2021
Gaëtan Kelounou
Septemba/ Oktoba 2021


WASIFU WA SABINI WA ENEO

Gaëtan Kelounou

Gaëtan Kelounou aliitwa kama Sabini wa Eneo mnamo Aprili 2021. Mzee Kelounou anatokea Brazzaville, Jamhuri ya Kongo. Kwa sasa anatumikia Kanisa kama mratibu wa Seminari na Vyuo vya Dini.

Kabla ya hapo, alifanya kazi kwa miaka minne kama Mkurugenzi wa Operesheni ya Mafuta kwa Mashirika ya Afrika ya Mafuta na Gesi. Mzee Kelounou ana Shahada ya Kwanza katika Mitandao na Mawasiliano ya Simu.

Kabla ya wito huu, alikuwa akihudumu kama mshauri katika Urais wa Misheni ya Jamhuri ya Kongo Brazzaville. Miito yake ya awali inajumuisha kuhudumu kama mmisionari, askofu, mshauri mkuu, mshiriki wa urais wa misheni na mshiriki wa urais wa kigingi. Alikuwa pia msaidizi wa masuala ya fedha wa Misheni ya Jamhuri ya Kongo Kinshasa huko Brazzaville kwa miaka tisa.

Mzee Kelounou na mkewe, Cornelie Omfoura, ni wazazi wa watoto sita. Kwa sasa wanaishi Brazzaville, Jamhuri ya Kongo.

Mzee Kelounou anasema kwamba ana shukrani nyingi kwa fursa hii mpya ya kuhudumu kama shahidi wa Bwana na kuwa chombo katika mikono Yake, “si tu kusaidia kazi Yake isonge mbele bali pia kuigeuza mioyo ya wanadamu Kwake kwa ajili ya wokovu wao,” anasema. “Ninajua Russell M. Nelson ni Nabii wa kanisa Lake na nina shukrani nyingi kuwa nao katika maisha yangu.”