“Maagano na Mungu Yanatuimarisha, Yanatulinda, na Kutuandaa kwa Ajili ya Utukufu wa Milele,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Mei 2022.
Kikao cha Wanawake
Maagano na Mungu Yanatuimarisha, Yanatulinda, na Kutuandaa kwa Ajili ya Utukufu wa Milele
Dondoo
Je, umewahi kusimama kwenye kilele kirefu vidole vyako vya miguu vikiwa kwenye ukingo wake na mgongo ukielekea shimo kubwa? Katika kushuka mlima kwa kamba, hata ingawa umefungwa vyema kwenye kamba imara na vifaa ambavyo vinaweza kukushusha hadi chini kwa usalama, kusimama ukingoni bado kunaleta hofu moyoni. Kupiga hatua kwa nyuma kutoka kileleni na kuelea hewani kwenye hewa nyepesi huhitaji imani katika nanga iliyokitwa kwenye kifaa kisichotetereka. Inahitaji imani katika mtu ambaye atatumia nguvu kwenye kamba wakati unaposhuka …
Chombo cha kiroho ambacho hutuzuia tusivunjike kwenye miamba ya dhiki ni ushuhuda wetu wa Yesu Kristo na maagano tunayofanya. Tunaweza kutegemea misaada hii ili kutuongoza na kutupeleka mahali penye usalama. Kama mwenzi wetu aliye tayari, Mwokozi hataturuhusu tuanguke mbali na ufiko Wake ….
Hakuna kilicho muhimu zaidi kwa maendeleo yetu ya milele kuliko kutunza maagano yetu na Mungu. …
Ninashuhudia kwamba tunapochagua kufanya maagano na Baba wa Mbinguni na kutafuta nguvu ya Mwokozi ili kuyatunza maagano hayo, tutabarikiwa kwa furaha zaidi katika maisha haya kuliko vile tunavyoweza kufikiri sasa na uzima wa milele ujao wenye utukufu.