Hujambo kutoka Estonia!
Sisi ni Margo na Paolo. Mwaka huu tunasafiri kuzunguka ulimwengu kujifunza kuhusu watoto wa Mungu. Jiunge nasi tunapozuru Estonia!
Estonia iko Ulaya ya kaskazini. Ina visiwa zaidi ya 2,000. Takriban watu milioni 1.3 wanaishi Estonia.
Hivi ndivyo unavyosema “hujambo” kwa Kiestonia: Teres!Na hivi ndivyo unavyosema jina la Kanisa: Viimse Aja Pühade Jeesuse Kristuse Kirik
Hii ni Tallinn, mji mkuu wa Estonia. Umekuwepo kwa miaka 800! Estonia ina nyika nyingi, kama miti na sehemu teketeke. Kwa kweli, zaidi ya nusu ya Estonia imefunikwa na msitu. Watu wengi wa Estonia hupenda kutumia muda kwenye vitu vya asili.
Je, nini ni kwa ajili ya chakula cha usiku Estonia? Labda nguruwe au samaki wa achali na viazi, kabeji, malai chachu, na mkate mweusi. Hiyo huitwa sandwichi ya sprati.
Je, unapenda kuimba katika darasa la Msingi? Kila baada ya miaka mitano, Waestonia hukusanyika kwenye sherehe kubwa kusherehekea nchi yao kwa kuimba na kucheza.
Kanisa katika Estonia ni dogo lakini imara. Kuna takriban waumini elfu moja wa Kanisa. Hekalu lao la karibu liko Helsinki, Finland.
Kutana na wamisionari wawili kutoka Estonia!
Usiku mmoja nilipotaka kwenda kulala, mwanasesere wangu haukuonekana. Niliutafuta lakini sikumpata. Niliomba. Kisha nilimpata mwanasesere wangu na kuwa na ndoto nzuri.
Bianka J., miaka 7
Familia yetu inapenda kuwatumikia wengine. Kutumikia hutusaidia kuhisi Roho Mtakatifu, ambaye hutupatia hisia nzuri ya amani. Mimi na dada yangu hutengeneza zawadi kwa ajili ya wengine kwa sababu tunataka wao wahisi kupendwa.
Piibe J., miaka 10
Asante kwa kutalii Estonia pamoja nasi. Tutaonana wakati mwingine!