2019
Jaribu Baadhi ya Tamaduni Mpya za Pasaka
Aprili 2019


Jaribu Baadhi ya Tamaduni Mpya za Pasaka

Pasaka hii, tumia muda mwingi zaidi kukumbuka zawadi kuu kuliko zote iliyowahi kutolewa.

baby Jesus, Mary and Joseph

Maelezo yamechukuliwa kutoka Kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, na Lynne Millman Weidinger

Krismasi mara nyingi hupata umakini wakati inapofikia mapumziko. Hata hivyo bila matukio ya muda mrefu uliopita tunayo sherehekea kila Pasaka, Krismasi isingekuwepo.

Rais Gordon B. Hincley (1910–2008) aliwahi kufundisha, “Hapangekuwepo na Krismasi kama isingekuwepo Pasaka. Mtoto Yesu wa Bethlehemu angekuwa kama mtoto mwingine tu bila Kristo wa kukomboa wa Gethsemane na wa Kalvari, na ushindi wa kweli wa Ufufuko.”1

Hapa kuna baadhi ya tamaduni chache ambazo ungeweza kufikiria kuongeza kwenye usherehekeaji wako wa mapema.

1. Nenda Kaimbe Nyimbo za Furaha

kids singing

Ukiachilia mbali tafsiri ya ajabu ajabu kuhusu kulungu na kibwengo, Krismas ni kuhusu Yesu Kristo. Pasaka ni wakati muafaka kwa ajili ya muziki kuhusu Mwokozi, na ndiyo, hata kama ukiimbwa mbele ya milango ya jirani zako.

Kama umeishiwa na mawazo, angalia kipengele cha “mada” cha kitabu cha nyimbo za kanisa kwenye “Pasaka” na “Upatanisho” kwa ajili ya nyimbo. Wimbo wowote unaomsifu Yesu Kristo ni sahihi kwa ajili ya nyimbo za furaha za Pasaka.

2. Msamehe Mtu

girls hugging

Ni mara ngapi umekuwa na shukrani kwa zawadi ya toba? Pasaka inatoa fursa ya kuweka mawazo zaidi kwenye jinsi tunavyotoa roho sawa na hiyo ya msamaha kwa wengine.

Yesu alifundisha: “Kwa hiyo, ninawaambia, kwamba mnapaswa kusameheana ninyi kwa ninyi. …

“Mimi, Bwana, nitamsamehe yule nitakaye kumsamehe, lakini ninyi mnatakiwa kuwasamehe watu wote” (Mafundisho na Maagano 64:9–10).

Jiulize: Ni nani unayehifadhi hisia mbaya dhidi yake? Omba kwa ajili ya nguvu ili kumsamehe mtu huyu, na mwache Mwokozi asaidie hisia hizo za uchungu kutoweka.

3. Vaa sura ya Kuigiza, Kucheza au Uigizaji mwingine

boy dressed up

Unaweza kuandaa igizo la Pasaka. Mfano rahisi unaweza kuwa usomaji wa maandiko kwa ajili ya jioni ya familia nyumbani au tamasha la kuimba pamoja na jumuia.

4. Tembelea Makaburi ya Wapendwa Wako

family visiting graves

Kwa sababu ya Yesu Kristo, kifo kimepoteza uchungu wake (ona 1 Wakorintho 15:55). Tumia muda kutembelea makaburi ya wapendwa wako kutafakari habari hii njema.

Unaweza hata kusoma kwa sauti baadhi ya maandiko unayoyapenda ambayo yanahusiana na Ufufuo wakati ukitembelea makaburi haya. machache (kati ya maandiko mengi) ya kuzingatia kwa ajili ya hili ni 1 Wakorintho 15:20–22; Alma 11:42–44; na Mafundisho na Maagano 88:14–16

5. Kuwa Bora Zaidi

Christ visiting the Americas

Maelezo yamechukuliwa kutoka Yesu Kristo Anazuru Amerika, na John Scott

Pasaka inaheshimu matukio ya Gethsemane, kilichotukia msalabani, Mwokozi kufufuka kutoka wafu siku ya tatu, na kisha kuhudumu Kwake kwa siku 40 kabla ya kupaa mbinguni.

Kwa kuongezea, muda mfupi baada ya kupaa mbinguni, Yesu Kristo aliwatokea Wanefi na kuwahudumia (ona 3 Nefi 11–28). Hayo ni mengi ya kusherehekea!

Kwa nini usipanue msimu wako wa Pasaka? Acha nafsi yako ifurahie kwa muda mrefu katika miujiza ya Pasaka. Fanya juhudi za makusudi kuwa zaidi kama Kristo kipindi cha siku 40 baada ya Pasaka. Kwa ajili ya msukumo, fikiria mwaliko ufuatao kutoka kwa Rais Russell M. Nelson: “Weka wakfu sehemu ya muda wako kila wiki ili kujifunza kila kitu Yesu alichosema na kufanya kama ilivyoandikwa katika Agano la Kale, kwani Yeye ni Yehova wa Agano la Kale. Jifunze sheria Zake kama zilivyoandikwa katika Agano Jipya, kwani Yeye ni Kristo wake. Jifunze mafundisho Yake kama yalivyoandikwa katika Kitabu cha Mormoni, kwani hakuna kitabu cha maandiko ambacho kwacho kazi Yake na huduma Yake vimefunuliwa wazi. Na jifunze maneno Yake kama yalivyoandikwa katika Mafundisho na Maagano, kwani anaendelea kufundisha watu Wake katika kipindi hiki cha maongozi ya Mungu.”2

Tamaduni Zako Zinasubiri

Mzee Dieter F. Uchtdorf wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili amefundisha, “Kujua siku muhimu zaidi katika historia, lazima turudi nyuma kwenye jioni ile karibu miaka 2000 iliyopita katika Bustani ya Gethsemane wakati Yesu Kristo alipopiga magoti kuomba na kujitoa Yeye Mwenyewe dhabihu kama malipo ya dhambi zetu.”3

Matukio muhimu zaidi katika historia yana thamani kutengewa muda wa kutafakari kila mwaka. Tamaduni hutusaidia kufanya hivyo, iwe ni zile zilizopo kwenye orodha hii au yoyote ile utakayochagua.

Ni kipi utaongeza mwaka huu?

Muhtasari

  1. Gordon B. Hinckley, “Maajabu na Hadithi ya Kweli ya Krismasi,” Ensign, Des. 2000, 5.

  2. Russell M. Nelson, “Manabii, Uongozi, na Sheria Takatifu” (worldwide devotional for young adults, Jan. 8, 2017), broadcasts.lds.org.

  3. Dieter F. Urchtdorf, “Tazama Mtu!” 107–10 Liahona, Mei. 2018, 108.