2022
Imara katika Dhoruba
Mei 2022


“Imara katika Dhoruba,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2022.

Kikao cha Jumamosi Asubuhi

Imara katika Dhoruba

Dondoo

bango la mnara wa taa

Pakua PDF

Kwa wale kati yetu ambao tunajijali sisi wenyewe pamoja na wale tunaowapenda, kuna tumaini katika ahadi ya Mungu aliyoifanya ya mahali pa usalama katika dhoruba zijazo. …

Maneno ya kinabii ya Mfalme Benyamini yanatumika kwetu katika siku yetu. …

Aliwaalika watu wake na sisi kujenga juu ya mwamba imara wa usalama, ambao ni Mwokozi. Aliweka wazi kwamba tunayo haki ya kujiamulia kati ya kilicho sahihi na kisicho sahihi na kwamba hatuwezi kuepuka matokeo ya chaguzi zetu. …

Asili zetu hubadilika na kuwa kama mtoto mdogo, watiifu kwa Mungu na wenye kupenda zaidi. Badiliko hilo litatufanya tustahili kufurahia vipawa ambavyo huja kupitia Roho Mtakatifu. Kuwa na wenzi wa Roho kutatufariji, kutuongoza na kutuimarisha.

Wakati dhoruba katika maisha zinapokuja, unaweza kuwa imara kwa sababu unasimama kwenye mwamba wa imani yako katika Yesu Kristo. Imani hiyo itakuongoza kwenye toba ya kila siku na kwa uthabiti kushika maagano. Ndipo daima utamkumbuka Yeye. Na kupitia dhoruba za chuki na uovu, utahisi kuwa imara na mwenye tumaini. …

… Kama mtoto mnyenyekevu na mwenye upendo, kubali msaada Wake. Weka na kuyashika maagano ambayo Yeye huyatoa katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Maagano yatakuimarisha. Mwokozi anaifahamu dhoruba na sehemu zenye usalama katika njia ya kwenda nyumbani Kwake na kwa Baba yetu wa Mbinguni. Yeye anaijua njia. Yeye ni njia.