Mkutano Mkuu
Imara katika Dhoruba
Mkutano mkuu wa Aprili 2022


15:44

Imara katika Dhoruba

Wakati dhoruba katika maisha zinapokuja, unaweza kuwa imara kwa sababu unasimama kwenye mwamba wa imani yako katika Yesu Kristo.

Akina kaka na akina na dada, tumebarikiwa leo kusikia watumishi wa Mungu wenye mwongozo wakitushauri na kutuhimiza. Kila mmoja wetu, popote tulipo, anajua kwamba tunaishi katika nyakati hatari. Maombi yangu ni kwamba ningeweza kuwasaidia kusimama imara katika dhoruba tunazokabiliana nazo, kwa moyo wa amani.1

Mahali pa kuanzia ni kukumbuka kwamba sisi kila mmoja wetu ni mtoto mpendwa wa Mungu na kwamba Yeye ana watumishi wenye mwongozo. Watumishi hao wa Mungu wameona mapema nyakati tunazoishi. Mtume Paulo alimwandikia Timotheo, “Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.”2

Mtu yeyote aliye na macho ya kuona ishara za nyakati na masikio ya kusikia maneno ya manabii anajua kwamba hiyo ni kweli. Nyakati za hatari kubwa zinakuja kwetu kutoka kwa nguvu za uovu. Nguvu hizi zinaongezeka. Na kwa hivyo itakuwa vigumu sana, sio rahisi, kuheshimu maagano ambayo sharti tufanye na kuyashika ili kuishi injili ya Yesu Kristo.

Kwa wale kati yetu ambao wanatujali sisi pamoja na wale tunaowapenda, kuna tumaini katika ahadi ya Mungu alifanya ya mahali pa usalama katika dhoruba zijazo.

Hapa kuna picha ya neno la mahali hapo. Imeelezwa kwa marudio na manabii walio hai. Kwa mfano, kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Mormoni, baba mwenye mwongozo na mwenye upendo aliwaambia wanawe jinsi ya kujiimarisha wenyewe ili kusimama imara katika dhoruba zilizo mbele yao: “Na sasa, wana wangu, kumbukeni, kumbukeni kwamba ni juu ya mwamba wa Mkombozi wetu, ambaye ni Kristo, Mwana wa Mungu, kwamba lazima mjenge msingi wenu; kwamba ibilisi atakapotuma mbele pepo zake kali, ndio, mishale yake kimbungani, wakati mvua yake ya mawe na dhoruba kali itapiga juu yenu, hautakuwa na uwezo juu yenu kuwavuta chini kwenye shimo la taabu na msiba usioisha, kwa sababu ya mwamba ambako kwake mmejengwa, ambao ni msingi imara, … ambako watu wote wakijenga hawataanguka,”3

Taabu na majonzi yasiyo na mwisho ambayo aliongea juu yake ni madhara mbaya ya dhambi tunapokosa kuzitubu kikamilifu. Dhoruba zinazoongezeka ni majaribu na ongezeko la mashambulizi ya Shetani. Kamwe haijawahi kuwa muhimu sana kama ilivyo sasa kuelewa jinsi ya kujenga juu ya msingi imara. Kwangu mimi, hakuna mahali bora pa kutazama kuliko mahubiri ya mwisho ya Mfalme Benyamini, yaliyoandikwa pia katika Kitabu cha Mormoni.

Maneno ya kinabii ya Mfalme Benyamini yanatumika kwetu katika siku yetu. Alijua kutokana na uzoefu wake mwenyewe hatari za vita. Aliwalinda watu katika mapambano, akitegemea nguvu za Mungu. Aliona kwa uwazi nguvu mbaya za Lusiferi za kutia majaribuni, kujaribu kushinda, na kuwavunja moyo watoto wa Mungu.

Aliwaalika watu wake na sisi kujenga tu juu ya mwamba imara wa usalama, ambao ni Mwokozi. Alisema wazi kwamba sisi tuna uhuru wa kuchagua kati ya kilicho sahihi na kosa na kwamba hatuwezi kuepuka matokeo ya chaguzi zetu Aliongea moja kwa moja na dhahiri kwa sababu alijua ni huzuni gani ingewapata wale ambao hawangesikia na kufuata maonyo yake.

Hivi ndivyo alivyoelezea matokeo ambayo yangefuata chaguzi zetu iwe ni kufuata msukumo wa Roho au kufuata jumbe ovu ambazo zinakuja kutoka kwa Shetani, ambaye anadhamiria kututia majaribuni na kutuangamiza.

“Kwani tazama, ole kwa yule anayechagua kumtii huyo pepo [ovu]; kwani akichagua kumtii, na kuishi na afariki katika dhambi zake, yeye anakunywa adhabu kwa nafsi yake; kwani yeye hupokea kwa mshahara wake adhabu isiyo na mwisho, kwa sababu ya kuvunja sheria ya Mungu kinyume cha ufahamu wake.

“Kwa hivyo kama mtu huyu hatatubu, na aishi na afe akiwa adui wa Mungu, matakwa ya haki takatifu huzindua nafsi yake isiyokufa kwa hatia yake mwenyewe, ambayo humsababisha kutetemeka mbele ya Bwana, na hujaza kifua chake na hatia, na uchungu, na huzuni, ambayo ni kama moto usiozimika, ambao miale yake hupaa juu milele na milele.

Mfalme Benyamini aliendelea kusema, “Ee ninyi, watu wote wazee, na pia ninyi vijana, na ninyi watoto wachanga mnaoweza kuelewa maneno yangu, kwani nimezungumza wazi kwenu ili muweze kuelewa, naomba kwamba muamke kwa ukumbusho wa mahali pa kuogofya pa wale walioanguka kwenye dhambi.”4

Kwangu mimi, nguvu za onyo hilo la kutubu hufanya katika akili yangu picha ya wakati halisi ambapo wewe na mimi tutasimama mbele ya Mwokozi baada ya maisha haya. Sisi tunataka kwa mioyo yetu yote tusitetemeke bali tumtengemee Yeye, kuomwona Yeye, na kumsikia Yeye akisema “Vema, mtumwa mwema na mwaminifu: … ingia [ndani].”5

Mfalme Benyamini anasema wazi jinsi tunaweza kupokea tumaini la kusikia maneno hayo kama tutapata njia katika maisha haya ya kuwa na asili yetu kubadilishwa kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo. Hiyo ndiyo njia ya pekee tunayoweza kujenga juu ya msingi imara na kusimama kwa uthabiti wakati wa dhoruba za majaribu na majaribio yajayo. Mfalme Benyamini anaeleza kwamba mabadiliko katika asili yetu kwa isitiari ambayo daima iligusa moyo wangu. Ilitumiwa na manabii kwa ajili ya milenia na Bwana Mwenyewe. Katika hii: tunapaswa kuwa kama mtoto—mtoto mdogo.

Kwa wengine, hiyo haitakuwa rahisi kukubali. Wengi wetu tunataka kuwa na nguvu. Tunaweza pia kuona kuwa kama mtoto kama kuwa mdhaifu. Wazazi wengi wanatazamia siku ile ambapo watoto wao hawatenda kwa utoto. Lakini Mfalme Benyamini, ambaye alielewa vile vile kama mtu yeyote kile ilimaanisha kuwa mtu mwenye nguvu na jasiri, na anasema wazi kwamba kuwa kama mtoto si utoto. Ni kuwa kama Mwokozi, ambaye alimuomba Baba Yake nguvu za kuweza kutenda mapenzi ya Baba Yake na kulipia dhambi za watoto wote wa Baba Yake na kisha akafanya hivyo. Asili yetu lazima ibadilike na kuwa kama mtoto na kupata nguvu lazima tuwe nazo ili kusimama imara na kuwa na amani nyakati za hatari.

Hapa kuna maelezo ya Mfalme Benyamini ya kuchochea ya jinsi mabadiliko uja: “Kwani mwanadamu wa asili ni adui kwa Mungu, na amekuwa tangu anguko la Adamu, na atakuwa hivyo, milele na milele, asipokubali ushawishi wa Roho Mtakatifu, na kumvua mtu wa asili na kuwa mtakatifu kupitia upatanisho wa Kristo aliye Bwana, na kuwa kama mtoto, mtiifu, mpole, mnyenyekevu, mvumilivu, mwenye upendo tele, aliye tayari kukubali vitu vyote ambavyo Bwana anaona sahihi kuyaweka juu yake, hata kama vile mtoto hunyenyekea kwa baba yake.”6

Tunapokea mabadiliko hayo tunapofanya na kufanya upya maagano na Mungu. Hiyo huleta nguvu za Upatanisho wa Kristo kuruhusu mabadiliko katika mioyo yetu. Tunaweza kuyahisi kila wakati tunapopokea sakramenti, kufanya ibada za hekaluni kwa ajili ya babu aliyeondoka, tunaposhuhudia ushahidi wa Mwokozi, na tunapomtunza mtu mwenye mahitaji kama mwanafunzi wa Kristo.

Katika uzoefu huo, tunakuwa baada ya muda kama mtoto katika uwezo wetu wa kupenda na kutii. Tunasimama kwenye msingi imara. Imani katika Yesu Kristo hutuleta kwenye toba na kutii amri Zake. Tunatii, na kupata nguvu za kushinda majaribu, na kupata ahadi ya wenza wa Roho Mtakatifu.

Asili yetu ubadilika kuwa kama mtoto mdogo, mtiifu kwa Mungu na wenye kupenda zaidi. Mabadiliko hayo yanatuhitimisha sisi kufurahia vipawa ambavyo huja kupitia Roho Mtakatifu. Kuwa na uwenzi wa Roho kutatufariji, kutatoongoza na kutuimarisha.

Nimekuja kujua baadhi ya kile Mfalme Benyamini alimaanisha aliposema kwamba tungeweza kuwa kama watoto wadogo mbele za Mungu. Nimejifunza kutokana na uzoefu mwingi kwamba Roho Mtakatifu uongea mara nyingi katika sauti tulivu, usikika kwa urahisi sana wakati moyo wa mtu ni mnyenyekevu na ni msikivu, kama ule wa mtoto. Kwa kweli, maombi ambayo hufanya kazi ni “Mimi nataka tu kile Wewe unataka. Niambie tu hicho ni nini. Nitakifanya.”

Wakati dhoruba katika maisha zinapokuja, unaweza kuwa imara kwa sababu unasimama kwenye mwamba wa imani yako katika Yesu Kristo. Imani hiyo itakuongoza wewe katika toba ya kila siku na kwa uthabiti kushika maagano. Kisha wewe daima utamkumbuka Yeye. Na kupitia dhoruba za chuki na uovu, wewe utahisi kuwa imara na kuwa na matumaini.

Zaidi ya hayo, utajipata mwenyewe ukitafuta kuwainua wengine hadi kwenye usalama juu ya mwamba pamoja nawe. Imani katika Yesu Kristo daima itakuaongoza kwenye tumaini kuu na kwenye hisia za hisani kwa wengine, ambayo ni upendo halisi wa Kristo.

Natoa ushahidi wangu wa dhati kwamba Bwana Yesu Kristo ametoa mwaliko “Njooni kwangu.”5 Yeye anawaalika, kutokana na upendo kwa ajili yenu na kwa wale mnaowapenda, kuja Kwake kwa ajili ya amani katika maisha haya na uzima wa milele katika ulimwengu ujao. Yeye anajua vyema dhoruba mtakazokabiliana nazo katika majaribu yenu kama sehemu ya mpango wa furaha.

Ninawasihi mkubali mwaliko wa Mwokozi. Kama mtoto mnyenyekevu na mwenye upendo, mkubali msaada Wake. Mfanye na kuyashika maagano Yeye anayotoa katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Yatawaimarisha. Mwokozi anajua dhoruba na sehemu za usalama katika njia ya kwenda nyumbani Kwake na kwa Baba yetu wa Mbinguni. Yeye anaijua njia. Yeye ndiye Njia. Ninashuhudia hivyo, katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.