Maandiko Matakatifu
Alma 33


Mlango wa 33

Zeno alifundisha kwamba watu waombe na kuabudu mahali popote, na kwamba hukumu zimeondolewa kwa sababu ya Mwana—Zenoki alifundisha kwamba rehema inatolewa kwa sababu ya Mwana—Musa aliinua nyikani mfano wa Mwana wa Mungu. Karibia mwaka 74 K.K.

1 Sasa baada ya Alma kumaliza kusema maneno haya, walimtumia mnenaji wakitamani kujua kama wangeweza kumwamini katika Mungu mmoja, ili waweze kupokea hilo tunda ambalo alilizungumzia, au vile wangeweza kupanda ile mbegu, au hilo neno ambalo alilizungumzia, ambalo alisema lazima lipandwe ndani ya mioyo yao; au jinsi gani wangeanza kutumia imani yao.

2 Na Alma akawaambia: Tazama, mmesema kwamba hamuwezi kumwabudu Mungu wenu kwa sababu mmetupwa nje ya masinagogi yenu. Lakini tazama, ninawaambia, ikiwa mnadhani ati hamuwezi kumwabudu Mungu, mnafanya kosa kubwa, na mnahitaji kupekua maandiko; ikiwa mnadhania kwamba yamewafundisha hii, ninyi hamuelewi.

3 Je, mnakumbuka mlisoma yale ambayo Zeno, nabii wa kale, aliyosema kuhusu sala au ibada?

4 Kwani alisema: Wewe una rehema, Ee Mungu, kwani umesikia sala yangu, hata nilipokuwa nyikani; ndiyo, ulikuwa mwenye rehema wakati niliposali kuhusu wale ambao walikuwa maadui zangu, na ukawarudisha kwangu.

5 Ndiyo, Ee Mungu, na ulikuwa na rehema kwangu wakati nilipokulilia kwenye shamba langu; wakati nilipokulilia kwa sala yangu, na ulinisikiliza.

6 Na tena, Ee Mungu, wakati nilipoingia kwenye nyumba yangu ulinisikia mimi kwenye sala yangu.

7 Na wakati nilipoingia katika kijumba changu, Ee Bwana, na kuomba kwako, na ulinisikia.

8 Ndiyo, una huruma kwa watoto wako, wakati wanakulilia wewe, ili wasikilizwe nawe na sio na watu, na utawasikiliza.

9 Ndiyo, Ee Mungu, umekuwa na rehema kwangu, na kusikia vilio vyangu miongoni mwa umati wako.

10 Ndiyo, na pia umenisikia wakati nimetupwa nje na kudharauliwa na maadui zangu; ndiyo, ulisikia vilio vyangu, na uliwakasirikia maadui zangu, na ukawatembelea kwa ghadhabu yako na maangamizo ya haraka.

11 Na wewe ulinisikia kwa sababu ya mateso yangu na uaminifu wangu; na ni kwa sababu ya Mwana wako kwamba umekuwa na rehema jinsi hivyo kwangu, kwa hivyo nitakulilia wewe katika mateso yangu yote, kwani nina shangwe ndani yako; kwani umeniondolea hukumu zako, kwa sababu ya Mwana wako.

12 Na sasa Alma aliwaambia: Mnaamini hayo maandiko ambayo yaliandikwa na wale wa kale?

13 Tazama ikiwa mnayaamini, lazima mwamini yaliyosemwa na Zeno; kwani tazama, alisema: Umeondoa hukumu zako kwa sababu ya Mwana wako.

14 Sasa, tazama, ndugu zangu, ningeuliza kama mmesoma maandiko? Ikiwa mmeyasoma, jinsi gani mnaweza kutomwamini Mwana wa Mungu?

15 Kwani haikuandikwa kwamba Zeno pekee ndiye alisema vitu hivi, lakini Zenoki pia alizungumzia vitu hivi—

16 Kwani tazama, alisema: Umewakasirikia, Ee Bwana, watu hawa, kwa sababu hawataelewa rehema zako ambazo umewapatia kwa sababu ya Mwana wako.

17 Na sasa, ndugu zangu, mnaona kwamba nabii wa pili wa kale ameshuhudia juu ya Mwana wa Mungu, na kwa sababu ya watu kutoelewa maneno yake walimpiga na mawe hadi akafa.

18 Lakini tazama, haya si yote; hawa sio pekee ambao wamezungumza kuhusu Mwana wa Mungu.

19 Tazama, alizungumziwa na Musa; ndiyo, na tazama mfano uliinuliwa nyikani, kwamba yeyote atakayeuangalia aweze kuishi. Na wengi waliangalia na wakaishi.

20 Lakini wachache walielewa maana ya vitu hivyo, na hii ni kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao. Lakini kulikuwa na wengi ambao walikuwa wagumu kiasi kwamba hawangeangalia, kwa hivyo waliangamia. Sasa sababu yao ya kukataa kuangalia ni kwa sababu hawakuamini kwamba ingewaponya.

21 Ee ndugu zangu, ikiwa mngeponywa tu kwa kuangalia na macho yenu ili muweze kuponywa, msingetazama haraka, au ni afadhali mshupaze mioyo yenu kwa kutokuamini, na kuwa wavivu, kwamba msiangalie kwa macho yenu ili mweze kuangamia?

22 Ikiwa hivyo, taabu itawapata; lakini ikiwa si hivyo, basi zungusha macho yako na uanze kuamini katika Mwana wa Mungu, kwamba atakuja kukomboa watu wake, na kwamba atateseka na kufa ili alipie dhambi zao; na kwamba atafufuka tena kutoka kwa wafu, na kutimiza ufufuo, kwamba watu wote watasimama mbele yake, kuhukumiwa katika siku ya mwisho ya hukumu, kulingana na matendo yao.

23 Na sasa, ndugu zangu, natamani kwamba mtapanda hili neno kwenye mioyo yenu, na itakavyoanza kumea endelea kuvimba kwa imani yenu. Na tazama, itakuwa mti, ukikua ndani yako kwenye maisha yasiyo na mwisho. Na kisha Mungu akubali kwamba mizigo yenu iwe miepesi, kupitia kwa shangwe inayotokana na Mwana wake. Na hata haya yote mnaweza mkafanya mkipenda. Amina.