Mkutano Mkuu
Je Mpango Unafanya Kazi?
Mkutano mkuu wa Aprili 2022


Je Mpango Unafanya Kazi?

Ninashuhudia kwamba mpango wa furaha unafanya kazi. Ulitengenezwa na Baba yako wa Mbinguni, anayekupenda.

Je, Mpango Unafanya Kazi?

Hivi karibuni nilikuwa na mazungumzo na kijana aliyehudumu misheni miaka kadhaa iliyopita na sasa alikuwa akijihusisha na kazi yake aliyobobea. Kwa mitazamo kadhaa, maisha yake yalikwenda vyema. Lakini imani yake ilikuwa inafifia. Alikuwa anazama kwenye bahari ya mashaka kuhusu Mwokozi na Kanisa Lake. Alielezea kwamba hakuwa anapokea baraka tarajiwa kutoka injili ya urejesho. Hakuhisi kwamba mpango wa furaha ulikuwa unafanya kazi katika maisha yake.

Ujumbe wangu leo ni kwa wale wote ambao wanaweza kuwa na hisia kama hizo. Ninazungumza na wale ambao kwa wakati fulani “walihisi kuimba wimbo wa upendo wa ukombozi” lakini “hawahisi hivyo sasa.”1

Baba yetu wa Mbinguni ameandaa kwa ajili yetu mpango mzuri kwa ajili ya furaha yetu ya milele. Lakini pale maisha yanapokuwa hayatoi kwa njia tuliyotarajia, inaweza kuonekana kwamba mpango haufanyi kazi.

Huenda tunahisi jinsi ambavyo wafuasi wa Yesu walihisi wakati walipokuwa kwenye merikebu, “katikati ya bahari, ikitaabika sana na mawimbi; maana upepo ulikuwa wa mbisho.”2

Kisha, asubuhi mapema sana:

“Yesu aliwaendea, akitembea juu ya maji;

“Wanafunzi walipomwona akitembea juu ya bahari, wakafadhaika, … wakapiga yowe kwa hofu.

“Mara Yesu alinena, akawaambia, Jipeni moyo ni mimi; msiogope.

“Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji.

“Akasema, Njoo. Na wakati Petro aliposhuka kutoka kwenye merikebu, alitembea juu ya maji, kwenda kwa Yesu.

“Lakini alipoona upepo mkali, aliogopa; na kuanza kuzama, alipiga yowe, … Bwana, niokoe.

“Na mara moja Yesu akanyoosha mkono wake, na akamshika,na akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka?”3

Je, ninaweza kushiriki nanyi kanuni tatu nilizojifunza kutoka kwa Petro? Ninaomba kwamba kanuni hizi ziweze kumsaidia yeyote anayehisi kwamba mpango wa furaha haufanyi kazi katika maisha yao.

Kwanza, tenda kwa imani katika Yesu Kristo.

Binafsi ninashangazwa na imani ya Petro. Kwa mwaliko rahisi wa Yesu wa “njoo,” aliacha merikebu yake iliyokuwa inayumbishwa na dhoruba. Alionekana kujua kwamba kama Yesu Kristo angemwalika kufanya kitu fulani, angeweza kukifanya.4 Petro alimwamini Mwokozi zaidi kuliko alivyoamini merikebu yake. Na imani hiyo ilimpa nguvu ya kutenda kwa ujasiri wakati wa matatizo, unaotisha.

Imani ya Petro inanikumbusha uzoefu ambao niliusikia kutoka kwa Mzee José L. Alonso. Punde baada ya Kijana wa Alonso kufariki, akiacha familia yenye watoto wadogo, Mzee Alonso alisikia watoto wakizungumza.

“Tutafanya nini?” waliuliza.

Binti wa miaka tisa alijibu, “Baba yuko SAWA. Anahubiri injili ya Yesu Kristo.”

Kama Petro, msichana huyu mdogo aliona zaidi ya changamoto zake na aliamini katika Yesu Kristo na upatanisho Wake. Imani katika Mwokozi inaleta amani na nguvu ya kusonga mbele.

Kama ukirejelea uzoefu wako uliopita, Ninaamini utaona kwamba umetumia imani mara nyingi. Kujiunga na Kanisa ni tendo la imani. Kuzungumza na Baba wa Mbinguni katika sala ni tendo la imani. Kusoma maandiko ni tendo la imani. Kusikiliza ujumbe wangu katika mkutano huu mkuu ni tendo la imani. Kama Rais Russell M. Nelson alivyosema, “usipunguze kabisa imani uliyonayo tayari.”5

Somo lingine nililojifunza kutoka kwa Petro ni hili:

Katika nyakati za matatizo, mgeukie Yesu Kristo mara moja.

Alipokuwa akitembea kuelekea kwa Mwokozi, Petro alitishwa na upepo na alianza kuzama. Lakini Petro alipotambua nini kilikuwa kinatokea, hakujaribu kukanyaga maji yeye mwenyewe au kuogelea kurudi kwenye merikebu. Kuliko kuacha imani yake katika Kristo, alishikilia kwa nguvu zaidi, akipiga yowe, “Bwana niokoe.”

“Na mara moja Yesu akanyoosha mkono Wake, na akamshika.”6

Sisi wote tunakabiliana na pepo zenye nguvu ambazo zinaweza kutikisa imani yetu na kutusababishia kuzama. Hii inapotokea, tafadhali kumbuka kwamba mpango wa furaha wa Baba wa Mbinguni una jina lingine—mpango wa ukombozi. Mpango haukuwa wa sisi kuvuka kirahisi maisha haya, kutojikwaa kamwe, kamwe kutozama, kuwa na tabasamu siku zote usoni mwetu. Baba wa Mbinguni alijua kwamba tutahitaji kukombolewa. Hii ndio sababu Alitayarisha mpango wa ukombozi.7 Hii ndio sababu Alimtuma Mkombozi. Tunapopambana—kwa sababu yoyote ile—hiyo haimanishi mpango haufanyi kazi. Huo ndio wakati wa kuhitaji mpango sana!

Katika nyakati hizo, fuata mfano wa Petro. Mgeukie Mwokozi mara moja.

“Sasa ndiyo wakati na siku ya wokovu wenu. … Usihairishe siku yako ya toba.”8

Haijalishi tuko wapi na wapi tumiewahi kuwa, toba ni njia ya kusonga mbele. Rais Nelson amefundisha:

“Hakuna kinachotoa uhuru zaidi, cha kiungwana zaidi au cha muhimu zaidi kwa ukuaji wetu binafsi kuliko ilivyo fokasi ya mazoea ya kila siku kwenye toba. …

“Bila kujali unaendelea kusonga kwa bidii kwenye njia ya agano, umeteleza au kutoka kwenye njia ya agano, au huwezi hata kuona njia ya agano kutokea ulipo sasa, ninakusihi utubu. Kuwa na uzoefu wa nguvu ya uimarisho ya toba ya kila siku—ya kufanya vizuri zaidi na kuwa wazuri zaidi kila siku.”9

Kumgeukia Kristo kuna thamani zaidi kuliko kufikiri tu kumhusu Yeye au kuzungumza kuhusu Yeye au hata kumpenda yeye. Inamaanisha kumfuata Yeye. Inamaanisha kuishi njia Anayofundisha sisi kuiishi. Na kwa sisi sote, hiyo inamaanisha kutubu, bila kuchelewa.

Mmoja wa mabinti zangu alikuwa anafanya kazi kwenye kituo cha kufundishia wamisionari. Alinieleza juu ya mzee aliyemfundisha ambaye alimwelezea binti yangu kwamba hakuwa na uhakika kama Kitabu cha Mormoni kilikuwa cha kweli. Alikuwa amesali na kusali kwa ajili ya ushahidi wa kiroho, lakini hakupata jibu.

Binti yangu alisali kujua nini angelifanya kumsaidia mmisionari huyu. Msukumo alioupata ulikuwa kwamba maandiko hayakutolewa tu ili tuweze kuyasoma na kupata ushuhuda; yalitolewa pia kutufundisha kutii amri za Mungu. Binti yangu alishiriki wazo hili pamoja na mmisionari.

Baadaye, alimwona mmisionari huyu tena, akionekana mwenye furaha tele. Alimwambia kwamba hatimaye amepokea ushuhuda kwamba Kitabu cha Mormoni ni cha kweli. Alijua kwamba ushahidi huu ulikuja kwa sababu alikuwa anaweka juhudi kubwa kufanya kile Kitabu cha Mormoni kinafundisha.

Acha tufuate mfano wa Petro wa kumgeuka Mwokozi katika nyakati za matatizo. Mfuate Yesu Kristo badala ya kutegemea busara yako mwenyewe na nguvu. Bila kujali ni kwa muda gani umekuwa unajaribu kutembea juu ya maji bila Yeye, kamwe hujachelewa kumfikia Yeye. Mpango unafanya kazi!

Kanuni ya tatu niliyojifunza kutoka kwa Petro na uzoefu wake ni hii:

Jinyenyekeze mwenyewe mbele ya Bwana na Atakuinua juu kwenye vitu vikubwa.

Petro alionesha imani, katika kutembea juu ya maji na katika kumfikia Mwokozi wakati alipohitaji msaada. Hata hivyo, Mwokozi aliona ndani ya Petro uwezekano kwa ajili ya mengi zaidi. “Ewe mwenye imani haba” Alisema, “mbona uliona shaka?”10

Petro angeweza kuchukia karipio hili. Lakini alilikubali kwa unyenyekevu. Aliendelea kutafuta imani kubwa zaidi katika Yesu Kristo. Kupitia uzoefu mwingi wa ziada wa kujenga imani—baadhi ukiwa mgumu sana—Petro hatimaye akawa kiongozi imara ambaye Bwana alimtaka awe. Alikamilisha mambo makubwa katika huduma ya Bwana.

Ni mambo gani makubwa Bwana anakutaka uyakamilishe? Katika Kanisa Lake na ufalme, kuna fursa nyingi za kuhudumia na kuwatumikia wengine kama Mwokozi alivyofanya. Anakutaka wewe kuwa sehemu ya kazi Yake kuu. Kamwe mpango wa furaha hautakuwa halisi zaidi kwako kushinda wakati unapowasaidia wengine kuuishi.

Katika kujenga imani yangu mwenyewe, maneno haya ya Alma yalikuwa ya mabadiliko ya maisha: “Wamebarikiwa wale wanaojinyenyekeza wenyewe bila kulazimishwa kuwa wanyenyekevu.”11 Acha kwa unyenyekevu tujiweke wenyewe katika nafasi ambapo Yesu Kristo anaweza kutuinua, kutuongoza na kufanya mengi ya uwezo wetu.12

Ninashuhudia kwamba mpango wa furaha unafanya kazi. Ulitengenezwa na Baba yako wa Mbinguni, anayekupenda. Unafanya kazi kwa sababu Yesu Kristo alishinda dhambi na kifo kupitia Upatanisho Wake. Songa kwake, ukimfuata Yeye, na “mara moja mpango mkubwa wa ukombozi utaletwa kwako.”13 Katika Jina la Yesu Kristo, amina.

Chapisha