“Sasa Ndiyo Wakati,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2022.
Kikao cha Jumapili Alasiri
Sasa Ndiyo Wakati
Dondoo
Siku za baadaye daima hazitabiriki. Hali ya hewa hubadilika. Hali za kiuchumi hazitabiriki. Majanga ya asili, ajali na magonjwa yanaweza kubadilisha maisha kwa haraka. Matukio haya kwa sehemu kubwa yako nje ya uthibiti wetu. Lakini yako mambo tunayoweza kuyadhibiti, ikijumuisha jinsi tunavyoutumia muda wetu kila siku. …
Ndiyo, tunapaswa kujifunza kutokana na yaliyopita na ndiyo, tunapaswa kujitayarisha kwa ajili ya siku za baadaye. Lakini ni sasa pekee tunaweza kufanya hivyo. Sasa ndiyo wakati tunapoweza kujifunza. Sasa ndiyo wakati tunapoweza kutubu. Sasa ndiyo wakati tunapoweza kuwabariki wengine na “kuinyoosha mikono iliyolegea.”Waebrania 12:12]. …
… Ninarudia kusihi kwangu tangu asubuhi ya leo kufanya mambo yale ambayo yatakuongezea msukumo chanya wa kiroho, msukumo ule ambao Mzee Dieter F. Uchtdorf aliuzungumzia, ambao utakufanya usonge mbele kupita changamoto na fursa zozote zinazokuja.
Msukumo chanya wa kiroho unaongezeka tunapoabudu hekaluni na kukua katika uelewa wetu juu ya upana na kina cha baraka tunazopokea huko. Ninawasihi kukinzana na njia za kiulimwengu kwa kufokasi kwenye baraka za milele za hekaluni. …
Ninawapenda, kaka zangu na dada zangu wapendwa. La muhimu zaidi, Bwana anawapenda. Yeye ni Mwokozi wenu na Mkombozi wenu. Anaelekeza na kuliongoza Kanisa Lake. Na tuwe watu wenye kumstahili Bwana, ambaye alisema, “Mtakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wenu” [Yeremia 30:22].