Agano la Kale 2022
Mei 2–8. Kutoka 35–40; Mambo ya Walawi 1; 16; 19: “Utakatifu kwa Bwana”


“Mei 2–8. Kutoka 35–40; Mambo ya Walawi 1; 16; 19: ‘Utakatifu kwa Bwana,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)

“Mei 2–8. Kutoka 35–40; Mambo ya Walawi 1; 16; 19,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2022

Picha
Hekalu la São Paulo Brazil

Mei 2–8

Kutoka 35–40; Mambo ya Walawi 1; 16; 19

“Utakatifu kwa Bwana”

Unapojifunza maandiko, weka umakini katika misukumo ya kiroho unayoipokea kuhusu namna unavyoweza kuwa zaidi kama Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Andika Misukumo Yako

Kuondoka Misri—kama jinsi ilivyokuwa muhimu na ya kimiujiza—haikukamilisha nia ya Mungu kwa wana wa Israeli. Hata ustawi wa baadae katika nchi ya ahadi haikuwa kilele cha malengo ya Mungu kwa ajili yao. Hizi zilikuwa tu ni hatua kuelekea kwenye kile Mungu alichotaka kwa ajili ya watu Wake: “Mtakuwa watakatifu: kwani Mimi Bwana Mungu wenu ni mtakatifu” (Mambo ya Walawi 19:2). Ni kwa namna gani Mungu alitafuta kuwafanya watu Wake kuwa watakatifu wakati hawakujua kitu kingine chochote bali utumwa kwa vizazi vingi? Aliwaamuru kutengeneza mahali pa utakatifu kwa ajili ya Bwana—tabenako nyikani. Aliwapa maagano na sheria kuongoza matendo yao na, hatimaye, kubadili mioyo yao. Na pale walipoanguka katika jitihada zao za kushika sheria hizo, Aliwaamuru kutoa sadaka ya wanyama kuwakilisha upatanisho wa dhambi zao. Haya yote yalikusudia kuelekeza mawazo yao, mioyo yao, na maisha yao kuelekea kwa Mwokozi na ukombozi ambao Yeye hutoa. Yeye ni njia ya kweli ya utakatifu, kwa Waisraeli na kwetu sisi. Wote tumekaa kwa muda kwenye utumwa wa dhambi, na wote tunakaribishwa kutubu—kuacha dhambi nyuma na kumfuata Yesu Kristo, ambaye ameahidi, “ninaweza kuwatakasa” (Mafundisho na Maagano 60:7).

Kwa ajili ya muhtasari wa kitabu cha Mambo ya Walawi, ona “Mambo ya Walawi” katika Kamusi ya Biblia.

Picha
Learn More image
Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Kutoka 35–40; Mambo ya Walawi 19

Bwana ananitaka mimi niwe mtakatifu kama Yeye alivyo.

Kutoka 25–31 imeandikwa maelekezo ya Bwana kwa Waisraeli kuhusu namna ya kujenga tabenako, ambapo ibada takatifu zingewasaidia kuwa watu watakatifu. Kutoka 35–40 inaelezea juhudi za Waisraeli za kutii maelekezo haya. Unaposoma sura ya 35–40, angalia vitu ambavyo Bwana aliwataka watu Wake kuviweka kwenye tabenako, na tafakari vitu hivi vingeweza kuwakilisha nini na vinapendekeza nini kwako kuhusu kuongezeka katika utakatifu. Hasa fikiria kwa namna gani vitu hivi hugeuza fikra zako kumwelekea Mwokozi. Jedwali kama hili linaweza kukusaidia:

Ni kitu gani ulichopata?

Hiki kinaweza kuwakilisha nini?

Ni kitu gani ulichopata?

Sanduku la agano (Kutoka 37:1–9; 40:20–21)

Hiki kinaweza kuwakilisha nini?

Uwepo wa Mungu; Maagano na amri zake

Ni kitu gani ulichopata?

Madhabahu ya uvumba (Kutoka 40:26–27; ona pia Kutoka 30:1, 6–8)

Hiki kinaweza kuwakilisha nini?

Sala zikipanda kuelekea kwa Bwana

Ni kitu gani ulichopata?

Kinara cha mshumaa au kinara cha taa (Kutoka 37:17–24)

Ni kitu gani ulichopata?

Madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa (Kutoka 38:1–7; ona pia Kutoka 27:1; 29:10–14)

Ni kitu gani ulichopata?

Birika (beseni) la maji (Kutoka 30:17–21)

Kama umeshiriki ibada za hekaluni, unajifunza nini kuhusu tabenako kutoka katika Kutoka 35–40 ambacho kinakukumbusha wewe uzoefu wako huko? (ona pia “Mawazo ya Kuzingatia: Tabenako na Sadaka ya Kuteketezwa”). Tafakari ni kwa namna gani maagano ya hekaluni hukusaidia kuwa zaidi kama Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Ndio, kuwa tu katika sehemu takatifu haitufanyi sisi kuwa watakatifu. Mambo ya Walawi 19 inaelezea sheria na amri Bwana alizowapa Waisraeli ili kuwasaidia kuongeza utakatifu. Unagundua nini katika amri hizi ambacho kinaweza kukusaidia kuwa mtakatifu zaidi? Je, unahisi kutiwa msukumo kufanya nini ili kuishi kanuni hizi kwa ukamilifu zaidi?

Ona pia Carol F. McConkie, “Uzuri wa Utakatifu,” Liahona, Mei 2017, 9–12; “The Tabernacle” (video), ChurchofJesusChrist.org; Bible Dictionary, “Holiness”; temples.ChurchofJesusChrist.org.

Kutoka 35:436:7

Bwana ananitaka mimi kutoa matoleo yangu kwa moyo wa utashi.

Katika mwaka baada ya kutoka Misri, mahusiano ya wana wa Israeli na Yehova yangeweza kuelezewa kama yasiyo na uwiano. Na bado, unaposoma Kutoka 35:436:7, tazama namna gani Waisraeli walivyoitikia amri ya kujenga tabenako. Unajifunza nini kutokana kwa Waisraeli ambacho kingeweza kukusaidia kumtumikia Bwana vizuri zaidi?

Rais Bonnie L. Oscarson alifundisha: “Kila muumini lazima ajue ni kwa kiasi gani anahitajika. Kila mtu ana kitu muhimu cha kuchangia na ana talanta na uwezo maalumu ambao unasaidia kupeleka kazi hii muhimu mbele” (“Wasichana katika Kazi,” Liahona, Mei 2018, 37). Unaposoma Kutoka 36:1–4, tafakari kile ambacho Bwana “ameweka” ndani yako. Zingatia kumuuliza Baba wa Mbinguni kitu gani Amekupa wewe ili uweze kushiriki katika kazi yake.

Picha
watu wa kale wakileta matoleo kwa ajili ya kujenga tabenako

Wana wa Israeli walitoa matoleo kwa ajili ya tabenako wakiwa na “moyo wa kupenda” (Kutoka 35:5). Kielelezo na Corbert Gauthier, © Lifeway Collection/licensed from goodsalt.com

Mambo ya Walawi 1:1–9; 16

Kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, ninaweza kusamehewa.

Mengi katika kitabu cha Mambo ya Walawi yanaweza kuonekana mageni kwetu—sadaka za wanyama, mila zikihusisha damu na maji, na sheria zinazotawala mambo madogo madogo ya maisha. Ila mila hizi na sheria vilinuiwa kufundisha kanuni zinazofahamika—toba, utakatifu, na Upatanisho wa Mwokozi. Ili kupata kanuni hizi unaposoma Mambo ya Walawi 1:1–9; 16, fikiria maswali kama haya: Ninaweza kujifunza nini katika sadaka hizi kuhusu Yesu Kristo na dhabihu Yake ya upatanisho? Ni kwa namna gani niko kama wale wanaofanya sadaka hizi? Unaweza pia kufikiria kupitia “Mawazo ya kuweka akilini: Tabenako na Sadaka” katika nyenzo hii na “Sadaka” katika Mwongozo wa Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org).

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Kutoka 36:1–7.Katika Kutoka 36:1–7, tunajifunza nini kutokana na namna Waisraeli walivyoitikia amri ya kujenga tabenako? Kama familia, mngeweza kufikiria njia ambazo kwazo Bwana ametualika kushiriki katika kazi yake. Ni kwa namna gani tunaweza kufuata mfano wa Waisraeli?

Kutoka 40.Mnaposoma Kutoka 40 pamoja, ungeweza kuwaalika wanafamilia kuinua mikono yao kila mara wanaposikia kirai kama “kama Bwana alivyoamuru.” Tunaweza kujifunza nini kutoka kwenye sura hii kuhusu utiifu kwa Bwana?

Kutoka 40:1–34.Mnaposoma kuhusu kusanyiko la tabenako katika Kutoka 40, mngeweza kufanya kazi pamoja kutambua sehemu tofauti za tabenako, mkitumia picha ambayo imeambatanishwa na muhtasari huu. Kuunganisha majadiliano haya na kuabudu kwenye hekalu katika nyakati zetu, mnaweza kurudia kwa pamoja “Kwa nini Watakatifu wa Siku za Mwisho Hujenga Mahekalu” (temples.ChurchofJesusChrist.org) au tazama video “Temples” (ChurchofJesusChrist.org

Mambo ya Walawi 19.Kila mwanafamilia angeweza kutafuta mstari katika sura hii ambao wanahisi unaweza kuwasaidia “kuwa watakatifu” (Mambo ya Walawi 19:2) na kuushiriki na wanafamilia.

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “More Holiness Give Me,” Nyimbo za Kanisa, na. 131.

Kuboresha Kujifunza Binafsi

Mtafute Yesu Kristo. Maandiko yote, hata Agano la Kale, hushuhudia kuhusu Yesu Kristo. Unaposoma Agano la Kale, fikiria kile ambacho ishara, watu, na matukio vinaweza kukufundisha juu ya Mwokozi.

Picha
tabenako

Tabenako la Kale, na Bradley Clark

Chapisha