Kama msichana, je, ninapaswa kufokasi zaidi kwenye elimu na kazi au kwenye kuwa mke na mama?
Tunajua kwamba “familia ni kiini cha mpango wa Muumbaji” na kwamba “Akina mama kimsingi wana wajibu wa malezi ya watoto wao.”1 Na pia tunajua kwamba, kwa sababu nyingi nzuri, wote wanaume na wanawake wameshauriwa na manabii kupata elimu.2 Kwa kuongezea, tunajua kwamba wanawake wengi aidha watahitaji au wanataka kutafuta kazi.
Rais Dallin H. Oaks, Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza, amesema kwamba kwa wanawake, uchaguzi si kati ya aidha familia au elimu na kazi. “Muda muafaka ndio tunaopaswa kuchagua,” alisema. “Na tunatafuta mwongozo wa kiungu wa Bwana na mafundisho ya watumishi Wake katika kufanya hilo.”3
Panga kupata elimu, na panga kuwa na familia. Unaweza pia kupanga kuwa na kazi. Katika yote haya, fokasi yako inapaswa kuwa kwenye kufuata mpango wa Baba wa Mbinguni na kutafuta mapenzi Yake.