“Inamaanisha Nini Kuitwa na Bwana?,” Liahona, Machi 2023.
Njoo, Unifuate
Inamaanisha Nini Kuitwa na Bwana?
Katika Mathayo 10, Mwokozi anawatawaza Mitume Wake kumi na wawili, akiwapa uwezo, mamlaka na maarifa ya kuanza kuihubiri injili Yake na kuanzisha Kanisa Lake. Aliwaahidi pia uwezo wa kuponya, kutoa pepo na kuzungumza kwa mamlaka (ona mistari ya 1, 20). Unaposoma katika Mathayo 10 kuhusu Bwana akiwaandaa Mitume kwa ajili ya miito yao, zingatia jinsi Bwana alivyokuandaa kwa ajili ya huduma Kanisani.
Ushauri kutoka kwa Bwana
Bwana pia aliwapa Mitume baadhi ya maelekezo muhimu ambayo yangewasaidia na kuwaidhinisha katika huduma yao. Mengi juu ya ushauri huu yanaweza pia kutumika kwetu katika huduma yetu. Unaposoma mistari ifuatayo katika Mathayo 10, tilia maanani maelekezo na mialiko ambayo Bwana aliwapa.
-
Mstari wa 8:
____________________
-
Mstari wa 19:
____________________
-
Mistari 29–31:
____________________
-
Mstari wa 39:
____________________
Unapokuwa umeitwa kutumikia ndani ya Kanisa, Bwana atakusaidia uifanye kazi Yake. Atakubariki kwa uzoefu, maelekezo na ufunuo. Utatengwa na kupokea mamlaka kutoka kwa Mungu ili kutimiza wito wako.
Unaweza kujifunza mengi zaidi kuhusu majukumu ya wito wako kwenye Kitabu cha Maelekezo ya Jumla kwenye ChurchofJesusChrist.org.