Manabii na Mitume wetu
Yesu Kristo anaongoza Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kupitia manabii na mitume. Soma kuhusu wao hapa chini. Kisha kata na uondoe picha kwenye ukurasa wa R23 na uzigandishe mahali pake katika chati. Weka gundi juu ya kila picha ili uweze kuziinua kwa ajili ya kusoma kweli zilizoko chini!
Rais Russell M. Nelson
Rais wa 17 wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho
-
Alikuwa daktari mpasuaji wa moyo
-
Alijifunza lugha nyingi, ikiwemo Kichina
-
Ana watoto kumi: 9 mabinti na 1 wa kiume
Rais Dallin H. Oaks
Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza
-
Alisafisha duka la ufundi redio kama kazi yake ya kwanza
-
Alikuwa mwanasheria na hakimu wa Juu wa Mahakama ya Utah
-
Alikuwa rais wa Chuo Kikuu cha Brigham Young
Rais Henry B. Eyring
Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza
-
Alicheza mpira wa kikapu akiwa shule ya upili
-
Alijifunza fizikia kutoka kwa baba yake kwenye ubao wa chaki wa familia yao
-
Alikuwa rais wa Chuo cha Ricks, sasa Chuo Kikuu cha Brigham Young–Idaho
Rais M. Russell Ballard
Kaimu Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili
-
Alipewa jina la utani la “askofu” alipokuwa chuoni kwa sababu ya viwango vyake vya juu
-
Alikuwa mfanyabiashara wa magari
-
Alitumikia kama mmisionari huko Uingereza na kama rais wa misheni huko Toronto, Kanada
Mzee Jeffrey R. Holland
Wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili
-
Alikuwa mwenza mmisionari wa Mzee Cook huko Uingereza
-
Alifanya kazi kwenye Mfumo wa Elimu wa Kanisa
-
Alikuwa rais wa Chuo Kikuu cha Brigham Young
Mzee Dieter F. Uchtdorf
Wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili
-
Alikuwa mkimbizi mara mbili alipokuwa mtoto
-
Alikuwa rubani wa ndege
-
Hufurahia kuteleza kwenye theluji na watoto wake pamoja na wajukuu
Mzee David A. Bednar
Wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili
-
Alikuwa mlinzi kwenye timu yake ya mpira ya shule ya upili
-
Baada ya kutumikia misheni huko Ujerumani, alimbatiza baba yake kuwa muumini wa Kanisa
-
Alikuwa rais wa Chuo cha Ricks wakati kilipokuwa Chuo Kikuu cha Brigham Young–Idaho
Mzee Quentin L. Cook
Wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili
-
Alipata ushuhuda baada ya kusoma maandiko na kuomba pamoja na kaka yake mkubwa
-
Alimwona mkewe mtarajiwa kwenye onyesho la vipaji katika shule ya upili.
-
Alitumikia kama kiongozi wa Kanisa huko Ufilipino na Visiwa vya Pasifiki
Mzee D. Todd Christofferson
Wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili
-
Alioka mkate wa nyumbani kwa ajili ya familia yake changa
-
Alishiriki katika tamasha la Mlima Cumorah huko New York akiwa kijana aliyebalehe
-
Alifanya kazi kama mwanasheria kabla ya kuitwa kama Mtume
Mzee Neil L. Andersen
Wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili
-
Alikulia katika shamba la kufugia ng’ombe huko Idaho, Marekani
-
Alitumikia kama mmisionari na rais wa misheni huko Ufaransa
-
Anazungumza Kifaransa, Kireno, Kihispania, na Kiingereza
Mzee Ronald A. Rasband
Wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili
-
Alikuwa rais wa misheni huko New York, Marekani
-
Kauli mbiu yake ni “Ni watu ndio wenye umuhimu mkubwa”
-
Aliweka wakfu jengo la kwanza la Watakatifu wa Siku za Mwisho huko Jamhuri ya Cheki
Mzee Gary E. Stevenson
Wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili
-
Alitumikia kama mmisionari na baadaye kama rais wa misheni ya Japani
-
Alianzisha biashara ya kutengeneza na kuuza vifaa vya mazoezi
-
Alitumikia kama askofu wa Kanisa lote
Mzee Dale G. Renlund
Wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili
-
Jina lake la katikati, Gunnar, linamaanisha “askari shujaa”
-
Alihama na familia yake kutoka Utah kwenda Sweden alipokuwa na miaka 11
-
Alifanya kazi kama daktari wa moyo
Mzee Gerrit W. Gong
Wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili
-
Anapenda wanyama, ikijumuisha pengwini
-
Hupenda kukutana na watu katika kila nchi
-
Ana rekodi ya historia ya familia inayorudi nyuma mpaka kwa Dragon Gong wa kwanza miaka 837 Baada ya Kristo.
Mzee Ulisses Soares
Wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili
-
Anatokea Brazil na alitumikia kama mmisionari huko na kama rais wa misheni ya Urusi
-
Alijifunza kuhusu Kanisa pamoja na familia yake kama mvulana mdogo
-
Alianza kujiandaa kwa umisionari alipokuwa na miaka 12