2022
Lakini Hatukuwasikiliza
Mei 2022


“Lakini Hatukuwasikiliza,” Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2022.

Kikao cha Jumamosi Asubuhi

Lakini Hatukuwasikiliza (1 Nefi 8:33)

Dondoo

bango la mmea ukikua kwenye mwamba

Pakua PDF

Neno sikiliza hupendekeza kutilia maanani au kuweka umakini kwa mtu fulani au jambo fulani. …

Mafundisho ya Kristo yaliyoandikwa “kwa Roho wa Mungu aliye hai … katika mbao za nyama za [mioyo yetu]” [2 Wakorintho 3:3] huongeza uwezo wetu wa “kutosikiliza” vishawishi vinavyovuruga mawazo, dhihaka na upotoshaji mwingi katika ulimwengu wetu ulioanguka. …

Msimamo wa kuishi na kupenda maagano hujenga uhusiano na Bwana ambao ni wa kina na binafsi na wenye nguvu kiroho. …

Uhusiano wetu wa agano kwa Mungu na Yesu Kristo ndiyo njia ambayo kupitia kwayo sisi tunaweza kupokea uwezo na nguvu ya “kutosikiliza.” Na muunganiko huu unaimarishwa kadiri tunavyoendelea kushikilia kwa nguvu ile fimbo ya chuma. …

Wacha nipendekeze kwamba kushikilia kwa nguvu neno la Mungu kunahitaji (1) kukumbuka, kuheshimu na kuimarisha uhusiano binafsi tulionao kwa Mwokozi na Baba Yake kupitia maagano na ibada za injili ya urejesho na (2) kwa maombi, kwa dhati na kwa uaminifu kabisa kutumia maandiko matakatifu na mafundisho ya manabii na mitume walio hai kama vyanzo vya uhakika vya ukweli uliofunuliwa. …

Songa mbele. Shikilia kwa nguvu. Usisikilize

Ninatoa ushahidi kwamba uaminifu kwenye maagano na ibada za injili ya urejesho ya Mwokozi vinatuwezesha kusonga mbele katika kazi ya Bwana, kushikilia kwa nguvu kwake Yeye kama Neno la Mungu na kutosikiliza vivutio vya adui.