2022
Huduma ya Umisionari Imebariki Maisha Yangu Milele
Mei 2022


“Huduma ya Umisionari Imebariki Maisha Yangu Milele,” Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2022.

Kikao cha Jumamosi Asubuhi

Huduma ya Umisionari Imebariki Maisha Yangu Milele

Dondoo

Picha
bango la wamisionari

Pakua PDF

Kama nilivyotazama nyuma katika maisha yangu, nimeweza kuona baadhi ya uzoefu ambao ulileta utofauti mkubwa. Mojawapo ya uzoefu huo ni jinsi huduma yangu ya umisionari nikiwa kijana huko Uingereza ilivyobariki maisha yangu na kujenga hatima yangu ya kiroho. …

Huduma yangu ya umisionari iliniandaa kuja kuwa mume na baba bora na kufanikiwa katika biashara. Pia iliniandaa kwa ajili ya huduma ya maisha yote kwa Bwana katika Kanisa Lake. …

Bwana anakujua. Unapohudumu misheni yako, utapata uzoefu ambao utakusaidia wewe kumjua Yeye vyema. …

Kama Mtume wa Bwana Yesu Kristo, sasa ninatoa wito kwenu ninyi wavulana—na wasichana wale ambao mna hamu ya kuhudumu misheni—kuanza sasa hivi kuzungumza na wazazi wenu kuhusu kuhudumu misheni. Pia ninawaalika mzungumze na rafiki zenu kuhusu kuhudumu misheni, na ikiwa mmoja wa rafiki zenu hana uhakika kuhusu kuhudumu, wahimizeni wazungumze na askofu wao.

Jiwekeeni nadhiri kwenu wenyewe na kwa Baba wa Mbinguni kwamba mtahudumu misheni na kwamba kutoka wakati huu na kuendelea mtajitahidi kuiweka mioyo yenu, mikono yenu, na mawazo yenu safi na yenye kustahili. Ninawaalika mpate ushuhuda imara wa injili ya urejesho ya Yesu Kristo. …

Ni sala yangu kwamba ninyi wavulana na wasichana na wazazi wenu mtaona na kujua jinsi huduma ya umisionari itakavyobariki maisha yenu milele.

Chapisha