“Kila Mmoja Wetu Ana Hadithi,” Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2022.
Kikao cha Jumamosi Alasiri
Kila Mmoja Wetu Ana Hadithi
Dondoo
Marafiki, akina kaka na akina dada, kila mmoja wetu ana hadithi. Tunapogundua hadithi yetu, tunaunganika, tunakuwa sehemu ya, tunakuwa. …
Je, unaifahamu hadithi yako? …
… Unganisha kumbukumbu yako hai ya majina ya familia na majina bilioni 10 yanayoweza kutafutwa ambayo FamilySearch inayo sasa katika kusanyiko lake la mtandaoni pamoja na watu bilioni 1.3 katika Mti wake wa Familia. …
… Tunawaheshimu mababu zetu kwa kufungua mbingu kupitia kazi ya hekaluni na historia ya familia na kwa kuwa kiungio katika mnyororo wa vizazi vyetu. …
Kuunganika na mababu zetu kunaweza kubadilisha maisha yetu katika njia ya kushangaza. Kutokana na majaribu na mafanikio yao, tunapata imani na nguvu. Kutokana na upendo na dhabihu yao, tunajifunza kusamehe na kusonga mbele. …
… Huduma isiyo na ubinafsi ya hekaluni kwa ajili ya wapendwa wetu hufanya upatanisho wa Mwokozi wetu kuwa halisi kwa ajili yao na sisi. Tukiwa tumetakaswa, tunaweza kurudi nyumbani kwenye uwepo wa Mungu kama familia zilizounganishwa milele. …
Je, Tunaweza kufanya nini sasa? …
… Kukusanya picha zao na hadithi zao; kutengeneza kumbukumbu halisi. Kuandika majina yao, uzoefu wao, tarehe muhimu. Wao ni familia yako—familia uliyonayo na familia unayoitaka. …
Pili, acha tukio la historia ya familia liwe lenye lengo na la hiari. …
Tatu, tembelea FamilySearch.org. Pakua aplikesheni za simu. …
Nne, saidia kuunganisha familia milele. …
Kila mmoja wetu ana hadithi. Njoo ugundue ya kwako. Njoo upate sauti yako, wimbo wako, uwiano wako Kwake.