Misaada ya Kujifunza
21. Bonde la Yezereeli


21. Bonde la Yezereeli

picha 21

Ukiangalia kuelekea kusinimagharibi kutoka kilele cha Mlima Tabori kuelekea katika sehemu ya Bonde la Yezereeli ambalo pia hujulikana kama Uwanda wa Esdraloni. Ingawa Bonde la Yezereli mara nyingine watu hudhani kuwa ni bonde kuu, kwa kweli ni mlolongo wa mabonde ambayo huungana na Nyanda za Ako pamoja na Bonde la Yordani na eneo la Bahari ya Galilaya. Bonde la Megido, kwa mfano, ni sehemu ya magharibi ya bonde hili. Bonde la Yezereeli lilikuwa ni njia kuu katika Nchi Takatifu kati ya Bahari ya Mediterania kwenda magharibi na Bonde la Yordani upande wa mashariki.

Matukio Muhimu: Barabara kuu iunganishayo Misri na Mesopotania ilipita katika bonde hili, na vita vingi vilipiganwa hapa (Amu. 1:22–27; 5:19; 2 Fal. 23:29–30). Pambano kuu la mwisho katika nchi hii litaanzia kwa vita vya Armagedoni, ambavyo vitapiganwa muda mfupi kabla ya ujio wa Pili wa Mwokozi, vimechukua jina kutoka kwa Har-Megidoni, au Mlima wa Megido (Eze. 38; Yoe. 3:9–14; Zek. 14:2–5; Ufu. 16:14–16).