“Ni kwa Jinsi Gani Unaishi kwa Fundisho la Kristo?,” Liahona, Julai 2023.
Njoo, Unifuate
Ni kwa Jinsi Gani Unaishi kwa Fundisho la Kristo?
Baada ya Roho kujazwa kwa wingi katika siku ya Pentekoste, Petro na Mitume wengine walimshuhudia Kristo na kufundisha mafundisho Yake. Watu “wakachomwa mioyo yao” na kuuliza, “Tutendeje, ndugu zetu?” (Matendo ya Mitume 2:37). Petro aliwaalika kutubu, kubatizwa na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu (ona Matendo ya Mitume 2:38). Takribani watu 3,000 “waliopokea neno lake [na] wakabatizwa” (Matendo ya Mitume 2:41).
Kutumia mafundisho ya Kristo hutuleta karibu Naye. Tafakari jinsi unavyotumia maeneo haya matano ya kimafundisho:
-
Imani katika Bwana Yesu Kristo: Ni tabia na shughuli zipi husaidia kuchochea imani yako katika Yesu Kristo?
-
Toba: Ni kwa jinsi gani unafanya toba kuwa mchakato wa shangwe?
-
Ubatizo: Unafanya nini ili kuishi maagano yako ya ubatizo?
-
Kipawa cha Roho Mtakatifu: Ni mazingira yapi na shughuli ambazo hukupa wewe fursa nzuri zaidi ya kupokea misukumo ya Roho?
-
Kuvumilia mpaka mwisho: Ni kwa jinsi gani kutunza maagano yako, kuwa na tumaini kwa Kristo na kushikilia kwa nguvu fimbo ya chuma kumekusaidia kuvumilia majaribu makali? Ona Yeremia 17:7; 2 Nefi 31:20; Etheri 12:4.