“Mwokozi Anawezaje Kunisaidia?,” Liahona, Machi 2023.
Njoo, Unifuate
Mwokozi Anawezaje Kunisaidia?
Yesu Kristo, “alizunguka huko na huko, akitenda kazi njema” (Matendo ya Mitume 10:38): Alimponya mwenye ukoma (ona Mathayo 8:2–3). Alimponya mtumishi wa akida, ambaye hakuhisi kustahili lakini aliamini Mwokozi angeweza kumsaidia tu (ona Mathayo 8:5–13). Alitoa amani kwa wanafunzi Wake wakati wa dhoruba (ona Mathayo 8:23–27). Alipomwona mwanamke aliyehuzunishwa kwa kifo cha mwanaye wa pekee, alimfariji na kumpa tumaini, kisha alimfufua mwanaye kutoka wafu (ona Luka 7:11–15).
Shughuli
Tunaweza kuuhisi uwezo wa Mwokozi leo pale tunapoonesha imani Kwake. Soma moja ya matukio kutoka kwenye usomaji wa Njoo,Unifuate wa wiki hii. Tilia maanani jinsi Mwokozi alivyoitikia mahitaji na imani za watu.
Tafakari au jadili maswali yafuatayo ili kuzingatia jinsi ambavyo Mwokozi amekusaidia katika maisha yako:
-
Ni lini nimeweka imani yangu katika Mwokozi na kuhisi uponyaji Wake (kihisia, kiakili, kiroho au kimwili)?
-
Ni lini nimehisi amani Yake?
-
Ni lini nimepokea usaidizi ambao sikuutarajia kutoka kwa Mwokozi?
-
Ni lini nimeuona mkono Wake kupitia muujiza au huruma nyororo?
-
Kwenye maisha yangu sasa, ninawezaje kuimarisha imani yangu Kwake na kupokea usaidizi Wake?