Mkutano Mkuu
Yesu Kristo kwenye Kitovu cha Maisha Yetu
Mkutano mkuu wa Aprili 2024


Yesu Kristo kwenye Kitovu cha Maisha Yetu

Maswali muhimu ya nafsi, yale yanayojitokeza katika saa yetu ya giza na majaribu ya juu zaidi, yanashughulikiwa kwa njia ya upendo usioyumba wa Yesu Kristo.

Tunaposafiri kupitia maisha ya duniani, nyakati fulani tunasongwa na majaribu: majaribu machungu ya kupoteza wapendwa wetu, mapambano makali dhidi ya maradhi, uchungu wa dhuluma, uzoefu wa kutisha wa usumbufu au unyanyasaji, kivuli cha ukosefu wa ajira, dhiki ya kifamilia, kilio cha kimya kimya cha upweke au matokeo ya kuhuzunisha ya migogoro ya matumizi ya silaha. Katika nyakati kama hizo, nafsi zetu zinatamani kimbilio. Tunatafuta kwa dhati kujua: Tupate wapi malhamu ya amani? Katika nani tunaweza kuweka tumaini letu ili atusaidie na kujiamini na nguvu ya kushinda changamoto hizi? Nani mwenye subira, upendo , na mkono wa mwenyezi wa kutuinua na kututegemeza?

Maswali muhimu ya nafsi, yale yanayojitokeza katika saa yetu ya giza na majaribu ya juu zaidi, yanashughulikiwa kwa njia ya upendo usioyumba wa Yesu Kristo. Kwake Yeye, na kupitia baraka zilizoahidiwa za injili Yake ya urejesho, tunapata majibu tunayotafuta. Ni kwa kupitia Upatanisho Wake usio na ukomo ambako tunapewa zawadi isiyopimika—moja ya tumaini, uponyaji na uhakika wa uwepo Wake wa daima na wa kudumu katika maisha yetu. Zawadi hii inapatikana kwa wote wanaomfikia kwa imani, wakikumbatia amani na ukombozi ambao Yeye anautoa bure.

Bwana ananyoosha mkono Wake kwa kila mmoja wetu, ishara ambayo ndio kiini cha upendo na wema Wake mtakatifu. Mwaliko Wake kwetu sisi unapita mwito rahisi, ni ahadi ya kiungu, inayoimarishwa na nguvu ya kudumu ya neema Yake. Katika maandiko, Yeye kwa upendo anatuhakikishia sisi:

“Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

“Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu.

“Kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”

Uwazi wa mwaliko Wake “njooni kwangu” na “jitieni nira yangu” huthibitisha asili ya kina ya ahadi Yake—ahadi kubwa sana na kamilifu inayojumuisha upendo Wake, akitupatia dhamana ya dhati: “mtapata pumziko.”

Kwa bidii tunapotafuta mwongozo wa kiroho, tunaanzisha safari ndefu yenye matukio mengi inayoimarisha ushuhuda wetu. Tonapofahamu ukuu wa Baba wa Mbinguni na upendo mkamilifu wa Yesu Kristo, mioyo yetu hujawa kwa shukrani, unyenyekevu, na hamu iliyofanywa upya ya kufuata njia ya uanafunzi.

Rais Russell M. Nelson alifundisha kwamba: “Wakati fokasi ya maisha yetu iko katika mpango wa Mungu wa wokovu … na Yesu Kristo na injili Yake, tunaweza kuhisi furaha bila kujali nini kinatokea—au kutotokea—katika maisha yetu.” Shangwe inakuja kutoka Kwake na kwa sababu Yake.”

Alma, akizungumza kwa mwanawe Helamani, Alitamka: “Na sasa, Ee mwana wangu Helamani, tazama, wewe ni kijana, na kwa hivyo, nakuomba wewe kwamba usikilize maneno yangu na ujifunze kutoka kwangu; kwani najua kwamba wote watakaoweka imani yao katika Mungu watasaidiwa kwa majaribio yao, na taabu zao, na mateso yao, na watainuliwa juu katika siku ya mwisho.”

Helamani akizungumza na wanawe, alifundisha kuhusu kanuni hii ya milele ya kumweka Mwokozi kwenye kitovu cha maisha yetu: “Kumbukeni, kumbukeni kwamba ni juu ya mwamba wa Mkombozi wetu, ambaye ni Kristo, Mwana wa Mungu, kwamba lazima mjenge msingi wenu.”

Katika Mathayo 14 tunajifunza kwamba baada ya kusikia juu ya kifo cha Yohana Mbatizaji Yesu alitafuta mahali pa upweke. Hata hivyo, umati mkubwa ulimfuata. Akiongozwa na huruma na upendo, na kutoruhusu huzuni Yake kuvuta mawazo Yake kutoka kwa misheni Yake, Yesu aliwakaribisha, akawaponya wagonjwa miongoni mwao. Jioni ilipokaribia, wanafunzi Wake walikabiliwa na changamoto kubwa sana: umati ule wa watu na chakula kidogo kilichokuwepo. Walipendekeza kwa Yesu kwamba awaruhusu umati ule waende kununua chakula, lakini Yesu kwa upendo wa hali ya juu na matarajio ya juu, aliwaomba wanafunzi kuwalisha badala yake.

Wakati wanafunzi wakiwa na mawazo ya changamoto hiyo, Yesu alionyesha matumaini Yake na upendo kwa Baba Yake, ukijumuishwa na upendo usiotingishika kwa watu wale. Akawaelekeza umati kukaa chini juu kwenye nyasi, akachukua vipande vile vitano tu vya mikate na samaki wawili, huku Yeye akichagua kutoa shukrani kwa Baba Yake, akikubali utoaji wa Mungu juu ya mamlaka na uwezo Wake.

Baada ya kutoa shukrani, Yesu aliumega mkate, na wanafunzi wakagawa kwa watu. Kimiujiza, siyo tu chakula kile kilitosha bali kilikuwa kingi na kubakia vikapu 12. Kundi lililolishwa lilijumuisha watu elfu tano, wakiwemo wanawake na watoto.

Muujiza huu unatufundisha somo muhimu: tunapokabiliwa na changamoto, ni rahisi kuzama katika magumu yetu. Hata hivyo, Yesu Kristo alionyesha mfano wa nguvu ya kufokasi juu ya Baba Yake, akitoa shukrani, na kukubali kwamba suluhisho la majaribu yetu siyo daima hututegemea sisi wenyewe, bali kwa Mungu.

Tunapokabiliwa na magumu, kwa asili tunapenda kuelekeza akili kwenye vikwazo tunavyokumbana navyo. Changamoto zetu ni dhahiri na zinaamua umsimamo wetu, lakini kanuni za kuzishinda ziko katika fokasi yetu. Kwa kumweka Kristo katika kiini cha mawazo na matendo yetu, tunajiweka sambamba na mtazamo na nguvu Zake. Marekebisho haya hayapunguzi mapambano yetu; badala yake, yanatusaidia kupitia njia hizo chini ya mwongozo wa kiungu. Kama matokeo, tunagundua suluhisho na msaada ambao unainuka kutoka kwenye hekima ya juu. Kuuasili mtazamo huu wa Kristo kuwa kiini kunatutia nguvu kwa ujasiri na ufahamu kugeuza majaribu yetu kuwa ushindi, ikitukumbusha kwamba kwa Mwokozi, kitu kinachoonekana kama tatizo kubwa kinaweza kuwa njia ya kwenda kwenye ukuaji mkubwa wa kiroho.

Hadithi ya Alma Mdogo katika Kitabu cha Mormoni inatoa simulizi ya kuvutia ya ukombozi na matokeo makubwa ya kuelekeza maisha ya mtu karibu zaidi na Kristo. Mwanzoni, Alma alisimama kama mpinzani wa Kanisa la Bwana, akiwapotosha wengi kutoka kwenye njia ya haki. Hata hivyo, kuingilia kati kwa kiungu kunaashiria kutembelewa na malaika, kulimwamsha kutoka katika makosa yake.

Katika saa yake ya giza, akiteswa na hatia na kukata tamaa ya kutoka katika uchungu wake wa kiroho, Alma alikumbuka mafundisho ya baba yake kuhusu Yesu Kristo na nguvu ya Upatanisho Wake. Akiwa na moyo unaotamani kukombolewa, kwa dhati alitubu na kusihi kwa dhati huruma ya Bwana. Wakati huu muhimu wa kujisalimisha kikamilifu, kumleta Kristo mbele ya mawazo yake kwa kadiri Alma alivyotafuta rehema Yake kwa dhati, kulichochea mageuzi ya ajabu. Minyororo mizito ya hatia na kukata tamaa ilipotea na nafasi yake ilichukuliwa na hisia kubwa ya shangwe na amani.

Yesu Kristo ndiye tumaini letu na jibu la maumivu makubwa zaidi ya maisha. Kupitia dhabihu Yake, Yeye alilipia dhambi zetu na kujichukulia juu Yake mwenyewe mateso yetu yote—maumivu, ukosefu wa haki, huzuni na hofu—na Yeye anatusamehe na kutuponya tunapomtumaini Yeye na kutafuta mabadiliko ya maisha yetu ili kuwa bora. Yeye ni Mponyaji wetu, anayefariji na kutengeneza mioyo yetu kupitia upendo na uwezo Wake, kama tu alivyowaponya wengi wakati akiwa hapa duniani. Yeye ni maji ya uzima, akitimiza mahitaji ya kina ya nafsi zetu kwa upendo na wema Wake thabiti. Hii ni kama ile ahadi aliyofanya kwa mwanamke Msamaria kisimani, akitoa “chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.”

Natoa ushuhuda wa uhakika kuwa Yesu Kristo anaishi, kwamba Anaongoza katika hili, Kanisa Lake takatifu, Kanisa la YESU kristo la Watakatifu wa Sku za Mwisho. Ninashuhudia kwamba Yeye ni MwokozI wa ulimwengu, Mfalme wa Amani, Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana, Mkombozi wa ulimwengu. Ninathibitisha kwa uhakika kwamba sisi daima tuko katika akili na moyo Wake. Kama ushuhuda kwa hili, Yeye amerejesha Kanisa Lake katika hizi siku za mwisho na amemwita Rais Russell M. Nelson kama nabii Wake na Rais wa Kanisa kwa wakati huu. Ninajua alitoa uhai Wake ili kwamba sisi tupate uzima wa milele.

Kadiri tunavyojitahidi kumweka Yeye kwenye kitovu cha maisha yetu, mafunuo yanafunuliwa kwetu, amani Yake muhimu inatufunika, na Upatanisho Wake usio na kikomo unafanikisha msamaha na uponyaji wetu. Ni katika Yeye kwamba tunagundua nguvu ya kushinda, ujasiri wa kuvumilia, na amani ambayo inapita ufahamu wote. Na tujitahidi kila siku kujongea karibu zaidi na Yeye, chanzo cha yote yaliyo mema, mnara wa matumaini katika safari yetu kurudi katika uwepo wa Baba yetu wa Mbinguni. Katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.

Chapisha