2019
Reykjavík, Iceland
Aprili 2019


Kanisa Liko Hapa

Reykjavík, Iceland

reykjavik

Ukiwa na Mlima uliofunikwa na‑theluji katika upande wa nyuma, Reykjavík, mji mkuu wa kupendeza wa Iceland, unatoa ukaribisho kwa taifa la kisiwa zaidi ya maili 1,000 (1,609 km) kutoka bara la Ulaya. Awali ukikaliwa na Maharamia wa Scandinavia mnamo 874 BK, Reykjavík ni kitovu cha utamaduni, uchumi, na shughuli za kiserikali za Iceland, vilevile moja ya majiji masafi, ya kijani, na yenye usalama ulimwenguni.

Wakazi wawili wa kwanza wa Iceland walibatizwa huko Denmark mnamo 1851. Baada ya muda mfupi walirudi Iceland, na mnamo 1853 tawi la kwanza lilianzishwa. Leo kuna takribani waumini 300 katika Iceland katika matawi matatu, katika Reykjavik, Akureyri, na Sellfoss. Hekalu la karibu liko London, England, maili 1,177 (1,894 km) kutoka Reykjavík.

Ingawa idadi ya waumini ni ndogo, Kanisa linaendelea kukua. Licha ya changamoto za kutengwa, tafsiri ya nyenzo za Kanisa, hali ya hewa isiyo rafiki, na vikwazo vya kiutamaduni, viongozi wa Kanisa wameahidi kwamba siku moja Iceland itakuwa mfano kwa nchi zingine. Rais Gordon B. Hinckley (1910–2008) alizuru Iceland na kuwakumbusha waumini kwamba wao ni “watu ‘imara na wenye nguvu na uwezo’ wa kufanya mambo makubwa” (“Inapendeza kuwa na Nchi ya kuvutia, nchi Nzuri,” Habari za Kanisa, Sept. 21, 2002, 10).

  • Misheni ya Iceland ilianzishwa mnamo 1894, lakini ufundishaji wa injili ulisitishwa mnamo 1914. Iceland ikawa sehemu ya misheni ya Denmark Copenhagen mnamo 1975.

  • Mnamo 1977, Mzee Joseph B. Wirthlin (1917–2008), wakati huo akiwa mshiriki wa Akidi ya Kwanza ya Sabini, aliiweka wakfu rasmi Iceland kwa ajili ya kuhubiri injili.

  • Mnamo 1981 Kitabu cha Mormoni kilichapishwa katika lugha ya Iceland—lugha ambayo haiongelewi kokote ulimwenguni.