Kutoka kwa Urais wa Kwanza
ZawadiKuu ya Mungu
Kutoka “Shukrani Ziwe kwa Mungu,” Liahona, Mei 2012, 77–80.
Siku moja mimi na Dada Nelson tuliona samaki wa kitropiki kwenye bwawa la samaki. Samaki wenye rangi za kung’aa na maumbo na ukubwa tofauti walienda mbele na nyuma. Nilimuuliza mfanyakazi aliyekuwa karibu, “Nani huwalisha samaki hawa wa kupendeza?”
Alijibu, “Mimi.”
Kisha niliuliza, “Je, samaki wamewahi kukushukuru?”
Alijibu, “Bado!”
Baadhi ya watu ni kama samaki hao. Hawamtambui Mungu na wema Wake kwao. Ingekuwa vema kiasi gani ikiwa tungejua zaidi juu ya upendo wa Mungu na kudhihirisha shukrani Kwake.
Shukrani kwa ajili ya Yesu Kristo.
Mungu alimtuma Mwana Wake, Yesu Kristo, kutusaidia. Alifanya hivyo kwa sababu anatupenda sana.
Yesu Alikuja kutukomboa.
Kwa sababu ya Upatanisho Wake, tunaweza kufufuka baada ya kufa.
Kwa sababu ya Upatanisho Wake, tunaweza kurudi kuishi na Baba wa Mbinguni milele.
Yesu alielezea:
“Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima: Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi: Naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele (Yohana 11:25–26).
Huu ndio ujumbe wa kupendeza wa Pasaka. ●
Yesu ni Mwokozi Wangu
Yesu alifufuka asubuhi ya Pasaka. Soma sentensi kujua kile Yeye alichofanya kwa ajili yetu. Paka rangi mwale wa jua baada ya kusoma kila sentensi. Kisha paka sehemu iliyobaki ya picha.
-
Yesu aliteseka Gethsemane na pale msalabani kutuokoa kutokana na dhambi zetu.
-
Yesu alikufa na kufufuka ili kutuokoa kutokana na kifo.
-
Yesu alitupatia sakramenti ili kutusaidia sisi kumkumbuka Yeye.
-
Yesu Kristo alitufundisha kuwasamehe wengine.
-
Yesu alituonyesha jinsi ya kuwa wakarimu.
-
Kwa sababu ya Yesu, sote tutafufuka baada ya kufa.