Mkutano Mkuu
Maagano na Mungu Yanatuimarisha, Yanatulinda, na Kutuandaa kwa Ajili ya Utukufu wa Milele
Mkutano mkuu wa Aprili 2022


11:59

Maagano na Mungu Yanatuimarisha, Yanatulinda, na Kutuandaa kwa Ajili ya Utukufu wa Milele

Tunapochagua kufanya maagano na kuyashika, tutabarikiwa na furaha zaidi katika maisha haya na maisha matukufu ya milele yajayo.

Akina Dada, ni shangwe ilioje kukusanyika katika udada wa ulimwenguni kote! Kama wanawake ambao tunafanya na kuyashika maagano na Mungu, tunashiriki kamba za kiroho ambazo hutusaidia kukabiliana na changamoto za siku yetu na kutuandaa kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Yesu Kristo. Na kuyashika maagano hayo huturuhusu kuwa wanawake wenye ushawishi ambao wanaweza kuwavuta wengine kwa Mwokozi.

Wale ambao wamebatizwa walifanya agano katika siku ile kamwe isiyoweza kusahaulika kujichukulia juu yao jina la Yesu Kristo, na daima kumkumbuka Yeye, kutii amri Zake, na kumtumikia Yeye hadi mwisho. Tunapofanya mambo haya, Baba wa Mbinguni anaahidi kutusamehe dhambi zetu na kutupatia uenzi wa Roho Mtakatifu. Baraka hizi zinatuanzisha katika njia ambayo, kama tutasonga mbele na kuvumilia hadi mwisho, itaturuhusu kuishi pamoja Naye na Mwanawe, katika ufalme wa selestia. Kila mtu aliyebatizwa ana ahadi ya baraka hizi na fursa kama yeye atashika agano walilofanya siku hiyo maalumu.

Wale ambao wanafanya maagano zaidi katika hekalu wanapokea ahadi zenye nguvu zilizo na masharti ya uaminifu wa kibinafsi. Tunaahidi kwa dhati kutii amri za Mungu, kuishi injili ya Yesu Kristo, kuwa safi kimaadili, na kujitolea muda wetu na talanta zetu kwa Bwana. Kama malipo, Mungu anaahidi baraka katika maisha haya na fursa ya kurudi Kwake.1 Katika mchakato huo, tunapatiwa, au tunakuwa na endaumenti, ya nguvu za ufafanuzi kati ya ukweli na kosa, kati ya sahihi na kisicho sahihi, katikati ya sauti za mkanganyiko na hasi ambazo zinangonga. Ni zawadi yenye nguvu ilioje!

Katika maandalizi yangu ya safari ya kwanza kwenda hekaluni, mama yangu na akina dada wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama wenye uzoefu walinisaidia kuchagua vitu ambavyo ningehitaji, ikijumuisha nguo maridadi za sherehe. Lakini maandalizi muhimu kabisa yalikuja hata kabla sijajua nini cha kuvaa. Baada ya kunisaili ili kutathimini kama nilikuwa ninastahili, askofu wangu alinielezea maagano ambayo ningefanya. Maelezo yake makini yalinipa nafasi ya kufikiria na kuwa tayari kufanya maagano hayo.

Wakati siku ilipofika, nilishiriki kwa hisia za shukrani na amani. Ingawa sikuelewa kikamilifu umuhimu wa maagano niliyofanya, nilijua kwamba nilifungwa kwa Mungu kupitia maagano hayo na niliahidiwa baraka ambazo nisingeelewa kabisa kama ningeyashika. Tangu uzoefu wa kwanza, nimeendelea kuhakikishiwa kwamba kushika maagano tunayofanya na Mungu huturuhusu kuvuta nguvu za Mwokozi, ambazo hutuimarisha katika majaribu yetu ambayo hayana budi kuja, hutupa ulinzi kutoka kwa ushawishi wa adui, na hutuandaa kwa ajili ya utukufu wa milele.

Uzoefu wa maisha unaweza kuwa kutoka ucheshi hadi uchungu mkali moyoni, kutoka kuogopa hadi utukufu. Kila uzoefu hutusaidia kuelewa zaidi kuhusu upendo wa kukumbatia wa Baba yetu na uwezo wetu wa kubadilika kupitia kipawa cha neema ya Mwokozi. Kushika maagano yetu huruhusu nguvu za Mwokozi kututakasa tunaojifunza kupitia uzoefu—iwe ni kutoamua vyema au makosa makubwa. Mkombozi wetu yuko pale kutushika tunapoanguka kama tutamgeukia Yeye.

Kushuka kwa kamba mwambani

Je, wewe umeshawahi kusimama kwenye mwamba mrefu kwa vidole vyako vya miguu kwenye ukingo wake na mgongo ukiwa upande wa lindi kuu? Katika kushuka mwambani, hata ingawa umefungwa vyema kwenye kamba imara na vifaa ambavyo vinaweza kukushusha hadi chini salama, kusimama ukingoni bado kundundisha moyo. Kupiga hatua ya nyuma kutoka mwambani na kuwa hewani kwenye hewa nyepesi huhitaji imani katika nanga iliyokitwa kwenye kifaa kisichoondosheka hapo juu. Inahitaji imani katika mtu ambaye anashika kamba unaposhuka. Na ingawaje chombo hukupa uwezo fulani wa kuthibiti kushuka kwako, ni lazima uwe na imani kwamba mwenzi wako hatakubali uanguke.

Nanga za kushuka mwambani
Msichana akishuka kwa kamba mwambani

Nakumbuka wazi kabisa nikishuka mwambani na kundi la wasichana. Nilikuwa wa kwanza kushuka. Nilipochukua hatua kutoka mwambani, nilianza kuanguka bila uthibiti. Shukrani, kamba ilijikaza na kushuka kwa upesi sana kulisimama. Nilipokuwa nimening’inia katikati kwenye uso wa mwamba, nilisali kwa bidii kwa ajili ya yeyote au chochote kilichokuwa kinanizuia nisianguke maweni.

Baadaye, nilijua kwamba boliti ya nanga haikuwa imeshikishwa vizuri, na nilipochukua hatua kutoka ukingoni, mtu aliyekuwa ananikazia kamba alikazwa na kuvutwa kuelekea ukingo wa mwamba. Kwa njia fulani, alikanyaga kwa miguu yake kwenye miamba. Akiwa imara katika mahali hapo, aliweza kunishusha chini kwa makini, mkono juu ya mkono, kwa kamba. Ingawaje singeweza kumuona, nilijua alikuwa anafanya kazi kwa nguvu zake zote kuniokoa. Rafiki mwingine alikuwa huko chini ya mwamba, amejiandaa kunishika kama kamba ingeacha kushikilia. Nilipofika karibu, alishika lijamu yangu na kunishusha chini.

Tukiwa na Yesu Kristo kama nanga yetu na mwezetu kamili, tunahakikishiwa nguvu Zake za upendo katika majaribu na hatimaye ukombozi kupitia Kwake. Kama Rais M. Russell Ballard alivyofundisha: “Imani katika Mungu na Mwanawe, Bwana Yesu Kristo, ni … nanga ambayo lazima tuwe nayo katika maisha yetu na kutushikilia vizuri wakati wa nyakati za misukosuko na uovu wa kijamii. … Imani yetu … lazima ilenge Yesu Kristo, maisha yake na upatanisho wake, na katika urejesho wa injili yake.”2

Chombo cha kiroho ambacho hutuzuia tusianguke kwenye miamba ya dhiki ni ushuhuda wetu wa Yesu Kristo na maagano tunayofanya. Tunaweza kutegemea hiyo misaada ya kutuongoza na kutubeba salama. Kama mwenzi wetu mwenye hiari, Mwokozi hataturuhusu kuanguka mbali na ufikio Wake. Hata katika nyakati za kuteseka na huzuni, Yeye yupo kutuinua na kututia moyo. Nguvu zake hutusaidia kupona kutoka kwa athari za kuangamiza za chaguzi za wengine. Hata hivyo, kila mmoja wetu lazima avalie lijamu na kuhakikisha kwamba mafundo yamefungwa vyema. Sisi lazima tuchague kutia nanga kwa Mwokozi, kufungwa Kwake kwa maagano yetu.3

Ni kwa jinsi gani tunaimarisha nanga hiyo? Tunaomba kwa moyo wa unyenyekevu, kujifunza na kutafakari maandiko, kupokea sakramenti kwa roho ya toba na staha, tunajitahidi kutii amri, kufuata ushauri wa nabii. Na tunapotimiza kazi zetu za kila siku katika njia za “juu na takatifu”4 tunaunganishwa zaidi kwa Mwokozi na, wakati huo huo, kuwasaidia wengine kuja Kwake.

Je, “njia hiyo ya juu na takatifu” inaonekana vipi? Tunajaribu kuishi injili katika miingiliano yetu. Tunawatunza wale walio na mahitaji kwa kuhudumia kikweli, kuonyesha upendo kupitia huduma rahisi. Tunashiriki habari njema za injili na wale ambao wanahitaji amani na nguvu na “hawajui mahali pa kuupata.”5 Tunafanya kazi kuunganisha familia kwa umilele pande zote mbili za pazia. Na kwa wale ambao wamefanya maagano katika nyumba ya Bwana, kama Rais Russell M. Nelson alivyoeleza, “Kile mtu mzima mteja wa hekalu atavaa vazi takatifu la ukuhani, [ambalo] … hutukumbusha … kutembea kwenye njia ya agano kila siku katika njia ya juu na takatifu.”6 Matendo haya si tu koga la mara kwa mara bali ni muhimu kwa furaha ya kila siku—na shangwe ya milele.

Hakuna kilicho muhimu zaidi kwa maendeleo yetu ya milele kuliko maagano yetu na Mungu. Wakati maagano yetu yanapokuwa hai, tunaweza kuamini katika muungano na wapendwa wetu upande mwingine wa pazia. Mtoto yule au mzazi au mwenzi ambaye ameaga dunia anategemea kwa moyo wake wote kwamba utakuwa mkweli kwa maagano ambayo yanakufunga pamoja. Kama tunapuuza au kuchukulia kwa wepesi maagano yetu na Mungu, tunaweka hiyo miunganiko ya milele hatarini. Sasa ni wakati wa kutubu, kurekebisha, na kujaribu tena.

Furaha ni tupu kama tunabadilisha baraka za furaha ya milele kwa raha ya muda kidogo. Bila kujali umri wetu, huo ni ukweli kabisa: ufunguo wa furaha ya kudumu ni kuishi injili ya Yesu Kristo na kuyashika maagano yetu. Nabii wetu, Rais Nelson, amethibitisha kwamba “usalama wetu wa msingi na furaha yetu endelevu tu ipo katika kushikilia fimbo ya chuma ya injili ya urejesho ya Yesu Kristo, kamili na maagano na ibada zake. Tunapofanya hivyo, tunaweza kuongoza kwa usalama kupita maji yaliyochafuka kwa sababu tunapata nguvu za Mungu.”7

Wengi wetu sisi tunapata uzoefu wa maji yaliyochafuka. Tunaporushwa huku na huko na mawimbi ya dhiki na wakati mwingine tunapofushwa na mafuriko ya machozi ambayo huja katika magumu haya, tunaweza kuwa hatujui mwelekeo wa kupiga makasia mashua yetu ya maisha. Tunaweza hata tusikifirie tuna nguvu za kufika ufukweni. Kumkumbuka wewe ni nani —mtoto mpendwa wa Mungu—kwa nini uko hapa duniani, na lengo lako la kuishi pamoja na Mungu na wapendwa wako linaweza kufungua ono lako na kukuelekeza mwelekeo sahihi. Katikati ya dhoruba, kuna nuru angavu ya kutuonyesha njia? “Mimi ni nuru ingʼaayo gizani,” Yesu alitangaza.8 Tunahakikishiwa usalama wakati tunategemea nuru Yake na kudumisha msimamo wa maagano yetu.

Imekuwa fursa kukutana na wanawake wa umri wote wanaoishi katika mazingira mengi tofauti ambao wanashika maagano yao. Kila siku, wanamtegemea Bwana na nabii Wake kwa mwongozo, badala ya vyombo vya habari maarufu. Licha ya changamoto zao binafsi na falsafa zenye madhara za ulimwengu ambazo ujaribu kuwashawishi wasishike maagano yao, wameazimia kubaki kwenye njia ya maagano. Wanategemea ahadi ya “vyote ambavyo Baba anavyo.”9 Na umri wako wowote ule, kila mmoja wenu wanawake ambao mmefanya maagano na Mungu ana uwezo wa kushikilia nuru ya Bwana na kuwaongoza wengine Kwake.10 Kupitia maagano yako, Yeye atakubariki na nguvu za ukuhani Wake na kukuwezesha kuwa na ushawishi wa kina juu ya wale unaoingiliana nao. Kama vile Rais Nelson alivyotangaza, ninyi ni wanawake ambao mnatimiza unabii ambao ulitabiriwa!11

Akina dada wapendwa, juu ya yote, bakini kwenye njia ya agano kwenda kwa Yesu Kristo? Tumebarikiwa kuja duniani wakati mahekalu yamesambaa ulimwenguni. Kufanya na kushika maagano ya hekaluni yanayopatikana kwa kila muumini mstahili wa Kanisa. Vijana wazima, hamhitaji kuongoja mpaka ndoa au misheni kufanya hayo maagano matakatifu. Unaweza kujiandaa kama msichana kupokea ulinzi na nguvu maagano ya hekalu vipatikanavyo punde baada ya miaka 18 mnapokuwa tayari na kuhisi hamu ya kuheshimu maagano hayo ya hekalu.12 Ninyi ambao tayari mmepokea baraka za hekalu, msiache wakashifishaji au vivuruga mawazo kukuvuta mbali na kweli za milele. Jifunze na uulize vyanzo vya kuaminika kwa ajili ya uelewa mwingi wa umuhimu wa maagano mliyofanya. Nenda hekaluni kila mara kama unavyoweza na msikilize Roho. Utahisi hakikisho tamu kwamba wewe uko katika njia ya Bwana. Utapata ujasiri wa kuendelea vile vile kuwaleta wengine pamoja nawe.

Nashuhudia kwamba tunapochagua kufanya maagano na Baba wa Mbinguni na kupata nguvu za Mwokozi na kuzibakisha, tutabarikiwa na furaha zaidi katika maisha haya kuliko vile tunavyoweza kufikiria na maisha matukufu ya milele yajayo.13 Katika jina la Yesu Kristo, amina.