2022
Sauti ya Linahei
Machi 2022


“Sauti ya Linahei,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Machi 2022.

Sauti ya Linahei

Kuanzia muziki hadi historia ya familia, Linahei anatumia sauti yake vizuri.

Picha
msichana akiwa ufukweni

Picha na Stephane Sayeb; vielelezo na Claire Lock

Linahei D. kutoka Tahiti anajua jinsi ya kutumia sauti yake kuwabariki wengine—kwa njia zaidi ya moja. Kwa mfano, anasoma kuwa mtaalamu wa lugha siku moja. “Ninataka kuwasaidia watoto katika uandishi wao au jinsi wanavyozungumza,” anasema.

Huo ni mwanzo tu, hata hivyo. Akiwa amezaliwa kwenye familia ya wanamuziki wenye vipaji, Linahei wa miaka 14 anapata nafasi nyingi za kutumia sauti yake kwa kuimba. “Kaka yangu na mimi tunapenda kuimba pamoja. Kawaida yeye huimba sauti ya juu, na mimi huimba ya chini!”

Na kuna okestra nzima ya familia, pia. “Mama yangu hucheza piano kutusaidia kutufundisha nyimbo, na baba yangu hucheza gita na ukulele.” Na orchestra ya familia ni nini bila ngoma? “Mimi na baba yangu tunapenda kucheza to‘ere, ambayo ni ngoma ya jadi ya Polynesia.”

Picha
msichana akicheza ukulele

Pamoja na mkusanyiko mzima ukimuunga mkono, familia yake humsaidia zaidi ya muziki pekee. “Wazazi wangu kila wakati hunihimiza katika masomo yangu, na baba yangu hunipa baraka za ukuhani.” Wakati wa nyakati ngumu unapokuja, anajua anaweza pia kumgeukia Baba yake wa Mbinguni. “Ninajua ni kwa jinsi gani Bwana hunipenda na kwamba siku zote yupo kwa ajili ya watoto Wake.”

Picha
familia ikiimba na kucheza muziki

Linahei sio tu anatumia sauti yake kwa muziki na sala, lakini pia anaongea juu ya kusaidia wanafamilia upande wa pili wa pazia.

Sauti ya Upendo kwa Familia iliyopo nyuma ya Pazia

“Niliota ndoto usiku mmoja ambapo niliona mamia ya watu, lakini wasioweza kuwasiliana wao kwa wao,” anasema. “Nilidhani ninawatambua, lakini sikuwa na uhakika.”

Linahei hakujua nini maana ya ile ndoto mwanzoni. Halafu alikuwa na mawazo ya kufurahisha: “Kabla ya zuio la UVIKO-19, nilikuwa nimefanya ubatizo zaidi ya 100 kwa niaba ya mababu zangu—watu hawa katika ndoto yangu wanaweza kuwakilisha wale wana familia!”

Picha
msichana akiwa na picha ya mababu

Kuhisi kufurahishwa zaidi na historia ya familia kuliko hapo awali, Linahei alifanya kila awezalo kusaidia kupeleka majina hayo kwenye hekalu kupokea ibada zao za ziada. Hivi karibuni, Linahei na mama yake waliitwa kama washauri wa historia ya familia katika kata yao.

“Tulimsaidia mwanamke katika kata yetu kupata akaunti yake ya FamilySearch. Alipoona mti wa familia yake, alifurahi sana—ilikuwa mara yake ya kwanza kuona mababu zake wote!”

Picha
msichana na mama wakifanya historia ya familia

“Nilikuwa najisikia wasiwasi kwenda kwa watu katika kata yangu,” Linahei anakubali. “Lakini kwa kuwa sasa nipo na mama yangu, ninahisi ujasiri zaidi kuwafundisha watu juu ya historia ya familia.”

Paza Sauti Yako

Picha
msichana

Sasa Linahei anatarajia kusaidia watu kujifunza juu ya mababu zao. “Ninapenda kuona jinsi watu wanavyofurahi wanapofanya historia ya familia zao. Na nadhani mababu zetu wanafurahi kwamba tunawapenda na kutekeleza maagizo yao.

Katika wito wake kama mshauri wa historia ya familia, hivi karibuni aliandaa shughuli kwa wasichana wa kata yake. Sio tu kwamba aliwasaidia kupata majina ya familia kwenda nayo hekaluni, lakini pia aliwasaidia watoto wa Msingi kuanzisha akaunti ili waweze kushiriki.

“Tunakwenda hekaluni hivi karibuni,” anasema.

Picha
msichana na mama wakiwa hekaluni

Unataka kuwa vizuri kama Linahei? Usijali, inawezekana kabisa. “Vijana wanaweza kuendeleza ujumbe wa Mungu kwa kutumia teknolojia,” Linahei anasema. Chochote kinachotusaidia kuwafikiria babu zetu ni kizuri. Najua kufanya historia ya familia kutamletea kila mtu furaha zaidi katika maisha yao. Historia ya familia imenileta karibu na mababu zangu na Kristo wakati huo huo.”

Pamoja na kazi yote anayowafanyia mababu zake, jambo moja ni hakika: Familia ya Linahei hakika sio historia tu!

Chapisha