. Umati wa watu wenye hasira ulimtaka Yesu amhukumu.

Lakini jibu la Mwokozi lilikuwa lipi? Kwanza kabisa, hakujibu madai yao mara moja. Alipiga magoti na kuchora chini kwa muda kabla ya kusema. (Kidokezo: wakati mwingine ni bora kutojibu mara moja wakati mhemko uko juu.)

Halafu alionyesha upendo na huruma kwa yule mwanamke alipowaambia umati, “Yeye asiye na dhambi kati yenu, na atangulie kurusha jiwe “ (Yohana 8:7).

Yesu alimtendea mwanamke huyo kwa upendo, sio kulaani. Alionyesha utayari wake wa kumsamehe wakati alipomwalika “nenda, usitende dhambi tena” (Yohana 8:11).

Waambie wanafamilia wako kuwa unawapenda. Onyesha upendo huo kwa kuwasamehe na kuwaruhusu wabadilike—hata ikiwa wanakutendea kwa hasira. Upendo unaweza kuleta mabadiliko yote.

Kidokezo cha 3: Sali

Picha
msichana akisali

Sala huleta baraka za Mungu katika maisha yetu. Katika Kitabu cha Mormoni, Amuleki alifundisha, “Lazima mfungue roho zenu ndani ya vijumba vyenu, na mahali penu pa siri, na kwenye nyika zenu.

Ndio, … acha mioyo yenu ijae, mdumu katika sala kwake siku zote kwa ustawi wenu, na pia kwa ustawi wa wale ambao wako karibu nanyi” (Alma 34:26–27).

Hakika “wale walio karibu nawe” ni pamoja na familia yako—hata wale ambao hawawezi kuishi na wewe hivi sasa. Hivyo, sali na familia yako. Sali kwa ajili ya familia yako. Sali ili uweze kudhibiti hasira yako wakati mtu anakukasirisha. Sali kwamba uweze kujua jinsi ya kuchukulia hali ngumu zinazotokea katika familia yako. Sali kwa ajili ya msaada. Sali kwa ajili ya kicheko zaidi na upendo kuingia nyumbani kwenu. Na kisha fanya yote uwezayo kufanikisha hilo.

Unapojitahidi kuishi injili ya Yesu Kristo kikamilifu zaidi, utagundua kwamba familia yako pia itabarikiwa. Ubishi utapungua, na furaha yako itaongezeka.

Muhtasari

  1. David A. Bednar, mkutano mkuu wa Okt 2009 (Ensign au Liahona, Nov 2009, 19).

Chapisha