2022
Kwa nini Mungu alibadilisha jina la Yakobo kuwa Israeli?
Machi 2022


“Kwa nini Mungu alibadilisha jina la Yakobo kuwa Israeli?,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Machi 2022

Kwenye Hoja

Kwa nini Mungu alibadilisha jina la Yakobo kuwa Israeli?

msichana

Mchoraji ni Keith Larson

Yakobo alikuwa mwana wa Isaka na mjukuu wa Ibrahimu. Kama wao, Yakobo alikuwa na nia ya haki na alitafuta baraka za Bwana.

Katika wakati muhimu maishani mwake, “Yakobo alipambana na changamoto kubwa. Haki yake ya kujiamulia ilijaribiwa. Kupitia mweleka huu, Yakobo alithibitisha kile kilichokuwa muhimu zaidi kwake. Alionyesha kwamba yeye alikuwa radhi kuacha Mungu ashinde katika maisha yake. Katika kujibu, Mungu alibadilisha jina la Yakobo kuwa Israeli, maana yake “acha Mungu ashinde.” Kisha Mungu alimwahidi Israeli kwamba baraka zote ambazo zilikuwa zimetajwa juu ya kichwa cha Ibrahimu zitakuwa zake pia.” (Russell M. Nelson, “Acha Mungu Ashinde,” Okt. 2020 mkutano mkuu [Ensign au Liahona, Nov. 2020, 92]). Kuchukua jina hili jipya ilikuwa ishara ya kupokea agano ambalo baba yake na babu yake walikuwa wamepokea.

Wakati tunapobatizwa, tunafanya maagano. Pia tunaonyesha kwamba tuko radhi kujichukulia juu yetu jina jipya—jina la Yesu Kristo. Kwa kuongezea, tunakuwa sehemu ya nyumba ya Israeli—wale ambao wamefanya maagano na Mungu na wameahidi “kumruhusu Mungu ashinde” katika maisha yao. Kisha Mungu anatuahidi baraka zile zile alizomuahidi Ibrahimu, Isaka, na Yakobo.