2019
Nitamwona Yeye Tena
Aprili 2019


Nitamwona Yeye Tena

I Will See Him Again

Nilikulia huko Nicaragua. Nilipokuwa mdogo, nilifanya kila kitu pamoja na kaka yangu mkubwa. Tulienda shuleni pamoja. Tulienda dukani pamoja. Tulikuwa na maisha yenye vituko vyote kwenye ua wetu wa nyuma. Tulikuwa wenye furaha.

Kisha, nilipokuwa na miaka tisa, jambo la kuhuzunisha lilitokea. Kaka yangu alifariki kwenye tetemeko la ardhi. Mwanzoni haikuonekana halisi kwamba hakuwepo. Niliwahi kudhani kwamba angebisha kwenye mlango wetu wa mbele. Angetuambia kwamba alikuwa mbali mahala fulani. Niliwahi kuduwaa mlangoni, nikitamani hilo litokee. Nilitaka sana kumuona tena.

Baada ya muda, ilikuwa kidogo angalau. Bado niliendelea kumkosa kaka yangu, lakini niliweza kuhisi furaha tena.

Wakati huo, sikuwa muumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Lakini nilipokuwa mkubwa, nilijifunza kuhusu Kanisa na kubatizwa. Siku moja nilikuwa nikiosha vyombo vyangu. Ilikuwa ni wakati wa Pasaka. Nilikuwa nikifikiria juu ya Ufufuo na kumfikiria kaka yangu.

Ghafla hisia iliniijia. Nilikumbuka ndoto ya mchana niliyokuwa nayo kuhusu kaka yangu. Niligundua kwamba haikuwa ya kipuuzi hata kidogo! Ilikuja kutoka kwa Roho Mtakatifu, kunifariji na kuniongoza. Siku moja kaka yangu kweli atafufuka. Na nitamwona tena.

Ikiwa mtu unayempenda amefariki, ni SAWA kuwakosa na kuhisi huzuni. Zungumza na familia yako au mtu mzima unapohisi uko tayari kufanya hiyo. Omba kwa Baba wa Mbinguni kuhusu jinsi unavyohisi. Anaweza kukusaidia kuhisi amani tena.

Katika hali yoyote, kumbuka kwamba Yesu Kristo anakupenda. Wakati wa Pasaka tunakumbuka dhabihu Yake kwa ajili yetu. Kwa sababu Yake, sisi sote tutafufuka na tunaweza kuishi na familia zetu milele. ●

Kadi za Faraja

Kata na uondoe kadi hizi. Ungeweza kuzikunja katikati au kuzitumia kwa kuweka alama kitabuni. Zitunze katika maandiko yako au mahali pengine ili uweze kuzitazama wakati unapohisi huzuni, upweke, au woga.

“Sitawaacha ninyi yatima: Naja kwenu.”

Yohana 14:18

“Naye atafuta kila chozi katika macho yao.”

Ufunuo 21:4

“Changamkeni, na msiogope, kwani Mimi Bwana nipo pamoja nanyi, na nitasimama karibu yenu.”

Mafundisho na Maagano 68:6