2022
Sisi ni Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho
Mei 2022


Sisi Ni Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2022.

Kikao cha Jumamosi Asubuhi

Sisi Ni Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho

Dondoo

Picha
bango la kituo cha mkutano

Pakua PDF

Baada ya kupokea mwaliko “njoo na uone,” [Yohana 1:46], nilihudhuria Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kwa mara ya kwanza nikiwa na umri wa miaka 26. Wakati huo nilikuwa nimetengana na mume wangu wa kwanza. Nilikuwa na mvulana wa miaka mitatu. Na nilijihisi dhaifu na mwenye hofu. Nilipoingia kwenye jengo, nilijawa na hisia nzuri kwa kuona imani na shangwe ya watu walionizunguka. …

Wafuasi wenzangu wa Kristo, hebu tusidharau kazi ya kushangaza Bwana anayoifanya kupitia sisi, Kanisa Lake, licha ya mapungufu yetu. Wakati mwingine tu watoaji na wakati mwingine tu wapokeaji, lakini sote tu familia moja katika Kristo. …

… Kanisa ni zaidi ya majengo na muundo wa kikanisa; kanisa ni sisi, waumini. Sisi ni Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, tukiwa na Kristo kama kiongozi mkuu na nabii kama msemaji Wake. …

Lengo letu katika Ufalme Wake linapaswa kuwa kumleta kila mmoja wetu kwa Kristo. …

Kutoka kwa mvulana mdogo anayelipa zaka kwa imani, hadi kwa mama mhitaji wa uweza wa neema ya Bwana, hadi kwa baba anayepambana kuitunza familia yake, hadi kwa mababu zetu wanaohitaji ibada za wokovu na kuinuliwa, hadi kwa kila mmoja wetu tunaofanya upya maagano yetu na Mungu kila wiki, sote tunahitajiana, na tunaweza kuletana kila mmoja kwenye ukombozi wa uponyaji wa Mwokozi.

Chapisha