2022
Itakuwaje kama ninahisi juhudi zangu za kushiriki injili hazileti tofauti?
Machi 2022


Nifanye nini wakati ninapohisi juhudi zangu za kushiriki injili hazileti tofauti?” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Machi 2022.

Maswali na Majibu

“Nifanye nini wakati ninapohisi juhudi zangu za kushiriki injili hazileti tofauti?”

Fuata Mfano wa Kristo

Picha
msichana

“Wakati mmoja mwalimu wangu alisema Mungu hayupo. Nilikuwa nikisoma Kitabu cha Mormoni kila siku na nilijua kile alichokuwa akisema hakikuwa kweli. Nilijaribu kushiriki ushuhuda wangu, lakini hakuwa ananisikiliza. Nimejifunza matendo yangu yanazungumza zaidi kuliko maneno yangu. Marafiki zangu wananiunga mkono sana katika viwango. Daima wananiangalia kwa sababu mimi ni muumini wa Kanisa.

Valeria F., 18, Honduras

Omba Msaada

Picha
mvulana

Kuna mamia ya njia za kushiriki injili. Wakati mwingine juhudi zako zote hazitakuhakikishia kwamba rafiki zako watakuunga mkono. Hauko peke yako. Omba msaada kwa Baba yako wa Mbinguni na Mwokozi. Unaweza kugundua kitu kipya.”

Banri O., 15, Japan

Kuwa Mfano Mzuri

Picha
msichana

“Daima nakumbuka ushauri wa viongozi wangu: ‘Kuwa mfano ni mojawapo ya njia bora ya kushiriki injili.’ Ikiwa tunajitahidi kuweka mfano mzuri na kuwa nuru kwa wengine, itakuwa rahisi kwetu kushiriki injili na watu wengi. Kuwa mwakilishi wa Yesu Kristo kunaweza kuleta baraka kubwa maishani mwetu na kwa wale wanaotuzunguka.

Bonnie Q., 16, Bolivia

Ni Uchaguzi Wao

Picha
msichana

“Nimekataliwa mara nyingi wakati nimeshiriki injili. Kusema kweli, wakati mwingine ninahisi huzuni kwa sababu sioni matokeo yoyote. Nimejifunza kwamba sio kosa langu wakati watu hawakubali injili. Ni uchaguzi wao, na napaswa kuwa mvumilivu. Baadaye juhudi zangu zinaweza kuleta mabadiliko. Ninaweza kuwaombea watu ninaowaalika kila wakati.

Cristina B., 18, Romania

Fundisha na Utende Kama Kristo

Picha
mvulana

Tunaweza kufikiria njia mpya, za kufurahisha za kushiriki injili. Kwa mfano, tunaweza kujifunza kutoka kwenye njia ambayo Yesu Kristo alihubiri kupitia mifano na vitendo. Matendo yetu yanaonyesha sisi ni akina nani na viwango vyetu.”

Johann S., 16, Bolivia

Kuwa Mvumilivu

“Nimekataliwa mara nyingi wakati nimeshiriki injili. Kusema kweli, wakati mwingine ninahisi huzuni kwa sababu sioni matokeo yoyote. Nimejifunza kwamba sio kosa langu wakati watu hawakubali injili. Ni uchaguzi wao, na napaswa kuwa mvumilivu. Baadaye juhudi zangu zinaweza kuleta mabadiliko. Ninaweza kuwaombea watu ninaowaalika kila wakati.

Cristina B., 18, Romania

Endelea kujaribu

Mara nyingi ninapowaalika marafiki zangu kuja kanisani Jumapili, hukataa mwaliko. Ni ngumu kukataliwa, lakini ninaposoma maandiko, najua kwamba kila kitu tunachofanya kwa wengine, tunamfanyia Yesu Kristo. Ninaamini kwamba kuwa na uvumilivu ndio ufunguo. Hatuwezi kujua ni lini maneno tunayoshiriki yanaweza kuwabariki watu.”

Valeria V., 14, Bolivia

Sali kwa Ajili Yao

“Njia rahisi ya kushiriki injili ni kwa kuonyesha upendo wako kwa marafiki zako. Unaweza kusali kwa ajili ya ujasiri wa kushiriki injili. Unaweza pia kuwaombea wawe na uelewa mzuri wa ujumbe wa injili.”

Yuria K., 18, Japan

Chapisha