Kumuona Baba Akiimba
Maria Oka
California, Marekani
Nimekuwa katika misheni yangu huko Honolulu, Hawaii, Marekani, kwa miezi minne na nusu tu wakati nilipopata mshtuko mkubwa wa moyo na baadaye kubainika kuwa na kifafa. Miezi iliyofuata ilileta matembezi ya hospitali, vipimo visivyo na idadi, na dawa mpya yenye matokeo ya kukatisha tamaa.
Kabla ya hapo, nilikuwa nimefokasi sana kwenye kazi ya umisionari kiasi kwamba sikufikiria nyumbani, lakini tangu wakati wa mshtuko wangu wa moyo, moyo ulipata maumivu. Niliwakosa wazazi wangu na kuhisi mpweke hata wakati nilipozungukwa na watu wema, wenye kujali. Sikutaka kwenda nyumbani, bali nilitaka kuhisi amani.
Kwa ruhusa ya rais wangu wa misheni, nilizungumza na wazazi wangu kwenye simu kuhusu matibabu yangu. Baba yangu, ambaye alikuwa ametimiza ndoto yake ya maisha yote ya kujiunga na Kwaya ta Tabernacle ya Temple Square, alinihakikishia kwamba angeimba kwa moyo wake wote kwa ajili yangu katika mkutano mkuu, ambao ulianza siku iliyofuata.
Asubuhi iliyofuata, niliomba kwa dhati kwa ajili ya amani ambayo niliihitaji sana. Nilikuwa nimepokea majibu kwa maswali mahususi wakati wa mkutano mkuu kabla, na niliamini kwamba ningeweza kupokea mwongozo tena. Mkutano ulipoanza, kwaya iliimba “Dearest Children, God Is Near You,” (Nyimbo za Kanisa, na. 96). Ndani ya dakika ya kwanza, nilimwona baba yangu kwenye sikirini ya TV. Kamera ilimulika na kuvuta uso wake kwa muda kadhaa.
Machozi yalikuja machoni mwangu wakati hisia nzuri mno za amani ziliponifunika. Nilijua ya kwamba Mungu alinipenda. Yeye alijua kile hasa nilichohitaji siku ile—hakikisho rahisi kwamba Yeye alikuwa karibu na alikuwa akinifahamu. Nilihisi upendo wa Mungu, na kwa nyongeza, upendo wa familia yangu, wenza wangu, na rais wangu wa misheni. Badala ya kuhisi kulemewa, sasa niliona fursa ya kusogea karibu na Bwana.
Changamoto zangu za kiafya hazikuondoka. Ilinibidi nikatishe misheni yangu mapema baada ya yote, lakini nilijua kwamba Mungu alikuwepo pale na kwamba Yeye alinipenda. Hakikisho hilo limenifuata kupitia maumivu mengine mengi ya moyo na limenipa tumaini katika saa zangu za giza. Wengine wanaweza kuiita bahati, lakini ninajua kwamba kumwona baba akiimba kuhusu upendo wa Mungu ulikuwa ni muujiza mdogo katika wakati wangu wa uhitaji.