2023
Misheni Yangu Endelevu
Julai 2023


“Misheni Yangu Endelevu,” Liahona, Julai 2023.

Sauti za Watakatifu wa Siku za Mwisho

Misheni Yangu Endelevu

Barua ya mwisho ya baba yangu ilinivusha katika siku zangu za baadaye, ikinipa maneno ambayo yalimaanisha kila kitu kwangu.

Picha
fungua bahasha na barua

Nilikuwa nafurahia misheni yangu katika milima mizuri ya Cajamarca, Peru, wakati baba yangu ghafla alipatwa na kiharusi. Muda mfupi baadae, alifariki.

Nilipokutana na rais wangu wa msiheni, nililia nilipokuwa nakumbuka kwamba baba yangu alinifundisha kile ilichokuwa inamaanisha kuwa mmsisionari na kuwa mtu wa uadilifu. Aliniandikia kila wiki, akishiriki ushuhuda wake, akinifundisha ufahamu mkubwa wa kiroho, na kunihimiza kufanya kadiri niwezavyo.

Baada ya kikao, rais wa misheni alinipa barua—ya mwisho kutoka kwa baba yangu. Barua yake ilinivusha katika siku zangu za baadaye, ikinipa maneno ambayo yalimaanisha kila kitu kwangu.

“Unayo [misheni] nyingine miezi michache ijayo—misheni ngumu sana, ambapo utatakiwa kuweka wakfu maisha yako kwenye kanuni ambazo umezifundisha, kufanya vitu ambavyo, mpaka wakati huu, umevifundisha tu. Inaweza kuwa misheni yenye kuzaa matunda sana. Wewe ni kama hamira katika mkate. …

“Tunakupenda na kukuombea kila siku. Fanya kazi kwa bidii na fanya vitu vyema.”

Niliposoma maneno yake, nililia—kwa huzuni, nikijua yalikuwa maneno yake ya mwisho kwangu katika maisha haya, na kwa shangwe, nikijua nguvu na lengo la maneno hayo kwangu. Nilijua kwamba misheni yangu iliyofuatia—maisha yangu yote—yatakuwa ni kila kitu. Itakuwa ni muda wa majaribu halisi, na itahitaji yale yote niliyojifunza na kupitia kama mmisionari.

Najua kwamba Baba wa Mbinguni ana mpango wa dhati kwa kila mmoja wetu. Anaweza kuinua hali zetu hapa duniani na kutupatia macho ya kuona na kujua ukweli Wake. Nimeliona hili kwa kadiri nilivyoyakita maisha yangu Kwake na kupokea baraka zake. Na nimeliona hili wakati mimi na mke wangu tulipofanya kazi pamoja kujenga familia iliyojaa tumaini, watoto na injili.

Mwokozi ametutia nguvu tuliposali, kusoma maandiko, kwenda hekaluni na kwa wengine katika huduma. Nimeuona mkono wa Bwana ukikunjuliwa wakati wa nyakati za ajabu katika maisha yangu kwa kushiriki injili pamoja na familia yangu na marafiki.

Kazi Yake ni “kuleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu” (Musa 1:39). Misheni kweli bado inaendelea.

Chapisha