Unapokuwa Umevunjika Moyo
Maisha yana kupanda na kushuka. Wakati mwingine tunapokuwa chini, tunajiuliza kile Mungu anachofanya—kwa nini Baba mwenye upendo anaruhusu hili litokee? Mashaka haya yanaweza kupanda juu hata sisi kuuliza, “Hivi Mungu anajali kweli kuhusu mimi binafsi?”
Katika hali kama hii, nimepata maandiko haya kuwa yenye msaada:
-
Zaburi 8:4–5: “Mtu ni kitu gani hata umkumbuke? … Umemfanya mdogo punde kuliko malaika, na umemvika taji ya utukufu na heshima.”
-
Yohana 10:14: wakati wa maisha Yake hapa juu ya dunia, Yesu alijielezea Yeye kama “mchungaji mwema” na kuongeza, “[Mimi] nawajua kondoo wangu.”
-
Musa 1:39: huu ni mmojawapo wa mistari ninayoipenda sana, ambapo Bwana anafunua lengo Lake kwa Nabii Joseph Smith: “Kwa maana tazama, hii ndiyo kazi yangu na utukufu—kuleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu”—hivyo kusisitiza shauku Yake kwetu kama watu binafsi.
-
Luka 7:11–16: Siyo tu maelezo haya yanatufundisha juu ya nguvu ya Mwokozi dhidi ya kifo—ukumbusho muafaka kwenye msimu huu wa Pasaka—lakini kwangu yanawakilisha mfano bora wa uelewa wake makini kwa ajili yetu binafsi. Kati ya miujiza yote ya Yesu, michache ni ororo na yenye huruma kama kuhudumu Kwake kwa mjane wa Naini. Ninaposhiriki katika makala yangu (ona ukurasa wa 12), maelezo haya yanaonyesha kwa mfano shauku ya Mwokozi katika na upendo kwa kila mmoja wetu.
Keith Wilson
Profesa mshiriki, Chuo Kikuu cha Brigham Young