“Je, Unamsikilizaje Yeye?,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Machi 2022.
Neno la Mwisho
Je, Unamsikilizaje Yeye?
Kutoka kwenye hotuba ya mkutano mkuu wa Aprili 2020.
Pamoja na mwongozo wa amani tunaoupata kutoka kwa Roho Mtakatifu, muda baada ya muda, Mungu anatuhakikishia kwa nguvu na kila mmoja kibinafsi kwamba Anatujua na kutupenda. Kisha, katika nyakati zetu za magumu, Mwokozi huleta uzoefu huu tena katika akili zetu.
Fikiria juu ya maisha yako mwenyewe. Uzoefu huu unaweza kuja katika nyakati muhimu maishani mwetu au katika kile ambacho mwanzo kinaweza kuonekana kama matukio yasiyovutia. Kumbukumbu hizi za kuelezeka kiroho huja kwa nyakati tofauti na katika njia tofauti, zikiwa maalum kwa kila mmoja wetu.
Joseph Smith alielezea kwamba wakati mwingine sisi tunapokea “mpapaso wa ghafla wa mawazo” na mara chache “utiririkaji halisi wa maarifa.”1
Rais Dallin H. Oaks, katika kumjibu mwanaume ambaye alidai kamwe hakuwahi kuwa na uzoefu kama huo, alishauri, “pengine sala zako zimekuwa zikijibiwa tena na tena, lakini umekuwa na matarajio yako yaliyojikita kwenye ishara kubwa au sauti kubwa sana kwamba unadhani hujapata jibu.”2
Tumemsikia hivi karibuni Rais Russell M. Nelson akisema: “Ninakualikeni kufikiria kwa kina na mara nyingi kuhusu swali hili la msingi: Ni kwa jinsi gani wewe unamsikiliza Yeye? Mimi pia ninakualikeni kuchukua hatua za kumsikiliza Yeye vizuri zaidi na mara nyingi zaidi.”3