2022
Usiwe na Hofu: Amini Tu!
Mei 2022


“Usiwe na Hofu: Amini Tu!,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2022.

Kikao cha Jumamosi Alasiri

Usiwe na Hofu: Amini Tu!

Dondoo

Picha
bango la mbingu zenye nyota

Pakua PDF

Kwa hali zetu za sasa, ni ya kueleweka ikiwa mtazamo wa kuwa kijana unapungua kidogo. …

Ombi langu leo kwa vijana, nanyi wazazi na watu wazima mnaowashauri, ni kuanza kutafuta furaha yenu kwa kukumbatia wingi ambao tumekwishapokea kutoka kwa mtoaji wa kila kilicho chema. Katika wakati hasa ambapo wengi ulimwenguni wanauliza maswali ya dhati ya nafsi, tunapaswa kuyajibu kwa “habari njema” ya injili ya Yesu Kristo. Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, ambalo huinua misheni na ujumbe wa Mwokozi wa ulimwengu, linatoa njia ya msingi ya milele kwa vyote kutafuta mema na kutenda mema katika wakati kama huu wa uhitaji. …

Kwa kijana wetu yeyote huko nje ambao wanapitia magumu, bila kujali matatizo au magumu yako, kifo kwa kujiua siyo suluhisho. Hakitapoza maumivu unayohisi au yale unayodhani umeyasabisha. Katika ulimwengu ambao unahitaji sana kila nuru unayoweza kupata, tafadhali acha kupunguza nuru ya milele ambayo Mungu ameiweka nafsini mwako kabla ya ulimwengu huu kuwepo. Zungumza na mtu. Omba msaada. Tafadhali acha kuangamiza uhai ambao ilimgharimu Kristo kuutoa uhai Wake ili kuulinda. Unaweza kukabiliana na changamoto za maisha haya kwa sababu tutakusaidia kukabiliana nazo. Una nguvu sana kuliko unavyofikiria. Msaada unapatikana, kutoka kwa wengine na hususan kutoka kwa Mungu. Wewe unapendwa na kuthaminiwa na unahitajika. Tunakuhitaji! “Usiwe na hofu: amini tu.” …

… Tunayo mengi sana ya kufurahia. Tuna kila mmoja wetu na tunaye Mungu. Usitunyime nafasi ya kuwa na wewe.

Chapisha