2010–2019
Upinzani Katika Mambo Yote
Aprili 2016


15:27

Upinzani Katika Mambo Yote

Upinzani unaturuhusu kukua kuelekea kwa kile Baba yetu wa Mbinguni angetaka tuwe.

Kitovu cha injili ya Yesu Kristo ni mpango wa wokovu wa Baba kwa ajili ya ukuaji wa milele wa watoto Wake. Mpango huo, ilivyoelezwa katika ufunuo wa kisasa, unatusaidia kuelewa mambo mengi tunayokabiliana nayo katika maisha haya. Ujumbe wangu unalenga nafasi muhimu ya upinzani katika mpango huo.

I.

Madhumuni ya maisha ya dunia kwa watoto wa Mungu ni kutoa uzoefu unaohitajika “kuendelea kwenye ukamilifu na hatimaye kufikia hatima yao ya kiungu kama warithi wa uzima wa milele.”1 Kama Rais Thomas S. Monson alivyotufundisha kwa uwezo sana asuhubi ya leo, tunaendelea kwa kufanya chaguo, kwa kujaribiwa ili kuonyesha kwamba tutachagua kuweka amri za Mungu (ona Ibrahimu 3:25). Ili kujaribiwa ni lazima tuwe na wakala wa kuchagua kati ya njia mbadala. Ili kutoa mbadala ambao kwao tunaweza kutekeleza haki yetu ya kujiamulia, lazima kuwe na upinzani.

Sehemu iliyosalia ya mpango wote ni muhimu pia. Tunapofanya uchaguzi mbaya—kwa kuwa tutafanya—tunachafuliwa na dhambi na ni lazima tusafishwe ili kuendelea kuelekea kwenye hatima yetu ya milele. Mpango wa Baba hutoa njia ya kufanya hivyo, njia ya kukidhi mahitaji ya milele ya haki: Mwokozi analipa dhamana ya kutukomboa kutoka katika dhambi zetu. Mwokozi huyo ni Bwana Yesu Kristo, Mwana wa pekee wa Mungu Baba wa Milele, ambaye dhabihu Yake yake ya upatanisho—ambaye mateso Yake—hulipia gharama ya dhambi zetu kama tutatubu.

Mojawapo ya maelezo bora ya nafasi iliyopangwa ya upinzani ni katika Kitabu cha Mormoni, katika mafundisho ya Lehi kwa mwanawe Yakobo.

“Kwani lazima, kuwe na upinzani katika vitu vyote. Kama si hivyo, … utakatifu haungepatikana, wala uovu, wala utakatifu au hofu, wala uzuri au ubaya” (2 Nefi 2:11, tazama pia mstari wa 15).

Matokeo yake, Lehi aliendelea, “Kwa hivyo, Bwana Mungu amemruhusu mwanadamu kujitendea mwenyewe. Kwa hivyo, mwanadamu hangeweza kujitendea mwenyewe bila kuvutiwa na moja au nyingine.”(mstari 16). Vile vile, katika ufunuo wa kisasa Bwana anatangaza, “Na hapana budi kwamba ibilisi lazima awajaribu wanadamu, vinginevyo hawangeweza kujiamulia wao wenyewe” (M&M 29:39).

Upinzani ulikuwa muhimu katika bustani ya Edeni. Kama Adamu na Hawa hawangefanya uchaguzi ambao ungeleta maisha ya dunia, Lehi alifundisha, “wangeishi katika hali ya kitoto, … bila kutenda mema, kwani hawakujua dhambi.” (2 Nefi 2:23).

Tangu mwanzo, wakala na upinzani vilikuwa muhimu kwa mpango wa Baba na kwa uasi wa Shetani dhidi ya mpango huo. Kama vile Bwana alivyomfunulia Musa, katika baraza ya mbinguni Shetani “akatafuta kuangamiza haki ya mtu ya kujiamulia” (Musa 4:3). Uharibifu huo ulikuwa ni asili kulingana na toleo la Shetani. Alikuja mbele ya Baba akasema, “Tazama, niko hapa, nitume mimi, nitakuwa mwanao, nami nitawakomboa wanadamu wote, ili hata nafsi moja isipotee, na hakika nitatenda hivyo; kwa sababu hiyo nipe mimi heshima yako.” (Musa 4:1).

Hivyo, Shetani akapendekeza kutekeleza mpango wa Baba kwa njia ambayo ingezuia kufanikiwa kwa kusudi la Baba na kumpa Shetani utukufu Wake.

Pendekezo la Shetani lingehakikisha usawa kamili: “lingewakomboa watu wote,” ila hata nafsi moja haingepotea. Hapangekuwa na wakala au uchaguzi na mtu yeyote na, kwa hiyo, hakuna haja ya upinzani. Hapangekuwa na majaribio, kushindwa, na mafanikio. Hapangekuwa na ukuaji wa kufikia lengo ambalo Baba alitaka kwa ajili ya watoto Wake. Maandiko yanaandikwa kwamba upinzani wa Shetani ulisababisha “vita mbinguni” (Ufunuo 12:7), ambapo watu wote ila tu thuluthi ya watoto wa Mungu walistahili haki ya kuona maisha ya duniani kwa kuchagua mpango wa Baba na kukataa uasi wa Shetani.

Madhumuni ya Shetani yalikuwa ni kujichukulia mwenyewe heshima na uwezo wa Baba (Ona Isaya 14:12–15; Musa 4:1, 3). “Kwa hiyo,” Baba alisema, “kwa sababu yule Shetani aliasi dhidi yangu, … nikamfanya atupwe chini” (Musa 4:3) na nafsi zote zilizotekeleza wakala wao kumfuata (ona Yuda 1:6; Ufunuo 12:8–9; M&M 29:36–37). Kutupwa chini kama roho zisizokuwa na miili duniani, Shetani na wafuasi wake wanajaribu na kutafuta kudanganya na kuwaongoza utumwani watoto wa Mungu (ona Musa 4:4). Ndiposa yule mwovu, ambaye alitaka kuharibu mpango wa Baba, kwa kweli aliuwezesha, kwa sababu ni upinzani ambao huwezesha uchaguzi na ni fursa ya kufanya uchaguzi wa haki ndiyo huongoza kwa ukuaji ambao ni madhumuni ya mpango wa Baba.

II.

Cha muhimu, majaribu ya kufanya dhambi sio aina pekee ya upinzani katika maisha. Baba Lehi alifundisha kwamba kama Kuanguka haungefanyika, Adamu na Hawa “wangeishi katika hali ya kitoto, bila shangwe, kwani hawakufahamu dhiki” (2 Nefi 2:23). Bila uzoefu wa upinzani duniani, “vitu vyote lazima viwe kitu kimoja” ambayo kwayo hapatakuwa na furaha wala dhiki (mstari 11). Kwa hivyo, Baba Lehi aliendelea, baada ya Mungu kuumba vitu vyote “ili kutimiza makusudio yake ya milele katika, … ilibidi lazima kuwe na upinzani, hata tunda lililokataliwa kinyume cha mti wa uzima; mmoja ukiwa mtamu na mwingine ukiwa chungu.” (mstari 15).2 Mafundisho yake juu ya sehemu hii ya mpango wa wokovu inamalizika kwa maneno haya:

“Lakini tazama, vitu vyote vimetendwa kwa hekima ya yule ajuaye vitu vyote.

“Adamu alianguka ili wanadamu wawe; na wanadamu wapo, ili wapate shangwe” (mstari 24–25).

Upinzani katika umbo la hali gumu inayotukabili duniani pia ni sehemu ya mpango ambao unaendeleza ukuaji wetu duniani.

III.

Sisi sote tunapitia aina mbali mbali ya upinzani unaotujaribu. Baadhi ya majaribio haya ni majaribu ya kufanya dhambi. Baadhi ni changamoto za maisha mbali na dhambi za kibinafsi. Baadhi ni kubwa sana. Baadhi ni ndogo. Baadhi zinaendelea, na baadhi ni matukio tu. Hakuna hata mmoja wetu aliyesamehewa. Upinzani unaturuhusu kukua kuelekea kwa kile Baba yetu wa Mbinguni angetaka tuwe.

Baada ya Joseph Smith kukamilisha kutafsiri Kitabu cha Mormoni, ilimbidi apate mchapishaji. Hii haikuwa rahisi. Mchangamano wa muswada huu mrefu na gharama za uchapishaji na kungandisha maelfu ya nakala haikuwa rahisi. Kwanza, Joseph alimwendea E. B. Grandin, mchapishaji wa Palmyra, ambaye alikataa. Kisha akatafuta mchapishaji mwingine huko Palmyra, ambaye pia alikataa. Alisafiri hadi Rochester, maili 25 (40 km) mbali, na kukutana na mchapishaji maarufu zaidi katika magharibi mwa New York, ambaye pia alikataa. Mchapishaji mwingine wa Rochester alikuwa tayari, lakini hali ilifanya huu mpangilio kutowezekana.

Wiki zilikuwa zimepita, na Joseph lazima alikuwa ameshangazwa kutokana na upinzani katika kutimiza kazi yake takatifu. Bwana hakuifanya kuwa rahisi, lakini Yeye aliiwezesha. Jaribio la tano la Joseph, ilikuwa ni safari ya pili kwa mchapishaji wa Palmyra aitwaye Grandin, ambayo ilifanikiwa.3

Miaka baadaye, Joseph alifungwa jela kwa uchungu huko jela ya Liberty kwa miezi mingi. Alipoomba ili kupata nafuu, Bwana alimwambia kwamba “mambo haya yote yatakupa wewe uzoefu, na yatakuwa kwa faida yako” (M&M 122:7).

Sisi sote tunafahamu aina kadha ya upinzani katika maisha usiosababishwa na dhambi zetu binafsi, ikiwemo magonjwa, ulemavu, na kifo. Rais Thomas S. Monson alielezea:

“Baadhi yenu pengine mnaweza kuwa mmelia katika mateso yenu, mkishangaa ni kwa nini Baba yetu wa Mbinguni amewaruhusu kupitia aina yoyote ya majaribio yanayowakabili. …

“Maisha yetu ya dunia, hata hivyo, hayakukusudiwa kuwa rahisi au yenye raha mfululizo. Baba yetu wa Mbinguni … anajua kwamba tunajifunza na kukua na kunolewa kupitia kwa changamoto ngumu, huzuni wa kuvunja moyo, na maamuzi mazito. Kila mmoja wetu anapitia siku za giza wakati wapendwa wetu wanapokufa, wakati mgumu wakati afya zetu zinadhoofika, hisia ya kuachwa wakati wale tunaowapenda wanaonekana kutuacha. Haya na majaribu mengine yanatukabili na mtihani halisi wa uwezo wetu wa kuvumilia.”4

Juhudi zetu za kuboresha maadhimisho yetu ya siku ya Sabato zinaleta mfano rahisi wa upinzani. Tuna amri ya Bwana ya kuheshimu Sabato. Baadhi ya chaguzi zetu zinaweza kukiuka amri hiyo, lakini chaguzi zingine katika jinsi ya kutumia muda wakati wa Sabato ni tu swala la kama tutafanya kitu chema au kile bora au bora zaidi.5

Ili kuonyesha upinzani wa majaribu, Kitabu cha Mormoni kinaeleza mbinu tatu ambazo Ibilisi atatumia katika siku za mwisho. Kwanza, “atatawala katika mioyo ya watoto wa watu, na kuwakoroga kuwa na hasira dhidi ya yaliyo mema” (2 Nefi 28:20). Pili, “atawatuliza, na kuwaliwaza [waumini] mbali katika usalama wa kidunia,” akisema “Sayuni inanawiri, yote ni mema” (mstari wa 21). Tatu, atatuambia “hakuna kuzimu; na … mimi si shetani, kwa maana hamna shetani” (mstari 22), na kwa hiyo hakuna mema na mabaya. Kwa sababu ya upinzani huu tunaonywa ”tusilegee katika Sayuni!” (mstari 24).

Kanisa katika utume wake mtakatifu na sisi katika maisha yetu binafsi tunaonekana kupitia upinzani mwingi. Labda kadri Kanisa linavyokua kwa nguvu na sisi waumini tunakua katika imani na utii, Shetani anaongeza uwezo wa upinzani wake hivyo tutaendelea kuwa na “upinzani katika mambo yote.”

Baadhi ya upinzani huu hata hutoka kwa waumini wa Kanisa. Baadhi ambao hutumia uelewa binafsi au hekima ili kupinga mwelekeo wa kinabii hujipatia wenyewe jina lililokopwa kutoka kwa vikundi vilivyochanguliwa—“wapinzani waaminifu.” Hata hivyo kama ni sahihi kwa demokrasia, hakuna kibali kwa dhana hili katika serikali ya ufalme wa Mungu, ambapo maswali yanaheshimiwa na wala sio upinzani (ona Mathayo 26:24).

Kama mfano mwingine, kuna mambo mengi katika historia yetu ya zamani ya Kanisa, kama vile kile Joseph Smith alifanya au hakufanya katika kila hali, ambayo baadhi wanatumia kama msingi wa upinzani. Kwa wote nasema, ishi imani na uweke mategemeo kwenye mafundisho ya Mwokozi kwamba tunapaswa “Kuwatambua kwa matunda yao” (Mathayo 7:16). Kanisa linafanya juhudi kubwa ili kuwa na uwazi na rekodi tulizonazo, lakini baada ya yote tunayoweza kuchapisha, washiriki wetu wakati mwingine wanaachwa na maswali ya muhimu ambayo hayawezi kutatuliwa na utafiti. Hiyo ndiyo maoni ya historia ya Kanisa juu ya “upinzani katika mambo yote.” Mambo mengine yanaweza tu kueleweka kwa imani (ona M&M 88: 118). Tegemeo letu la mwisho lazima liwe ni imani katika ushahidi tuliopokea kutoka kwa Roho Mtakatifu.

Mungu ni nadra akiuke wakala wa yoyote ya watoto Wake kwa kuingilia kati dhidi ya baadhi kwa msaada wa wengine. Lakini Yeye hupunguza mizigo ya mateso yetu na kutuimarisha kuyabeba, kama alivyofanya kwa watu wa Alma katika nchi ya Helamu (ona Mosia 24: 13–15). Yeye hazuii majanga yote, lakini Yeye hujibu maombi yetu kuyageuza yaelekee mbali, jinsi alivyofanya na kimbunga cha kipekee ambacho kilitishia kuzuia kuwekwa wakfu kwa hekalu katika Fiji;6 ama anavyokomesha madhara yake, kama alivyofanya bomu la magaidi lililoangamiza maisha ya wengi sana huko uwanda wa ndege wa Brussels lakini liliwajeruhi tu wamisionari wetu wanne.

Kupitia kwa upinzani wote wa maisha, tuna uhakikisho wa Mungu kwamba “atabariki mateso [yetu] kwa faida [yetu]” (2 Nefi 2:2). Pia tumefundishwa kuelewa uzoefu wetu wa dunia na amri Zake kwenye muktadha wa mpango Wake mkubwa wa wokovu, ambao unatuambia lengo la maisha na unatupa uhakika wa Mwokozi, ambaye katika jina lake nashuhudia ukweli wa mambo haya. Katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. “The Family: A Proclamation to the World,” Liahona, Nov. 2010, 129.

  2. Vile vile, unabii wa kisasa unafundisha kuwa kama kamwe hatungepata machungu, hatungeweza kujua utamu (ona Mafundisho na Maagano 29:39).

  3. Ona Michael Hubbard MacKay and Gerrit J. Dirkmaat, From Darkness unto Light: Joseph Smith’s Translation and Publication of the Book of Mormon (2015), chapter -79.

  4. Thomas S. Monson, “Joy in the Journey” (address given at the BYU Women’s Conference, May 2, 2008), womensconference.ce.byu.edu. Insha fupi kuhusu uanamichezo na demokrasia ya John S. Tanner, kwa sasa ni rais waBYU–Hawaii, inajumuisha umaizi huu juu ya mada amayo sisi sote tunaifahamu: “Kujifunza kukubali kushindwa kwa heshima siyo tu jukumu la kiraia; bali nisharti la kidini. Mungu alisanifu maisha ya duniani ili kuhakikisha “upinzani katika mambo yote’ (2 Nephi 2:11). Vikwazo na ushinde ni sehemu ya mpango Wake kwa ulinzi wetu. … Ushinde ni sehemu muhimu katika ‘utafutaji wa ukamilifu’” (Maandishi ya Mwanagenzi: A Disciple’s Life in the Academy [2011], 57).

  5. Ona Dallin H. Oaks, “Good, Better, Best,” Liahona, Nov. 2007, 104–8.

  6. Ona Sarah Jane Weaver, “Rededication Goes Forward,” Church News, Feb. 28, 2016, 3.