Mkutano Mkuu
Sisi ni wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho
Mkutano mkuu wa Aprili 2022


Sisi Ni wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu waSiku za Mwisho

Kanisa ni zaidi ya majengo na muundo wa kikanisa; Kanisa ni sisi, waumini, na Kristo akiwa juu na nabii kama kinywa Chake.

Baada ya kupokea mwaliko “njoo uone,”1 nilihudhuria Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kwa mara ya kwanza nikiwa na umri wa miaka 26. Wakati huo nilikuwa nimetengana na mme wangu wa kwanza. Nilikuwa na mvulana wa miaka mitatu. Na nilijihisi mdhaifu na woga. Nilipoingia kwenye jengo, nilijawa na ukarimu kwa kuona imani na shangwe ya watu walionizunguka. Ilikuwa hakika “ni kimbilio kwenye dhoruba.”2 Wiki tatu baadaye, nilifanya maangano ya ubatizo na Baba yangu wa Mbinguni na kuanza safari yangu kama mfuasi wa Kristo, ingawa maisha yangu hayajawahi kuwa makamilifu katika safari hiyo.

Kwa mimi kupokea baraka za milele, mambo mengi ya kiroho na kimwili yalipaswa kuwepo. Injili ya Yesu Kristo ilikuwa imerejeshwa na kuhubiriwa; nyumba hiyo ya kukutania ilikuwa imejengwa na kutunzwa; palikuwepo na muundo wa kikanisa, kutoka kwa nabii mpaka viongozi wa kawaida; na tawi lililojawa na maagano lilikuwa tayari kunikumbatia mimi na kijana wangu tuliposonga kwa Mwokozi,“tukilishwa na neno zuri la Mungu,”3 na kupewa fursa ya kutumikia.4

Kutoka mwanzo, Mungu ametafuta kuwakusanya na kuwaweka pamoja watoto Wake5 “ili kuleta kutokufa [kwetu] na uzima wa milele.”6 Akiwa na lengo hilo akilini mwake, Ametuamuru sisi kujenga maeneo ya kuabudia7 ambapo tunapokea maarifa na ibada za wokovu na utukufu; kufanya na kutunza maaganao yanayotuunganisha na Yesu Kristo;8 tumapokea endomenti kwa “nguvu za uungu”;9 na kukusanyika kila mara kumkumbuka Yesu na kuimarishana sisi kwa sisi ndani Yake.10 Muundo wa Kanisa na majengo yake vipo kwa ajili ya faida yetu kiroho. “Kanisa … ni kiunzi ambacho kwacho tunajenga familia ya milele.”11

Wakati naongea na rafiki aliyekuwa anapitia kwenye changamoto, nilimuuliza ni kwa jinsi gani alihimili hali ya kiuchumi. Akitokwa na machozi, alijibu kwamba askofu alikuwa akimsaidia kwa kutumia pesa za matoleo ya mfungo. Aliongeza, “sijui familia yangu na mimi tungekuwa wapi kama sio Kanisa.” Nilimwitikia, “Kanisa ni waumini. Hao ndio kwa utashi wao na kwa furaha hutoa matoleo ya mfungo kutusaidia sisi wenye uhitaji. Unapokea matunda ya imani yao na maamuzi ya kumfuata Yesu Kristo.”

Wafuasi wenzangu wa Kristo, hebu na tusidharau kazi ya kushangaza Bwana anayoifanya kupitia sisi, Kanisa Lake, licha ya mapungufu yetu. Wakati mwingine tu watoaji na wakati mwingine tu wapokeaji, ila wote tu familia moja ya Kristo. Kanisa lake ni muundo ambao Yeye ameutoa kutuongoza na kutubariki tunapoendelea kumwabudu Yeye na kuhudumiana sisi kwa sisi.

Badhi ya kina dada wameomba msamaha kwangu, wakifikiri kwamba si waumini hai wa Muungano wa Usaidizi kwa sababu wanatumikia katika Msingi au kwa Wasichana. Akina dada hao ni kati ya wale ambao ni washiriki hai wa Muungano wa Usaidizi kwa sababu wanawasaidia watoto wetu wazuri na vijana kuimarisha imani yao.

Muungano wa Usaidizi wa hauishii kwenye chumba ndani ya jengo, somo la Jumapili, shughuli au uraisi katika ngazi ya eneo husika au ya juu. Muungano wa Usaidizi ni mwanamke wa agano wa Kanisa; ni sisikila mmoja wetu na sisi sote. Ni “jamii yetu ya ulimwengu mzima ya huruma na huduma.”12 Popote na kila mahali tuendapo, daima tu sehemu ya Muungano wa kadiri tunavyojitahidi kutimiza lengo lake takatifu, ambalo ni kwa wanawake kukamilisha kazi ya Mungu katika kila mtu na kwa njia za pamoja13 kwa kutoa unafuu, “unafuu wa umasikini, unafuu wa magonjwa; unafuu wa mashaka, unafuu wa ujinga—unafuu wa vizuizi vyote … furaha na kuendelea.”14

Mambo kama haya hupatikana katika akidi ya wazee na jumuya za Kanisa kwa kila umri, ikijumuisha watoto wetu na vijana. Kanisa ni zaidi ya majengo na muundo wa kikanisa; kanisa ni sisi, waumini. Sisi ni Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, na Kristo akiwa kiongozi mkuu na nabii kama msemaji Wake. Bwana amesema:

“Tazama, hili ni fundisho langu—yeyote atubuye na kuja kwangu, huyo ndiye kanisa langu. …

“Na … yeyote aliye wa kanisa langu, na alivumiliaye kanisa langu hadi mwisho, huyo nitamweka juu ya mwamba wangu.”15

Akina dada na kaka, hebu tutambue kuwa tu wenye bahati kuwa katika Kanisa la Yesu Kristo, tunapoweza kuunganisha imani yetu, mioyo, nguvu, mawazo na mikono kufanya miujiza Yake mikuu. “Kwa mwili [wa Kanisa la Yesu] si mwanachama mmoja, bali wengi.”16

Kijana mdogo alimwambia mama yake, “Nilipokuwa mdogo, kila mara nilitoa dola moja katika matoleo ya mfungo, nilifikiri kwamba kwa hiyo dola moja nyumba yote ya mkutano ingeweza kujengwa. Je huo si ujinga?

Akiwa ameguswa, alijibu, “Hiyo inapendeza! Uliweza kuziona pesa hizo akilini mwako?”

“Ndio!,” alisema. “Zilikuwa nzuri na zilikuwa mamilioni!”17

Rafiki zangu wapendwa, hebu tuwe na imani kama ya mtoto na kufurahi kwa kujua kwamba hata juhudi zetu ndogo hufanya jambo muhimu katika ufalme wa Mungu.

Lengo letu katika Ufalme Wake linapaswa kuwa kumleta kila mmoja wetu kwa Kristo. Kama tusomavyo kwenye maandiko, Mwokozi anatoa mwaliko kwa Wanefi:

“Mnao wowote ambao ni wagonjwa miongoni mwenu? Waleteni hapa. Mnao wowote ambao wame … sumbuka katika namna yoyote ile? Waleteni hapa na nitawaponya, kwani ninayo huruma juu yenu; matumbo yangu yamejaa na huruma.

“… Naona kwamba imani yenu yatosha kwamba niweze kuwaponya.”18

Je, sote hatuna mahangaiko yanayoweza kupelekwa miguuni mwa Mwokozi? Wakati baadhi yetu tunazo changamoto za kimwili, wengi zaidi hupambana na hali za kihisia, wengine hupambana kujenga mahusiano ya kijamii na sote tunatafuta pumziko wakati roho zetu hupitia changamoto. Sisi sote tunapitia masumbuko kwa namna moja.

Tunasoma kwamba “umati wote, kwa lengo moja, ulisonga mbele na wagonjwa wao na … pamoja na wote waliosumbuka kwa namna yoyote; na aliwaponya wote kila mmoja kadiri walivyoletwa kwake.

“Na wote, ambao walikuwa wameponywa, na wale ambao walikuwa wazima, waliinama chini miguuni mwake, na kumwabudu.”19

Kutoka kwa mvulana mdogo anayelipa zaka kwa imani, hadi kwa mama mhitaji wa uweza wa neema ya Bwana, hadi kwa baba anayepambana kutunza familia yake, hadi kwa mababu zetu wanaohitaji ibada za ukombozi na kuinuliwa, hadi kwa kila mmoja wetu tunaofanya upya maagano yetu na Mungu kila juma, tunahitajiana, na tunaweza kuletana sote kwenye ukombozi wa uponyaji wa Mwokozi.

Dada na kaka zangu wapendwa, acha tufuate wito wa Yesu Kristo wa kujipeleka sisi na masumbuko yetu Kwake. Tunapoenda Kwake na kuleta wapendwa wetu Kwake, Anaona imani yetu. Atawafanya kuwa wazima na Atatufanya sisi kuwa wazima.

Kama “wafuasi wa imani ya Kristo,”20 tunajitahidi kuwa wa “moyo mmoja na wazo moja”21 na kuwa wanyenyekevu; wapole; waungwana; wepesi kusihiwa; wenye utele wa subira na uvumilivu; wenye kiasi katika vitu vyote, wenye bidii katika kutii amri za Mungu wakati wote; mna imani, tumaini, na hisani, na kisha mtadumu katika kazi nzuri.22 Tunajitahidi kuwa kama Yesu Kristo.

Nashuhudia kwamba kama Kanisa la Kristo, sisi ni njia ambayo kupitia kwayo, kama Rais Russell M. Nelson alivyofundisha, “Mwokozi na Mkobozi wetu,Yesu Kristo, atafanya baadhi ya kazi Zake kuu kati ya sasa na Atakapo rudi tena.”23

Bwana amesema:

Tazama, nitaiharakisha kazi yangu katika wakati wake.

“Na ninatoa kwenu … amri kuwa jikusanyeni pamoja, na jipangeni, na jiandaeni, na jitakaseni; ndiyo, itakaseni mioyo yenu, na iosheni mikono na miguu yenu mbele zangu, ili niweze kuwafanya kuwa safi.”24

Na tuitikie mwaliko huu mtakatifu na kwa furaha tukusanyike, tujipange, na kujitakasa wenyewe ni sala yangu kwa unyenyekevu katika jina la Yesu Kristo, amina

Chapisha