“Kumfuata Yesu: Kuwa Mpatanishi,” Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2022.
Kikao cha Jumamosi Asubuhi
Kumfuata Yesu: Kuwa Mpatanishi
Dondoo
Bwana alifundisha jinsi ya kuishi, wakati huo na sasa katika ulimwengu wenye mabishano. “Heri wapatanishi,” Yeye alitangaza, “maana hao wataitwa wana wa Mungu.” [Mathayo 5:9]. …
Je, ni jinsi gani mpatanishi hutuliza na kupoza mishale yenye moto? Hakika si kwa kusitasita mbele ya wale wanaotudharau. Badala yake, tunabaki majasiri katika imani yetu, tukishiriki imani yetu kwa ari, lakini siku zote bila hasira au chuki. …
Ni nini hutupatia nguvu ya ndani ya kupoza, kutuliza na kuzima mishale yenye moto inayolenga kweli tunazozipenda? Nguvu huja kutokana na imani yetu katika Yesu Kristo na imani yetu katika maneno Yake. …
Ingawa tamanio letu la dhati ni kwamba mafundisho ya Mwokozi yathaminiwe na wote, maneno ya Bwana kupitia manabii Wake mara nyingi ni kinyume na mawazo na mitindo ya ulimwengu. Imekuwa hivyo siku zote. …
Kwa heshima tunawapenda na kuwajali jirani zetu wote, bila kujali ikiwa wanaamini kama sisi au la. …
… Kuna nyakati ambapo kuwa mpatanishi ina maana kwamba tunakataa msukumo wa kujibu na badala yake, kwa heshima, tunabaki kimya. …
… Cha kusikitisha, si wote watabaki imara katika upendo wao kwa Mwokozi na azimio lao la kushika amri Zake. …
Sisi pia tunaweza kujiondoa kwenye mabishano na kubariki maisha ya wengine huku tukiwa hatujitengi katika kona yetu wenyewe. …
Na tumpende Yeye na kupendana mmoja kwa mwingine. Na tuwe wapatanishi, kwamba tuweze kuitwa “wana wa Mungu,”