WASIFU WA SABINI WA ENEO
Alfred Kyungu
Alfred Kyungu Kibamba alizaliwa huko Kamina, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, mnamo Oktoba 31, 1966.
Amefanya kazi katika nyadhifa mbalimbali katika serikali ya Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo na katika Kanisa kama mratibu na mkurugenzi wa kanda wa Seminari na Chuo na kama meneja wa historia ya familia.
Mzee Kyungu ana Shahada ya kwanza na ya pili za Sayansi katika Sayansi za Jamii na Mahusiano ya Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Lubumbashi.
Akiwa kama Sabini wa Eneo wakati wa kupokea wito wake, pia amehudumu kama mwalimu wa chuo, karani wa wilaya, mwalimu wa Shule ya Jumapili wa kata, rais wa Shule ya Jumapili wa kata, mshauri kwenye uaskofu, mshauri mkuu, mshauri katika urais wa kigingi na rais katika Misheni ya Mbuji-Mayi Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo toka 2016 mpaka 2019. Mzee Kyungu na mkewe, Lucie Kabulo Malala, ni wazazi wa watoto watatu.
Katika jukumu hili jipya, Mzee Kyungu anasema anatazamia “kuonyesha upendo wa Baba yetu wa Mbinguni, na kushiriki mafundisho na mfano wa Mwokozi pamoja na kila mtu”. Mzee Kyungu anasema hamu yake ni kuualika ulimwengu kuja kwa Kristo na kusikiliza sauti Yake; kuyapekua maandiko kwa bidii na kupokea majibu ya maswali kupitia kipawa cha Roho Mtakatifu.